Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Moja ya njia za kutatua mgogoro ni Kuondoa uongozi mbovu. Ndio maana ninamuomba Mbowe astaafu.
 

Sina Jambo lolote. Msimamo wangu ni kwamba Mbowe kajuta kumwamini Samiah, na alionywa Sana. Fuatilia hotuba ya Diaspora aliyoitoa. Sasa leo atasemaje kwamba aliingizwa kingi na Samiah?. Huo ni ujinga. Unalazimisha Jambo ukifeli inaanza kulalamika.
 
Usiweke imani yako kwa mwanasiasa kwa sababu hoja zozote unazokuwa unazisikia huwa scripted...

Huwa wanaongea au kutenda vitu fulani wakiwa na lengo fulani kwa manufaa yao kisiasa...

Hizo kauli za Mbowe zina "huenda" nyingi mno...
 

Wewe ndio unachekesha. Unaniuliza ni lini CHADEMA imeizidi CCM akili halafu unataka Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti. Yani unakubali CHADEMA haijawahi kuizidi CCM akili na unataka huyo kiongozi aliyezidiwa akili Miaka yote na CCM aendelee kuwa Mwenyekiti.

Ndio maana nikasema kwasababu Mbowe kaonekana kuzidiwa akili na CCM muda wote, aakae pembeni tafadhali.
 

Tatizo lako unakwepa ukweli. Akina Lissu walimuonya mapema akawakatalia na hata kuwananga kwenye mkutano wake wa Diaspora, Leo baada ya kufeli ndio anakiri aliingizwa mtegoni. Yani angekubali ule ushauri kipindi kile Cha Mwanzo hakuna ambaye angemlaumu, ila kitendo Cha kukataa ushauri na Kuja kufeli baadae kina discredit Mbowe mazima.

Angesikiliza ushauri wa akina Lissu asingekuwa anatulilia kijinga. Ni kwamba Mbowe alikataa ushauri, Sasa Leo anamlilia nani? Aende huko.
 
Aisee! Watu walimtaka Mbowe aweke wazi anaongea nn ktk maridhiano, lkn yeye akafanya siri. Sasa inamtafuna.

Kwa maoni yangu Mbowe akubali kuwajibikq kwasabb plan yake hii imefeli.

Na hii ndio point yangu. Unajifanya busy na Jambo kana kwamba ipo serious, ukiulizwa unafanya Siri. Ikija kufeli unaanza kulilia watu. Mbowe must go.
 
Una hoja usikilizwe
 
Aisee! Watu walimtaka Mbowe aweke wazi anaongea nn ktk maridhiano, lkn yeye akafanya siri. Sasa inamtafuna.

Kwa maoni yangu Mbowe akubali kuwajibikq kwasabb plan yake hii imefeli.
Nadhani kuweka siri ilikuwa ni sharti la maridhiano. Hakuna Reconciliation inaanz ana uwazi kwa sababu kuna mambo mazito yanaongelewa humo.
 

Naona umerukia juu bila kusoma nilichokiandika. Kasome Historia yangu, sijawahi kuwa mwanacc na sitawahi. Nachokushauri Usipende kuzima mawazo ya watu kisa wanamkosoa Mbowe. Huyo Mbowe alituaminisha kwenye mkutano wa Diaspora marekani kwamba atahakikisha maridhiano yanafanikiwa na akawapinga waliokuwa wanamkataza kuhusu hayo maridhiano na hata alipoulizwa wanajadili Nini akadai ni Siri. Leo inakuwaje Tena anarudi kwa wanachama na kulia ametapeliwa?

Nyie endeleeni kumlamba miguu Mbowe mkidhanu mnamsaidia, ngoja akipeleke chama shimoni ndio mtaelewa. Amekifanya chama kisiwe na msimamo. Leo maridhiano, kesho maandamano, keshokutwa maridhiano etc. Tuwe na msimamo Kama chama la sivyo tutakuwa predictable kwa CCM kama Sasa hivi mama kashapata alichokitaka.
 
Usiweke imani yako kwa mwanasiasa kwa sababu hoja zozote unazokuwa unazisikia huwa scripted...

Huwa wanaongea au kutenda vitu fulani wakiwa na lengo fulani kwa manufaa yao kisiasa...

Hizo kauli za Mbowe zina "huenda" nyingi mno...

Sijawahi kuweka imani kwa kiongozi Bali imani yangu ipo kwenye Chama Cha CHADEMA
 
Huu ndio wakati wa Mbowe kujenga heshima yake isije kupotea Kama akina Mrema na Lipumba. Astaafu kwa heshima. Pia ni wakati wa CHADEMA kuleta fresh minds na fresh approach ya kuikabili CCM. Ila tukiendelea kuleta ujinga mwisho hautakuwa mzuri.
 
Huu ndio wakati wa Mbowe kujenga heshima yake isije kupotea Kama akina Mrema na Lipumba. Astaafu kwa heshima. Pia ni wakati wa CHADEMA kuleta fresh minds na fresh approach ya kuikabili CCM. Ila tukiendelea kuleta ujinga mwisho hautakuwa mzuri.
acha upotoshaji yaani chadema kuna fresh mind 🀣 tsaaatsaahhhaaa....πŸ’
 
Sijawahi kuweka imani kwa kiongozi Bali imani yangu ipo kwenye Chama Cha CHADEMA
kumbe ndio maana una imani haba, potofu na mtazamo hasi sana kwa kila jambo iwe limefanywa chadema au CCM? πŸ’
 
unavyomlamba miguu Lusu atakupeleka wap, nothing new at all πŸ’
 
Moja ya njia za kutatua mgogoro ni Kuondoa uongozi mbovu. Ndio maana ninamuomba Mbowe astaafu.
mawazo yako ni mazuri na huru, lakini hayatekelezeki kutokana na historia yako binafsi ya nyuma na historia ya unaowalamba miguu eti ndio watake over chadema πŸ’

never ever πŸ’
 
Huu ndio wakati wa Mbowe kujenga heshima yake isije kupotea Kama akina Mrema na Lipumba. Astaafu kwa heshima. Pia ni wakati wa CHADEMA kuleta fresh minds na fresh approach ya kuikabili CCM. Ila tukiendelea kuleta ujinga mwisho hautakuwa mzuri.

1. Ikumbukwe kina Putin, Medvedev na sasa Trump (yuko njia moja) waliwahi kushika hatamu wakatoka na baadaye kurudi.

2. Mtu unaweza ukatoka ukarudi ukipenda ukiwa fresh na mawazo mapya. Ndiyo maana kuna likizo, rest and recuperation, sabbatical leave, nk.

3. Kukaa kiti kile kile muda mrefu inaweza kumpa mtu chronic fatigue na bila kujitambua akabweteka.

4. Leo chadema ina chawa na vijana wa hovyo kama wale wengine.

5. Hapo #4 hata nidhamu na heshima imekuwa changamoto.

6. Hapo #5 si ajabu illiterates na hata vijiweni na mitandaoni kuwakuta wanamzodoa Shivji, Nyerere, Mandela, Tutu, Lissu nk kiboya boya, kwa uchawa wao tu bila kujali jitihada, michango au mafanikio ya watu kama hao duniani, kwa jina la chama.

7. Kina Nanye Go na wenzao wengi ni mfano wa watu hao ambao bila ya uhalali wowote, si nadra kuwaona na kujinadi kwa kudhani wao ni wanachama zaidi kuliko wengine, wakiwaitisha hata kama vipi kuondoka isipokuwa wao!

8. Kwamba hapo #7, vijana wa hovyo hawa, chama kimeshindwa hata kuwakemea hadharani? Ukiwa ni mwendelezo wa mapungufu ya yasiyo na afya ya yatokanayo na haya tunayoyaoigia kelele Kila leo kwa maslahi ya chama:

"Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama"

9. Hapo #8, ni hali isiyoweza kuwavutia wenye kujitambua au akili zao chamani. Kwa hakika ni ujasiri wa kutokuwa tayari kuwasusia fisi bucha kuendelea kukomaa nao.

10. Hatuwezi kuendekeza ujinga, wajinga au kuwAendekeza watu wasiojua wanataka au hawataki nini kwenye mapambano yasiyohitaji ajizi kuwatia CCM madarakani.

11. Wanasema mjini kwa mwendo huu hatuwezi kutoboa!

12. Siyo siri, tunahitaji mwanzo mpya wa mawazo. Tulipo tumegonga mwamba.

13. Waungwana wanasema, "retreat is no surrender."
 

Nilipanga kukupuuza lakini nikadhani sitakuwa nimekutendea haki:

1. Kwamba "umelazimiswa kuwapo chamani?!" Maneno magumu haya kutoka kwa mwanachama mmoja kwenda kwa mwingine.

2. Kwani wewe nani? Au wewe ndiye uliyelazimishwa kuwapo?

3. Kwani wewe una haki zaidi kuliko nani?

4. Au ni busara zako tu ndugu kwenda likizo bila taarifa au bila ya weye kujua?

5. Hao CCM mtawalaumu sana kama dobi tu, wakati kaniki ni rangi yake. Wengine wakisema mtamaliza bucha zote, nyama ni ile ile.

6. Tuwaseme Lipumba, Lungwe, au wengine unsowataja, kwani hao wanatuhusu sisi nini?

7. Hapo #6 tunawasema na tutaendelea kuwasema nyote kwa muktadha huu:

Tutambuane: Wenye ujasiri au sababu za kuikabili CCM

8. Kulikoni kututaka kumsema awaye yote kwa muktadha wako? Kwa muktadha wako si unamsema mwenyewe ndugu?

9. Hapo #7 ni nia yetu ya dhati kumfurusha CCM madarakani. Tunamfurusha huyo na majasiri na waliodhamiria kwenye hilo.

10. Hapo #7 tunajua mpo mlio CCM bila ya wenyewe kujitambua kwa maana bila mnadhani CCM ni rangi na siasa ni ushabiki tu kama wa mpira.

11. Hapo #10, wapo walio CCM hadi viongozi upinzani bila ya wao kujitambua. Hili halijali hata nyadhifa walizo nazo.

12. Hapo #11, misahafu inasema, "si wote waniitao bwana bwana, wataurithi ufalme wa mbinguni."
 
Hauna hoja nakwambia ukweli, ndio maana nimekuuliza maswali madogo umeshindwa kujibu.

Hiyo haki ya kila raia kwanini hamkupewa wakati ule wa Magufuli na mkanyamaza? au kwa Magufuli haikuwa haki ya raia!

- Kwanini hiyo "haki ya raia na kauli ya Rais" vikaja baada ya maridhiano?

Nakwambia tena, hauna hoja, kwa hiki ulichoandika hapa umekurupuka.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nimekwambia "kesi" nimetumia kama msemo, soma uelewe.

Habari ha kutofautiana mawazo kwangu sio tatizo, nachotaka taratibu zifuatwe.

Niko simple sana, sioni sababu ya kubishana, tatizo hunisomi vizuri unielewe, unaonekana unakimbilia kujibu tu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…