Wakuu Mimi nimepata manzi kutoka USA, Bahati nzuri katika kuchati na kuongea kaniambia anakuja Tanzania kutalii na anataka kujifunza Kiswahili pia anapenda Africa. Yeye Ni Black Amerika.Mpaka sasa tupo kwenye mahusiano.
Sasa naomba mnipe abcd na mawazo kupitia yeye niweze kuingia US.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Nitakuelezea kwa uelewa wangu na mwisho nitavaa uhusika wako.
Kwanza, Tu-assume sio tapeli ni mdada mwema kabisa. Lengo lake yeye ni kuja kutembea Afrika ajifunze kiswahili na kukuona wewe boyfriend wake.
Ila wewe lengo lako ni kumtumia kuingia USA.
Nitajitoa ufahamu hapa.
Sio wewe wa kwanza kuwatumia hawa watu kuingia nchi zao ni watu wengi tu wamefanikiwa kwa hili.
Kikubwa akupende wewe na asiwe choka mbaya, hapa utafanikiwa. Kupendwa naye ni pagumu kueleza...maana kila mmoja anapenda kivyake. Ila kikubwa hawa watu mwonekano na uwazi.
Black sio wazungu ni waafrika wanaoishi ulaya hivyo uzungu kwao sio kivile. Kwa hiyo usitarajie mengi kutoka kwake...ila kama angekuwa mzungu ungetarajia mengi.
ok...
Utamtumia kuingia hasa hasa kwa kutembea. hapa kuna mawili utapewa visa au usipewe.
Bahati nzuri Ukipewa.
Utaenda kumtembelea kama alivyokuja kukutembelea. Kama una roho ngumu Utamtoroka unakuwa umeshachora ramani huku. Hapa lazima uwe na mtu huko uendako maana huwezi ukamtoroka demu ukaingia mtaani pasipo na sehemu ya kwenda. [Sishauri ufanye au usifanye]
Upande wa pili
Mahusiano yenu yanaweza kuwa mazuri mkapanga kuoana. Hapa uwanja ni mpana maana utafuata sheria na utaishi kwa kujitawanja. Tatizo la hapa patachukua muda mrefu na mnaweza kuachana hata kabla ya kuprocess chochote.
-Njia zingine ni ndogo ndogo kama kumtumia akutafutie scholarship. n.k