Pre GE2025 Ushauri: Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
"Kesi" nimetumia kama msemo tu, nikiwa na maana kutofautiana mawazo.

Maswali yako mengine kuyajibu naona kuchoshana, kama una hoja iweke kwa mtindo huo twende sawa, lakini sio maswali juu ya maswali...

Ajabu unasema nimeandika mengi yasiyo eleweka halafu unasema kwangu neno "demokrasia ni shida", wakati kwenye hayo maelezo yangu nimekuonesha na wenzako demokrasia ikoje kwa vitendo, na sio maneno kama haya unayoandika hapa.

- Hapo demokrasia ni shida kwangu au kwenu? au kwenu demokrasia simply mnamaanisha mnachokitaka nyie ndio lazima kiwe tofauti na wengine walivyoamua?! kutaka Mbowe aondoke mna maana ipi? ndio demokrasia yenu hiyo?! hata siwalewi na ndio maana hata mleta mada nae amepotea!.

All in all, muda wa Mbowe ukifika ataondoka, simple, kama hamumtaki muandaneni yule mumtakaye, lakini kupiga kelele zenu wakati huu ni kukivuruga chama kikiwa kwenye harakati zake nyingine.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 

1. Kama kesi umetoa kwenye maneno yangu umeninukuu sivyo. Hakuna popote nimesema hayo!

2. Kama kutofautiana kimawazo ni tatizo kwako si tatizo kwetu. Tatizo ni misimamo, imani na falsafa kuparaganyika.

3. Kwenda sawa ni jambo la msingi. Kama ni nia yako kujadili tukubaliane kwenda na hoja moja moja. Kumbuka nilijibu na kuuliza tokea kwenye lukuki uliyokuwa umeandika.

4. Kuondoka ni jambo la afya. Hakuna wa kukaa milele, kumtaka au kutokumtaka Hilo ni jambo la kidemokrasia na kiutendaji.

5. #4 ukikiuka misingi tutakosa uvumilivu.

6. Kukivuruga chama ni kukiuka haki za wengine. Kuziita hoja za wengine wenye mawazo tofauti kupiga kelele ni mfano wa vurugu hizo za wazi.

7. Umoja ni nguvu hapo #6 sijui ni harakati zipi za chama zitafanikiwa kwenye utengano.

8. Hapo #3 yapo maoni ya wazi ya namna ya kuendelea mbele. Uchaguzi ni wako.

9. Ukipenda angalia mdau hapa na umuhimu wa imani thabiti:

"Imani ni kuwa na uhakika."

10. Bila kusahau, hakuna popote nimesema demokrasia ni kile tu tunachosema sisi, labda wewe kama unadhani demokrasia ni kile tu mnachosema ninyi.
 

Tatizo unataka kunilazimisha kuukataa ukweli. Naomba nikuelimishe kidogo tu, mikutano ya siasa ni haki ya kila raia, haikutakiwa maridhiano kujirudisha Bali kauli ya kisiasa tu kutoka kwa Rais.

Naomba nikupe ushahidi wa mambo mawili kwamba Mbowe alituhakikishia kwamba mambo yataenda vizuri. Kwa mfano Kwenye mkutano wa kwanza wa CHADEMA 2022, pale Mwanza Mbowe alisema wazi kwamba yeye hatamsema vibaya Mama Samiah. Ile kauli ilisababisha CCM kudai Mbowe anampigia kampeni mama Samiah na kuonesha kwamba CHADEMA inamuunga mkono mama Samia, pamoja na dhihaka zote Mbowe akiendelea na hiyo kauli. Leo utasemaje kwamba ilikuwa bahati mbaya?. Mbowe kakiingiza chama kwenye Jambo ambalo chama kingeweza kuepuka.

Pia baada ya hapo Akina Lissu wakapinga maridhiano na CCM ikiwemo na Mimi, Mbowe akashupaza shingo na kudai ameweka taifa mbele kuliko chama. Sasa leo utadai ni bahati mbaya au makosa ya kibinadamu?. Yani mtu anashauriwa hataki, halafu Leo analeta stori za kujuta wakati amekiingiza chama kwenye shida?.

Msimamo wangu ni kwamba pamoja na Mbowe kujuta, aachie madaraka kuonesha kweli anajutia.
 
Kumbe unakiri ule ulikuwa uwanja wa vita, ajabu unataka Mbowe aende kwenye uwanja wa vita bila silaha, wake up dude!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Nikuulize swali, Mbowe ameenda kwenye vita gani? Na Silaha gani?. Kwa hivyo kujirahisisha kwa Samiah ndio Silaha. Wewe ndio uamke usingizini.

Mbowe must go, maana approach yake imeshindwa ameleta dharau kwa CHADEMA. Yani kukiri kuzidiwa maarifa na mama Samiah ni upuuzi mkubwa.
 


Wewe ndio unatakiwa kupanua ubongo. Nimeeleza kwenye mada yangu, issue sio kukosa, issue ni kuendelea na makosa hayo kila siku. Mbowe amekifanya chama kuwa bila msimamo. Leo maridhiano, kesho maandamano, kesho kutwa maridhiano etc. Sasa huu ni ujinga, CCM wanachukia advantage, ni heri kuwa na msimamo mmoja mpaka mwisho.

Sio unashupaza shingo hutaki kuambiwa, siku Samiah amekuingiza mjini inaanza kulia najuta kumwamini Samiah, that is a shame. Mbowe astaafu, tujenge image mpya ya chama.
 

Napropose Lissu Mwenyekiti na Heche Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti tumpe Catherine Ruge.
 
Wewe ni Nani kwenye hii Taasisi!
Kwaki kutomuamini ni dhambi!
Fuatilia yanayiendelea Amerika na kwengineko acha uchawa.
 

Nani hatambui mchango wa Mbowe? Nani hatambui Mbowe alivyojitoa kwaajili ya chama?. Ninachosema approach anayotumia haitatufikisha popote, CCM watakuwa wanatuchezea kila siku.

Halafu unaweza kufanya mengi mazuri ukayaharibu yote kwa siku moja. Pia unaweza kuwa hero uakaishia zero. Kasome hadithi ya Mugabe alivyoishia Kama zero. You can do good but spoil all the good in one day.

Mbowe kafanya mazuri mengi sana, ila ili akumbukwe Kama kiongozi Bora ajiuzulu kwa kukiingiza chama kwenye mtego wa CCM , na mwishowe kukiri CCM walimrubuni. Hatuwezi kuendelea na kiongozi anaendelea kurubuniwa na CCM kila siku. Akae pembeni.
 
Sasa kama ametambua hilo na kusahihisha, shida iko wapi? Admitting weaknesses/failures is a positive attribute.

Kukubali amekosea sio vibaya, shida ni kwamba wakati anakosea akaonywa ila akakaza shingo na kuwaona akina Lissu ndio wenye shida. Leo anarudi kulalamika amaechezewa na CCM. Sasa anamlalamikia nani?.

Ili kunielewa vizuri, kaangalie video ya mkutano wa Mbowe Marekani kwa diaspora alivyoongea na Leo anavyoongea. CHADEMA haiotaji kiongozi kinyonga never.
 

Mbowe astaafu kwa heshima, asilazimiahe awe Kama mrema au Lipumba. Miaka 22 ni mingi Sana. Ndio maana anafanya makosa ya wazi kabisa.
 

CHADEMA haitaki malaika Bali inataka kiongozi asiyeyumba. Akisema hapana ni hapana. Sio inaitwa ikulu unageuza msimamo haraka.
 

Mbowe amefanya mengi, Sasa ni wakati wakuwaachia vijana aliowatengeneza kushika haramu. Kwa Sasa Hana ushawishi, maana hachelewi kugeuza msimamo.
 

Tatizo mkuu umesoma mada yangu kwa juu juu bila kuipitia vizuri. Nimesema Mbowe ajiuzulu Kama Mwenyekiti wa CHADEMA. Hoja yangu ipo objective kwenye uongozi na sio Mbowe.

Nasema hivi kwa Sasa tulipofikia, Mbowe ameonesha kutokuwa na msimamo. Alitetewa maridhiano wanachama wa CHADEMA wakapinga ila Mbowe akadai anapamabania nchi, leo anawarudia wenzake waliomkataza na kuwalilia kuwa anajuta muwaamini CCM.

Mbowe Hana msimamo na hivyo kujifanya CHADEMA kiyumbe. Leo maridhiano, kesho maandamano etc. Kama umeamua maridhiano endelea na maridhiano , Kama umeamua confrontational uwe confrontational, sio unakuwa vuguvugu mpaka CCM wanajua jinsi ya kukuhadaa maana wanajua huna msimamo.

Kuhusu CCM nani awalalmikie wakati wanajulikana ni matapeli?. Kwenye madam nimetoa mfano wa maalim seif jinsi walivyomtapeli akaingia kwenye mtego wa CCM na pamoja na kujishusha kwake CCM walimlima marungu 2020. So CCM ni waovu tangiepo.
 

Kiongozi angekuwa Lisu au mwingine yoyote sidhani kama angekubali kwenda ikulu baada ya kutolewa jela na mtu aliyemfunga, kuacha kupigania katiba mpya, kuingia maridhiano yao wawili binafsi, kukubali 150mn binafsi kwa niaba ya kanisa, kutetea maridhiano ya kificho.

Ni wao wawili tu walikuwa wanajua wanaridhiana nini?
 

Acha kujiona unajua zaidi ya wengine, huo ni udhaifu. Halafu usipende kuconclude mambo Kama unavyotaka. Nimetoa sababu kwanini nimesema hivyo. CCM hawaaminika na ndio maana Mbowe ameenda kwenye Maridhiano wamegeuka.

Mbinu ambayo wanaotakiwa kunitumia ni passive Confrontational politics. Siasa za msimamo mkali zisizokuwa na vurugu ndani yake.

Kwa mfano tulikuwa tunapenda vizuri. Tulikataa uchaguzi, tuliwafukuza kina halima, tulikataa Ruzuku, tulikataa kwenda kwenya mabaraza ya kinafiki etc. Hiyo ndio passive Confrontational politics, siku mambo yakienda vibaya tutaendea mbali zaidi.
 
Wewe ni Nani kwenye hii Taasisi!
Kwaki kutomuamini ni dhambi!
Fuatilia yanayiendelea Amerika na kwengineko acha uchawa.

Wewe ni nani wa kuniuliza Hilo swali? Halafu usinipangie Cha kusema.
Huwezi kujua Mimi ni nani ndani ya CHADEMA, ila nikuhakikishie nimekuwa mwanachama wa CHADEMA kabla Mbowe hajawa mwenyekiti wa CHADEMA. Sisi ni wale tutafia CHADEMA.

Halafu Kama wewe ni chawa Baki nao huko mwenyewe. Mimi siyumbishwi na watu Kama wewe wakuja na kupitia. Sisi tunajua CHADEMA imetoka wapi na inaenda wapi. Hivyo punguza ujuaji. Mimi naita koleo ni koleo sio Kijiko kikubwa.
 
Mbowe kajenga nyumba kali sana
 
Mbowe ni chawa wa CCM, mnajuwa leo...!?
 
Kama kuna kitu kinajuwa kuwapotezea Watz muda na kuwatia umaskini, ujinga na kuhasimiana ni VYAMA VYA SIASA.
 
Chama ni chama mbowe alichorithishwa na mkwe wake,.kwa hiyo ni mali yake binafsi na siyo mali ya chama.kama unataka wewe ondoka muachie mbowe kitega uchumi chake.
Jinga wewe, Mwinyi (baba) alikuwa Rais Zanzibar na baadae Jamuhuri ya Muungano, kwanini hukumzuia mtoto awe Rais? Sijuhi wewe jamaa ni punguani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…