USHAURI: Mdogo wangu amekataa shule, nataka nimtafutie fani ya ufundi asiwe mzigo mbeleni

USHAURI: Mdogo wangu amekataa shule, nataka nimtafutie fani ya ufundi asiwe mzigo mbeleni

Naombeni ushauri kuhusu mdogo wangu wa kiume ambaye hajamaliza hata shule ya msingi na sasa amekuwa mzigo, kwani mawazo ya kusoma hana. Nataka nimtafutie fani (ufundi) ili mbeleni asijekuwa mzigo, kumbuka ni miaka 18+.

Naombeni ushauri wa fani inayoweza kumfaa na labda pia kama mnajua chuo cha veta kinachotoa fani husika.

Location yake ni Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Musoma au Geita.

Nawasilisha
Yeye anapendelea nini .unaweza kukuta anapenda biashara ukamuanzishia genge, kioski akatoka huko , akaja kukusaidia baadae
 
Kwanza nikupongeze kwa yafuatayo
1.upendo wako wa hali ya juu
2.akili njema ya kujua kuzuia mizigo ijayo

Pili nije kwa mada kaka huyo bado kwa umri wake mdogo usimkatie tamaa huyu tukikushauri vyema ww ndo badae itakuwa tegemezi kwake .
Naomba unijibu haya ndipo nikushauri juu ya mdogo wetu
1.kaa nae muulize anapendelea maishani afanye shughuli gani ya kulea familia yake.mtajie bajeti yako familia mwambie na yy atakuwa nayo si muda na atalipia yy je amejipangaje
2.je analewa.anavuta sigara? Ni wa ngapi kuzsliwa
3.ana kipaji chochote cha kuzaliwa

4.nidhamu yake kwenye hela yake ikoje

5.ni lazima aishi mwanza au huko?
6.unabajet kiasi gani kumsaidia?
Ahsante saana naomba nikujibu kama ifuatayo.
1.kwanza yeye bado yupo nyumbani analelewa na ukimwambia habari ya maisha kuwa ni magumu haoni kama n kweli kwasababu bado analelewa
2.halewi, havuti sigara na kuhusu nidhani ni kuwa anaweza kuishi na mtu yeyote yule sema ana ka ushamba flani hvi samahan sijamdharau.
3.yeye ndiye kitinda mimba.
4.hana kipaji chochote kile lakn pia katk hii siwezi msemea saana kwa maana sijakaa nae muda mrefu kumpima ila naona kama anapenda maswala ya umeme umeme.
5.kuhusu nidhamu ya hela pia siwez semea maana hajawahi pata pesa za kwake yeye kama yeye ila ni mwaminifu.
6.sio lazima aishi mwanza au huku ila nilitamani iwe hayo maeneo maana ndio itakuwa rahisi mmi kummonita
6.kuhusu bajet nimejipanga kulingana na kile nitakachokiona kinafaa
 
Hapa sasa nimepata nguvu ya kukushauri
1.huyu ana shida ya ugonjwa wa umwisho ni mbaya sana.mjitaahidi akakaae kwa mtu baki kwanza au wa mbali .hii sisi tulibahatika kusoma tunaikuta chuo kikuu mm wa meru vijijin nlisoma huko ghafla nkafaulu chuo nkabidi nianze kujua bei ya nyanya na ugumu wa maisha
2 .apelekwe gereji mwaka ili aingie kwenye ulimwengu halisi na ajue wakubwa tunaposema maisha magumu tunamaanisha nini akisha fanya mwaka akapangiwe chumba mkoa wa mbali na nyie muwe mnamtembelea hii ni ajenge nidhamu ya kujitegemea .hii kwa wasomi unaikuta chuo kwenu musoma unapata chuo mtwara unajifunzs kwa nguvu
3.endelea kumsimamia mpaka 21 ulimsoma hasa yeye moyo wake uko kazi gani .mtu ambae hajasoma njia pekee ni kufanya kazi ya hobi yale ataipenda
4.kamlipie gym au mpe jezi akatoe huo umwisho huko ukimuandaa pia muandikishe udereva haraka
5.endelea kumuweka karibu na mambo ya liroho

Akifika 21 tutakushauri baada y lutupa uzoefu .
 
Huyo kama kusoma hataki hata usimpeleke VETA, mtafutie gereji akajifunze maisha huko. Au mtafute fundi ujenzi mkabidhi afundishwe kazi apige na vibarua vya zege.
Gereji Gani mtu atapokea mtu asiyejua chochote kuhusu magari labda iwe gereji ya familia au ndugu unayemjua

Vijana wengi wamemaliza VETA ufundi magari ngumu sana kupata hata gereji ya kujitolea Bure .Wamiliki hawataki labda uwe ndugu Yao

Kajaribu hata wewe uone mziki wake sio Rahisi kihivyo peleka ndugu Yako uone
 
Sorry naomba ufafanuzi juu ya huu Mfumo ww QT utaratibu wake upoje na ukifaulu inatambulika na cheti unapewa?
Mkuu hujui hata QT??anyway ni Elimu ya kawaida ya Sekondari isipokuwa hii badala ya kusoma miaka 4(Form 1 mpaka Form 4)hii unasoma kwa miaka 2,au badala ya kusoma Form 5 na 6 kwa miaka miwili kwa QT unasoma kwa mwaka mmoja kisha unapiga Mtihani wa Taifa wa Form 6. Mtihani wa Kitaifa atafanya uleule watakaofanya wale waliosoma kwa miaka 4,sasa hii QT inabidi kukaza maana badala ya miaka 4 unasoma kwa miaka 2
 
Back
Top Bottom