Ndugu zangu watoa ushauri tunawashukuru saana. Binafsi nimefarijika kuwaona mpo nasi hapa kutusaidia namna ya kupenya. Asanteni kwa hilo
lusungo izzo na wengineo. Niseme tu kwa maelezo yenu kutoka nje na kufanikiwa kupata paper sio kazi nyepesi kama wengi tulivyokuwa tunategemea au tulivyoaminishwa na maagent tuliokutana nao. Labda walitaka tuwape pesa then turudishwe airport turudi bongo tuendeleze hii hali ngumu.
Najua bado mnaendelea kutushauri njia za kupita ila naomba nitoe changamoto zinazotugharimu sisi kama wahitaji msaada. Binafsi ningeshakuwa Scandinavia siku nyingi maana mipango nilianza kitambo since 2015. Lakini nilikosa miongozo nilijua ni sawa na kwenda kenya tu maana nimekaa kaa kenya. Ok Nikianza na njia ya kwanza ya
izzo ya malta changamoto zake hizi hapa kwa sisi waendaji....
1. Kupata host agent wa kuaminika. Kama mnavyojua kuna maagent wazinguaji kama kina britanicca binafsi alitaka kunipiga nikamgundua mapema. Maagent tunaokutana nao wanamilolongo mingi hawapo serious hasa wa bongo. Laiti kama tungewapata maagent watushughulikie visa na sehemu ya kufikia kwa muda hukk nchini malta tungejilipua hata kuanzia kesho au kesho kutwa. Lakini maagent wengi ni wa Asia countries kama oman, Qatar, dubai n.k
2. Ni namna ya kupata visa na namna ya kuendelea kuishi ukishafika nchi ya watu. Kama mnavyojua visa zinataratibu zake za kuipata. Na rahisi ni tourist kwa malta kwa mtu kama mim niliye na passport tu. unakuta unayo passport na vipesa vyako vipo mkononi. Suala linakuja sasa je uombe visa ya tourist ama! Na ukishaipata ukifika malta utumie mbinu gani kuishi maana visa ikiisha utaishi maisha ya shida ya kukimbizana na polisi na hatimaye utarudishwa kama
izzo alivyosema. Tukija kwenye mtu wa kukuinvite.. huko malta unakuta hauna mtu na ukisema ukae hotelini au upange huku ukiwa na tourist visa mpaka umalize miezi si utakuwa unatumia kiasi kikubwa cha pesa ambacho kitashindikana kukimudu ukitegemea haufanyi kazi maana aina ya visa haikuruhusu! Binafsi hii ni changamoto maana njia ya malta Nimeipenda saana. Hapa mtu ukipata invitation inakuwa ni rahisi kidogo. Na bado akikuinvite muda si utaisha? Je paper zitapatikanaje?
3. Kuna suala lingine hili la ndoa au uchumba mmeliongea saana lakini sio simple brethren kihivyo. Online dating ni kazi saana hata mtu wa nje kukujibu text au call yako ni kazi. Sometimes ni kubahatisha. Je na visa yake ipoje inahitaji criteria gani? ni mbinu gani zingine kuwakamata hawa watu? Kwenda na tourist visa ukiwa na lengo la kuhook kwa lifemate ya visa yako? Je ukikosa! Ingawa kwenye kutafuta tunatake risk ila tunatakiwa kujiuliza hayo maswali. Ukikosa kwa huo muda si itakuwa ni kazi bure! !.
Halafu
izzo naomba utoe ufafanuzi juu ya hiyo visa ya uchumba. Inapatikana kupitia criteria zipi.