USHAURI: Milioni 20 ya mkopo kipindi cha Magufuli, niwekeze kwenye nini?

Kama n mechanics nakushauri ufungue duka la vipuri na vilaijishi vya gari na unakuwa fundi mwenyewe , unafanya service ya magari na kujaza upepo , ukimaliza kufanya service unawaoshe gari zao bure utapata wateja wengi sana aise
 
Wadau nimepata kafursa ka kuvuta kama milioni 20 hivi kipindi kigumu hiki cha magu hadi wanaume tumeona sifa kujiita "wanaume suruali" ili tusinyoyolewe.

Nilikua naomba michango yenu ya mawazo proper investment ambayo naweza wekeza ili nitakapoanza kukatwa mlolongo wa makato kama mwanafunzi wa marekani..kuanzia loan board,paye,nssf,hako kamkopo ..nibaki na stress kwa mawazo kipindi kinachobaki

Natanguliza shukrani za dhati maana katika miaka yangu mitano ya uanachama jamiiforum haijawahi niangusha
Kama kupata huo mkopo uliweka dhamana ya nyumba, hesabu hiyo nyumba ushawauzia benki...
 
Biashara yoyote ni Risk, yaani kuna hatari ya kupata hasara pia.
Kuwa na mtaji wa kipesa halafu kutafuta wazo la biashara hakutoi uhakika wowote wa kuweza kufanikiwa kibiashara, japokuwa ni jambo zuri na muhimu. Why? Biashara ni Ujuzi, Utundu, Uzoefu, Sanaa na Sayansi. Wazo la kibiashara linaweza kujibu hitaji la Kisayansi(Mbinu za kupata faida) katika biashara, lakini halijibu mahitaji hayo mengine manne ya Biashara.

USHAURI WANGU.
1/Kama una biashara yoyote ile ndogo unaifanya kwa sasa, basi tumia huo mtaji wa kipesa kuikuza zaidi.

2/Kama hujawahi kufanya biashara, basi anza kufanya biashara yenye mtaji mdogo sana ili kupata UJUZI, UTUNDU, UZOEFU na USANII katika biashara. Usiogope kupata hasara katika hili, na ili kuepuka maumivu, mtaji wake uwe mdogo sana.

3/Kwa mazingira yaliyopo sasa hapa Tanzania, sio wakati mzuri sana wa kuwekeza pesa zako kwenye Biashara yenye kuhitaji mzunguko mkubwa wa kuuza na kununua.(Wafanyabiashara wengi kwa sasa wanalia sana), njia nyepesi kabisaa kwa sasa ni kulinda mtaji wako wa kipesa kwa kuwekeza kwenye Real Estate(Viwanja na Nyumba). Hakuna namna tena, ndio mahali salama zaidi pakukimbilia.
Kwa mtaji wa Milioni 20, Unaweza kupata Viwanja hata Vitatu(ukubwa wa Mita 20X20) maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar, Arusha na Mwanza.
Kwa mikoa mingine unaweza kupata zaidi ya hapo.
Ama unaweza kununua shamba la Miti michanga lenye ukubwa wa Ekari zaidi ya Tano katika mikoa ya Iringa na Njombe. Utavuna miti baada ya miaka Minne au zaidi. Faida yake ni kubwa sana(Mara mbili au Tatu ya mtaji uliouweka).

Ni hayo tu kwa leo......
 
NMEKUELEWA SANA
 
mi nilikuwa nasoma comments tu,utadhani mi ndo nashauriwa!!but mi ningenunua kiwanja tu, kama unacho katikati ya mji jenga chumba sebule kadhaa na upangishe kwa 40000@
 
NILICHOJIFUNZA NI KUA WATANZANIA WENGI WANAPENDA CRITICIZE HATA BILA KUJUA UPANDE WA PILI HAYA MAWAZO NI MAPANA SNA NA NTAYAFANYIA KAZI MKOPO BADO SIJACHUKUA ILA NAJARIBU KUWEKA WAZO TU KWE AKILI ZA WATU...HV LETS SAY WEWE MDA HUU UMEPATA HICHO KIASI UTAFANYIA NN....MAJORITY YA WATTU NILIOKAA NAO HAWAKUA NA MAJIBU MOJA KWA MOJA HII INAONYESHA ULE MSEMO NADHAN ALIKUA WAZIRI MKUU WA ISRAEL AU DONALD TRUMP KUWA WAAFRIKA WENGI HAWAFIKIRII ZAIDI YA MIAKA 3 MBELE...NANYI JIULIZENI MKIPATA HIYO AMOUNT MTAFANYIA NN INAWEZA WAPANUA MAWAZO...NASHUKURU WALAIOWEZA NIJIBU MAJIBU MAZURI
 
Na amni wewe utakuwa umesoma vizur kama umesoma vizuri utakuwa na upeo wa akili vizur .

Ushauri kama ni mkazi wa Dar es salaam nenda kanunue shamba kama hekari moja na nusu au mbili maeneo ya Bunju anzisha ka bustani cha mboga mboga mfano nyanya ,mchicha nk utatengeneza hela nzuri na utakuwa huja poteza hela hata kama biashara ikikushinda unayo plot
bunju hekari moja sh ngap?
 
Biashara yoyote ni Risk, yaani kuna hatari ya kupata hasara pia.
Kuwa na mtaji wa kipesa halafu kutafuta wazo la biashara hakutoi uhakika wowote wa kuweza kufanikiwa kibiashara, japokuwa ni jambo zuri na muhimu. Why? Biashara ni Ujuzi, Utundu, Uzoefu, Sanaa na Sayansi. Wazo la kibiashara linaweza kujibu hitaji la Kisayansi(Mbinu za kupata faida) katika biashara, lakini halijibu mahitaji hayo mengine manne ya Biashara.

USHAURI WANGU.
1/Kama una biashara yoyote ile ndogo unaifanya kwa sasa, basi tumia huo mtaji wa kipesa kuikuza zaidi.

2/Kama hujawahi kufanya biashara, basi anza kufanya biashara yenye mtaji mdogo sana ili kupata UJUZI, UTUNDU, UZOEFU na USANII katika biashara. Usiogope kupata hasara katika hili, na ili kuepuka maumivu, mtaji wake uwe mdogo sana.

3/Kwa mazingira yaliyopo sasa hapa Tanzania, sio wakati mzuri sana wa kuwekeza pesa zako kwenye Biashara yenye kuhitaji mzunguko mkubwa wa kuuza na kununua.(Wafanyabiashara wengi kwa sasa wanalia sana), njia nyepesi kabisaa kwa sasa ni kulinda mtaji wako wa kipesa kwa kuwekeza kwenye Real Estate(Viwanja na Nyumba). Hakuna namna tena, ndio mahali salama zaidi pakukimbilia.
Kwa mtaji wa Milioni 20, Unaweza kupata Viwanja hata Vitatu(ukubwa wa Mita 20X20) maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar, Arusha na Mwanza.
Kwa mikoa mingine unaweza kupata zaidi ya hapo.
Ama unaweza kununua shamba la Miti michanga lenye ukubwa wa Ekari zaidi ya Tano katika mikoa ya Iringa na Njombe. Utavuna miti baada ya miaka Minne au zaidi. Faida yake ni kubwa sana(Mara mbili au Tatu ya mtaji uliouweka).

Ni hayo tu kwa leo......
namba mbili nmeielewa,
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mkulima na mfanyabiashara wa mazao, upo hapo? watu lazima wale hata kama kuna ugumu wa maisha wa namna gani, mazao faida yake ni ndogo lakini yanatoka sana na hayana changamoto nyingi zaidi ya kulipa ushuru wa halmashauri husika basi, biashara zingine TRA, TFDA, Zimamoto, Umeme, Mlinzi, leseni nk. Ok we ndiyo mwenye maamuzi mkuu.
[/QUOTE]bei ya mazao ni pasua kichwa haieleweki hasara nje nje
 
NILICHOJIFUNZA NI KUA WATANZANIA WENGI WANAPENDA CRITICIZE HATA BILA KUJUA UPANDE WA PILI HAYA MAWAZO NI MAPANA SNA NA NTAYAFANYIA KAZI MKOPO BADO SIJACHUKUA ILA NAJARIBU KUWEKA WAZO TU KWE AKILI ZA WATU...HV LETS SAY WEWE MDA HUU UMEPATA HICHO KIASI UTAFANYIA NN....MAJORITY YA WATTU NILIOKAA NAO HAWAKUA NA MAJIBU MOJA KWA MOJA HII INAONYESHA ULE MSEMO NADHAN ALIKUA WAZIRI MKUU WA ISRAEL AU DONALD TRUMP KUWA WAAFRIKA WENGI HAWAFIKIRII ZAIDI YA MIAKA 3 MBELE...NANYI JIULIZENI MKIPATA HIYO AMOUNT MTAFANYIA NN INAWEZA WAPANUA MAWAZO...NASHUKURU WALAIOWEZA NIJIBU MAJIBU MAZURI
we nunua kiwanja au gari ya kutembelea tu, biashara kama unafanya kazi unaweka mtu wa kuisimamia umeumia, watu wanasimamia biashara zao 24hrs na bado wanafilisika ijekuwa wewe unaeshinda ofisini?
 
Ungekua na kama 30m ungepata tractor New Holland nzuri tu kwa mtu umkabidhi ndugu yako unaemuamini akufanyie kazi morogoro ndani ya mwaka tu usingekosa angalau 20m kwenye tractor bado nawew ungeamua kulima mashamba yako...
 
New Holland sio tractor nzuri inawahi sana kuchoka na spare zake gharama sana, ugonjwa wake mkubwa ni diff, atafute Massey mtumba, ila hiyo mil 30 haiwezi kutosha sababu ili apate hela nzuri anahitaji jembe zuri, na jembe zuri chapa samaki ni 8mil jipya, vile vile inabidi awe na hela ya kukodi shamba kwa ajili ya tractor yani shamba litakalo hudumia tractor huwezi kutegemea hela ya wakulima peke yake lasivyo tractor litakaa juu ya mawe,unalima kwanza shamba ulilokodi la kwako halafu ndio unaenda kwenye mashamba mengine ya watu kuwalimia hapo utapata faida maradufu
 
bado najifunza kitu hapa>>asanteni
 
Back
Top Bottom