Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Barua ya mwaliko au offer ya chuo ndiyo msingi wa safari yako ya matembezi au kwenda masomoni.

Tiketi ya kwenda na kurudi (kwa matembezi) ni jambo la pili na la msingi.
Kwa mfano nikiwa na tiketi.naenda Zambia.Nina passport. Wataniuliza ticket ya kwenda na kurudi?
 
Aisee, jamaa alikuwa fighter sana. Ila kwa sasa hali ya usalama ni mbaya especially middle east. Unless u-force kuvuka Mediterranean kama jamaa wa Libya na syria wanavyofanya. Ukiumbwa mwanaume ni kupambana...

Indeed!
Kumbuka wakati ule rebels wakiongozwa na John Garang walikuwa wakipigana na serikali ya Sudan na jamaa alisema alikamatwa na askari wa sudan katikati ya Juba na Kartoum na aliwekwa ndani for several days kabla hajaachiwa. Alidiriki kusema kuna wakati alikaa na njaa kwa siku 3 akishindia maji ya kunywa tu
Maisha ni kupambana
 
Rais John Magufuli akiwa ktk ziara Mtwara amesema ni sawa tu kwa Serikali ya Msumbiji kwa kuwafukuza wahamiaji haramu.

Na amewataka watanzania warudi tu nyumbani kuna kila kitu ili tujenge nchi yetu.

Na ulivyokwenda ndivyo utakavyorudi kwasababu Serikali haikukupeleka Msumbiji na hata usafiri wanaopewa hauna sababu kwa sasa.

Amemshanga mtanzania kutoka Shinyanga kwenye dhahabu kwenda kuchimba madini Msumbiji.

Msumbiji ni marafiki wa Tanzania na wahamiaji haramu wasisababishe kuharibu mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Nini hichi umeandika!?
 
Napata jaziba sana naposikia maneno kama haya kutoka kwa Rais wa nchi...badala ya kuwatetea watu wake yeye ndo anawachuuza...! Sasa huyu Rais wa kazi gani sasa? anakera sana ...
Mkuu unategemea nini kutoka kwa raisi huyu tulie nae kwenye inshu kama hiyo. Saana ni maudhi tu kama hayo.

Wewe raisi mwenyewe hata swala kutoka nje ya nchi kwake ni anasa ndio aje atetee wanyonge walionda nje kutafuta ridhiki.
 
Mkuu unategemea nini kutoka kwa raisi huyu tulie nae kwenye inshu kama hiyo. Saana ni maudhi tu kama hayo.

Wewe raisi mwenyewe hata swala kutoka nje ya nchi kwake ni anasa ndio aje atetee wanyonge walionda nje kutafuta ridhiki.

Kutoka nje kwa riaisi wa nchi ni anasa?
 
Mkuu unategemea nini kutoka kwa raisi huyu tulie nae kwenye inshu kama hiyo. Saana ni maudhi tu kama hayo.

Wewe raisi mwenyewe hata swala kutoka nje ya nchi kwake ni anasa ndio aje atetee wanyonge walionda nje kutafuta ridhiki.
Inasikitisha sana. Ila muda siyo mrefu, passport yao nitaitupa kwenye dust bin
 
...kama we ni heath personnel..basi tafuta nafasi za masomo ya juu ng,ambo..ndio njia pekee na rahisi ya kukutoa ambayo hata lusingo amegusia kwenye Uzi wake...


mulemule kumbe afya ndio dili ee ngoja nami nitasogea huko mkuu tujumuike wote nisaidie tu barua ya mwaliko niwe kama mgeni wako nikija nakuachia fungu kidogo natafuta njia yangu nami yakutokea by the way nami ni health personal.
 
Mshkaji mwingine hadi naandika haya yupo Nogales, Mexico akisubiri mvushaji ama maarufu kwa jina la COYOTE amvushe boda kumwingiza USA
Kwa kifupi alipanda ndege from Dar to Adis then from Adis to Rio de Janeiro. From Rio alienda Mexico City na sasa yupo Nogales mji ambao upo kwenye border ya Mexico na US akisubiri kuwa-smuggled into US
Anasema hapo transit Nogales kuna mafuriko ya watu toka Latin America, west Africans na Asians wakisubiri kuvuka boda kuingia US
Mungu ambariki atimize ndoto yake
Bro u sound very innocent

I like your attributes unaonekana shule ipo pia.

You have a good heart too.

Keep it up n god bless u
 
Hao wachina wenyewe wamezamia hapa kwetu wapo kariakoo wanauza ubuyu na popcorn so ukienda kwao imekula kwako.
Inategemeana. kuna kijana tunatoka kijiji kimoja (Ingawa niliwaacha wakiwa bado watoto wadogo) ameenda china and it seems maisha siyo mabaya. huko anamiliki saloon na business zingine. huwa tunachart kwenye hizi social media...so, inategemeana na jinsi ya kukabiliana na ugumu/risks...
 
Ndugu wana JF
Kwa muda mrefu kumekuwa na masuala mbalimbali yahusuyo kujilipua (kwenda nje ya nchi) ambayo watu wanauliza mmoja mmoja kwa lemgo la kutaka msaada na ushauri namna ya kufika na jinsi ya kuanza maisha huko nje.

Kutokana na kutoa msaada kwa wengi (binafsi) kwa kutumia njia binafsi nimeona nifungue uzi huu ili kuweka mambo yote wazi kwa kadiri itakavyowezekana na kualika wengine pia waweze kutoka maoni yao.

Ndugu zangu nchi yetu ya Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini.

Nchi masikini wenzetu huko mbele raia wao wamejaa haswa kutokana na moyo wa kusaidiana na kuvutana.

Nimeamua nilete hoja hii kama ambavyo wenzetu hufanya huko Nairaland ya Nigeria ili kila mtu mwenye ujuzi au ufahamu juu ya namna ya kutoka (kujilipua) atoe msaada kwa wengine kwenda huko... si lazima wewe binafsi usaidie mtu binafsi NO, hata mbinu tu za jinsi ya kufika huko.

Kabla sijaingia kwenye kiini cha mada naomba nitoe faida na changamoto za kujilipua.

FAIDA
1. Fursa nzuri za kiuchumi na kujiinua hasa ukiwa na malengo.. Wakuu binafsi nimeishi Marekani kwa miaka nane. moja ya faida nilizopata huko ni kujiinua kiuchumi.... binafsi wakati naenda kusoma huko nilijiwekea malengo ya kujenga ghorofa nyumbani, kufungua mashine za kusaga na kukoboa nafaka pamoja na kumiliki fuso za mizigo...

kipato cha mfanyakazi wa kule ni kikubwa mno kushinda hata cha baadhi ya maboss wetu hapa... hivyo nilijitahidi nilipokuwa kule malengo yangu yaimie... ni kweli baada ya muda huo nilifanikiwa kutimiza yote.

2. Huduma nzuri za afya, Elimu, Sheria, miundombinu.

CHANGAMOTO
1. changamoto kubwa kwa kuwa kule ni upweke (ku feel home mara kwa mara japo wakati mwingine ukizoea hutoweka)

2. Xenophobia hii ni kwa baadhi ya nchi tu sio zote.

USHAURI WA WAPI UENDE NA NAMNA GANI UENDE
Kwa wale wahitaji wa masuala ya maisha kujijenga na kuchuma nashauri nchi hizi, USA, UK, NORDIC COUNTRIES, NA WESTERN EUROPE COUNTRIES. kwa Afrika nashauri SA.

Jinsi gani utaenda namna ni nyingi.... naorodhesha baadhi hapo chini...
1. kwenda kimasomo ambapo unaweza tafuta sponsors then ukapata scolarship itayokuwezesha kupata visa na kujilipua huko baada ya masomo...

2. Kutafuta mwenzi wa nje ambaye atakualika huko kisha mtaoana na kukuwezesha kupata resident permit na baadae uraia.

3. Kuhamisha mataji na biashara njia hii unakubaliwa popote alimradi uwe na biashara halali,

4. kwenda kwa shughuli za utamaduni

Wenzetu wakenya na wanigeria wameunda mfumo wa kualikana wao kwa wao, kwamba mtu anakutumia barua ya mwaliko, then unakwenda ukifika huko anakutafutia mtu mnaoana kisheria tu ili upate karatasi kisha kila mtu anasika hamsini zake....

Wapendwa mambo ni mengi siwezi andika yote ndio maana nimeanziasha uzi huu tutaendelea kujuzana kwa kairi michango ya watu itakavyokuwa na maswali yatayojitokeza.

Nawakaribisha wafuatao: BAK kui Isanga family Sky Eclat


Matola MziziMkavu Copenhagen DN Ng'wamapalala Pascal Mayalla Nyani Ngabu rev kishoka Bavaria FaizaFoxy farkhina MfalmewaKiha mwandende Slim5

Na wote wenye maujuazi au mauzoefu ya huko mbele... karibuni tusaidiane tujenge taifa letu... Tuwasaidie vijana wakasake fursa.
Mkuu bado na wait jibu lako nahitaji unisaidie njia nyepesi ya kupata passport.
 
Kuna nchi inaitwa lithuania naona wa Nigeria wana recommend sana kwenda maana hawana longo longo hasa kwa wale wanao enda kusoma Degree na kuendelea. Maana nchi nyingi wanataka ufanye test zao zile za Teofel so hawana kuna kozi kibao nzuri. Mimi ndio nataka nipitie Huko. Hapa na jichanga kwanza mpk October nitajua mbivu na mbichi.

Lithuania uchumi wao ni mbaya saana,hata wao wanapambana kukimbilia nchi nyingine,chuo utapata lkn kazi hazipo,nisawa na Spain choka mbaya huko .au Italy,romania bora ya Tanzania
 
Nyani Ngabu usibanie michongo ya kutimkia huko[emoji1]

Faiza Fox toa michongo ya Canada

BAK toa michongo ya US

Kimweri lete ushauri
 
Lithuania uchumi wao ni mbaya saana,hata wao wanapambana kukimbilia nchi nyingine,chuo utapata lkn kazi hazipo,nisawa na Spain choka mbaya huko .au Italy,romania bora ya Tanzania

Italy choka mbaya??
 
Lithuania uchumi wao ni mbaya saana,hata wao wanapambana kukimbilia nchi nyingine,chuo utapata lkn kazi hazipo,nisawa na Spain choka mbaya huko .au Italy,romania bora ya Tanzania
Ila ndio nasikia ndio njia pia rahisi ya kuingia ulaya.
 
Bro u sound very innocent

I like your attributes unaonekana shule ipo pia.

You have a good heart too.

Keep it up n god bless u
Daa! jamaa umemuremba wewe au unataka akushike mkono ee 😛😛😛😛 nakutania bro usipanic
 
Ahaha... Utashitakiwa na jamhuri mkuu
Hapana mkuu! nikishapata citizenship ya nchi nyingine, uraia wa tz una cease automatically. Btw, napata shida kurudi ku-rew passport inapoisha ama kujaa...
 
Back
Top Bottom