Huu uzi ni kati ya nyuzi bora kabisa kupata kuanzishwa hapa JF. Nimekua nao toka page ya kwanza nikilike kila kilichonivutia, ubarikiwe ndugu Lusungo hakika return ya ulichokifanya itakuwa kubwa sana ni suala la muda tu.
Kuna sehemu nacheka sana kama comments za mkuu Wonderful, una namna ya kuwafanya watu watabasamu, ubarikiwe.
Kuna sehemu hadi machozi yamenitoka kwenye Comments za mkuu Kaveli, you are such a wonderful creature, mkweli, muwazi, sio fake (kama watu wamefuatilia comments zako kwenye nyuzi mbalimbali humu JF). Hakika you have my all prayers, Yule unayemuamini akupiganie katika kile chema unachokitaka maishani mwako. Halafu nimeupenda uandishi wako, kudos.
Mkuu Izzo uwepo wako ni ushahidi wa kuwa waTanzania bado wapo wenye roho nzuri sana, umekuwa msaada kwa wenzetu wengi wenye nia yakwenda nje kusaka maisha katika mtazamo mwingine.
Pia Mbarikiwe wachangiaji wote mliotoa miongozo, misaada, changamoto, na taarifa mbalimbali kuhusu nchi za wenzetu, mmpanda mbegu bora kabisa, jueni kuwa hamjaupoteza muda wenu bure. Kila la heri wote mnaofanya michakato yakuzama nchi za nje, wenye nia njema wote Mungu awaongoze.
Mwisho, kwenye kuhost hapo kama kuna mgeni anatakuwa interested kuja kanda ya kati (Dodoma) naomba nipewe nafasi, malazi yapo sehemu salama kabisa. Nina imani atakuwa salama.