Ushauri: Maswala ya Elimu yote kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vya ualimu yawe chini ya Wizara ya ELIMU, TAMISEMI wapunguziwe mzigo.

Ushauri: Maswala ya Elimu yote kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vya ualimu yawe chini ya Wizara ya ELIMU, TAMISEMI wapunguziwe mzigo.

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Husika na kichwa habari hapo juu;
Nashauri, masuala yanayohusu Elimu nchini yashughulikiwe kipekee zaidi kuanzia usimamizi na uratibu wake.

Hivyo basi: nashauri wizara ya Elimu iwe ndo mratibu mkuu wa shughuli zote za Elimu nchini kuanzia halmashauri mpaka Taifa, na vibao vyote vya shule viandikwe wizara ya Elimu, sayansi na Teknolojia badala ya TAMISEMI.

Kule halmashauri kuwe na ofisi ndogo za wizara ya Elimu ambazo zitashugulikia Maswala ya ualimu, ofisi hizo ziwe na;
1. Afisa Elimu
2. Mtaaluma
3. Afisa utumishi wa wizara ya Elimu.

NB: Mambo ya Elimu ni Maswala nyeti ni vyema utekelezaji wake usiwe na mgawanyiko gawanyiko, kwa mfano: kwasasa shule zote za msingi zipo TAMISEMI lakini vyuo vyote vya ualimu vipo wizara ya Elimu, tufanye shule na vyuo vyote viwe chini ya Wizara ya ELIMU sayansi na Teknolojia.

KAZI IENDELEE
 
Back
Top Bottom