Yeye anapendelea nini .unaweza kukuta anapenda biashara ukamuanzishia genge, kioski akatoka huko , akaja kukusaidia baadaeNaombeni ushauri kuhusu mdogo wangu wa kiume ambaye hajamaliza hata shule ya msingi na sasa amekuwa mzigo, kwani mawazo ya kusoma hana. Nataka nimtafutie fani (ufundi) ili mbeleni asijekuwa mzigo, kumbuka ni miaka 18+.
Naombeni ushauri wa fani inayoweza kumfaa na labda pia kama mnajua chuo cha veta kinachotoa fani husika.
Location yake ni Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Musoma au Geita.
Nawasilisha
Ahsante saana naomba nikujibu kama ifuatayo.Kwanza nikupongeze kwa yafuatayo
1.upendo wako wa hali ya juu
2.akili njema ya kujua kuzuia mizigo ijayo
Pili nije kwa mada kaka huyo bado kwa umri wake mdogo usimkatie tamaa huyu tukikushauri vyema ww ndo badae itakuwa tegemezi kwake .
Naomba unijibu haya ndipo nikushauri juu ya mdogo wetu
1.kaa nae muulize anapendelea maishani afanye shughuli gani ya kulea familia yake.mtajie bajeti yako familia mwambie na yy atakuwa nayo si muda na atalipia yy je amejipangaje
2.je analewa.anavuta sigara? Ni wa ngapi kuzsliwa
3.ana kipaji chochote cha kuzaliwa
4.nidhamu yake kwenye hela yake ikoje
5.ni lazima aishi mwanza au huko?
6.unabajet kiasi gani kumsaidia?
Hapa sasa nimepata nguvu ya kukushauriAhsante saana naomba nikujibu kama ifuatayo.
1.kwanza yeye bado yupo nyumbani analelewa na ukimwambia habari ya maisha kuwa ni magumu haoni kama n kweli kwasababu bado analelewa
2.halewi, havuti sigara na kuhusu nidhani ni kuwa anaweza kuishi na mtu yeyote yule sema ana ka ushamba flani hvi samahan sijamdharau.
3.yeye ndiye kitinda mimba.
4.hana kipaji chochote kile lakn pia katk hii siwezi msemea saana kwa maana sijakaa nae muda mrefu kumpima ila naona kama anapenda maswala ya umeme umeme.
5.kuhusu nidhamu ya hela pia siwez semea maana hajawahi pata pesa za kwake yeye kama yeye ila ni mwaminifu.
6.sio lazima aishi mwanza au huku ila nilitamani iwe hayo maeneo maana ndio itakuwa rahisi mmi kummonita
6.kuhusu bajet nimejipanga kulingana na kile nitakachokiona kinafaa
Uzi ufungweHuyo kama kusoma hataki hata usimpeleke VETA, mtafutie gereji akajifunze maisha huko. Au mtafute fundi ujenzi mkabidhi afundishwe kazi apige na vibarua vya zege.
Gereji Gani mtu atapokea mtu asiyejua chochote kuhusu magari labda iwe gereji ya familia au ndugu unayemjuaHuyo kama kusoma hataki hata usimpeleke VETA, mtafutie gereji akajifunze maisha huko. Au mtafute fundi ujenzi mkabidhi afundishwe kazi apige na vibarua vya zege.
Sorry naomba ufafanuzi juu ya huu Mfumo ww QT utaratibu wake upoje na ukifaulu inatambulika na cheti unapewa?Mwambie aende QT miaka 2 umemaliza tayari 4m4 halafu ndio aende veta
Mkuu hujui hata QT??anyway ni Elimu ya kawaida ya Sekondari isipokuwa hii badala ya kusoma miaka 4(Form 1 mpaka Form 4)hii unasoma kwa miaka 2,au badala ya kusoma Form 5 na 6 kwa miaka miwili kwa QT unasoma kwa mwaka mmoja kisha unapiga Mtihani wa Taifa wa Form 6. Mtihani wa Kitaifa atafanya uleule watakaofanya wale waliosoma kwa miaka 4,sasa hii QT inabidi kukaza maana badala ya miaka 4 unasoma kwa miaka 2Sorry naomba ufafanuzi juu ya huu Mfumo ww QT utaratibu wake upoje na ukifaulu inatambulika na cheti unapewa?