Biashara yoyote ni Risk, yaani kuna hatari ya kupata hasara pia.
Kuwa na mtaji wa kipesa halafu kutafuta wazo la biashara hakutoi uhakika wowote wa kuweza kufanikiwa kibiashara, japokuwa ni jambo zuri na muhimu. Why? Biashara ni Ujuzi, Utundu, Uzoefu, Sanaa na Sayansi. Wazo la kibiashara linaweza kujibu hitaji la Kisayansi(Mbinu za kupata faida) katika biashara, lakini halijibu mahitaji hayo mengine manne ya Biashara.
USHAURI WANGU.
1/Kama una biashara yoyote ile ndogo unaifanya kwa sasa, basi tumia huo mtaji wa kipesa kuikuza zaidi.
2/Kama hujawahi kufanya biashara, basi anza kufanya biashara yenye mtaji mdogo sana ili kupata UJUZI, UTUNDU, UZOEFU na USANII katika biashara. Usiogope kupata hasara katika hili, na ili kuepuka maumivu, mtaji wake uwe mdogo sana.
3/Kwa mazingira yaliyopo sasa hapa Tanzania, sio wakati mzuri sana wa kuwekeza pesa zako kwenye Biashara yenye kuhitaji mzunguko mkubwa wa kuuza na kununua.(Wafanyabiashara wengi kwa sasa wanalia sana), njia nyepesi kabisaa kwa sasa ni kulinda mtaji wako wa kipesa kwa kuwekeza kwenye Real Estate(Viwanja na Nyumba). Hakuna namna tena, ndio mahali salama zaidi pakukimbilia.
Kwa mtaji wa Milioni 20, Unaweza kupata Viwanja hata Vitatu(ukubwa wa Mita 20X20) maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar, Arusha na Mwanza.
Kwa mikoa mingine unaweza kupata zaidi ya hapo.
Ama unaweza kununua shamba la Miti michanga lenye ukubwa wa Ekari zaidi ya Tano katika mikoa ya Iringa na Njombe. Utavuna miti baada ya miaka Minne au zaidi. Faida yake ni kubwa sana(Mara mbili au Tatu ya mtaji uliouweka).
Ni hayo tu kwa leo......