nyambele01
Member
- Nov 15, 2016
- 14
- 6
Kama kupata huo mkopo uliweka dhamana ya nyumba, hesabu hiyo nyumba ushawauzia benki...Wadau nimepata kafursa ka kuvuta kama milioni 20 hivi kipindi kigumu hiki cha magu hadi wanaume tumeona sifa kujiita "wanaume suruali" ili tusinyoyolewe.
Nilikua naomba michango yenu ya mawazo proper investment ambayo naweza wekeza ili nitakapoanza kukatwa mlolongo wa makato kama mwanafunzi wa marekani..kuanzia loan board,paye,nssf,hako kamkopo ..nibaki na stress kwa mawazo kipindi kinachobaki
Natanguliza shukrani za dhati maana katika miaka yangu mitano ya uanachama jamiiforum haijawahi niangusha
NMEKUELEWA SANABiashara yoyote ni Risk, yaani kuna hatari ya kupata hasara pia.
Kuwa na mtaji wa kipesa halafu kutafuta wazo la biashara hakutoi uhakika wowote wa kuweza kufanikiwa kibiashara, japokuwa ni jambo zuri na muhimu. Why? Biashara ni Ujuzi, Utundu, Uzoefu, Sanaa na Sayansi. Wazo la kibiashara linaweza kujibu hitaji la Kisayansi(Mbinu za kupata faida) katika biashara, lakini halijibu mahitaji hayo mengine manne ya Biashara.
USHAURI WANGU.
1/Kama una biashara yoyote ile ndogo unaifanya kwa sasa, basi tumia huo mtaji wa kipesa kuikuza zaidi.
2/Kama hujawahi kufanya biashara, basi anza kufanya biashara yenye mtaji mdogo sana ili kupata UJUZI, UTUNDU, UZOEFU na USANII katika biashara. Usiogope kupata hasara katika hili, na ili kuepuka maumivu, mtaji wake uwe mdogo sana.
3/Kwa mazingira yaliyopo sasa hapa Tanzania, sio wakati mzuri sana wa kuwekeza pesa zako kwenye Biashara yenye kuhitaji mzunguko mkubwa wa kuuza na kununua.(Wafanyabiashara wengi kwa sasa wanalia sana), njia nyepesi kabisaa kwa sasa ni kulinda mtaji wako wa kipesa kwa kuwekeza kwenye Real Estate(Viwanja na Nyumba). Hakuna namna tena, ndio mahali salama zaidi pakukimbilia.
Kwa mtaji wa Milioni 20, Unaweza kupata Viwanja hata Vitatu(ukubwa wa Mita 20X20) maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar, Arusha na Mwanza.
Kwa mikoa mingine unaweza kupata zaidi ya hapo.
Ama unaweza kununua shamba la Miti michanga lenye ukubwa wa Ekari zaidi ya Tano katika mikoa ya Iringa na Njombe. Utavuna miti baada ya miaka Minne au zaidi. Faida yake ni kubwa sana(Mara mbili au Tatu ya mtaji uliouweka).
Ni hayo tu kwa leo......
Pia siyo mbayaguest ya 20 million kaka?ah ah nasikia magufuri anataka zipunguza mjini..labda nkodishe af niipimp huduma zote muhimu natoa mimi
bunju hekari moja sh ngap?Na amni wewe utakuwa umesoma vizur kama umesoma vizuri utakuwa na upeo wa akili vizur .
Ushauri kama ni mkazi wa Dar es salaam nenda kanunue shamba kama hekari moja na nusu au mbili maeneo ya Bunju anzisha ka bustani cha mboga mboga mfano nyanya ,mchicha nk utatengeneza hela nzuri na utakuwa huja poteza hela hata kama biashara ikikushinda unayo plot
Mm sio dalali kaka haya ni mawazo na mifano tu tulikuwa tunatoa kwa mdau cjui bei gani .bunju hekari moja sh ngap?
unazingua basiMm sio dalali kaka haya ni mawazo na mifano tu tulikuwa tunatoa kwa mdau cjui bei gani .
Dah kweli nyie Watanzania mnamatatizo sn ....sasa nazingua nini? Nimekwambia mm sio dalali tatizo nini .unazingua basi
namba mbili nmeielewa,Biashara yoyote ni Risk, yaani kuna hatari ya kupata hasara pia.
Kuwa na mtaji wa kipesa halafu kutafuta wazo la biashara hakutoi uhakika wowote wa kuweza kufanikiwa kibiashara, japokuwa ni jambo zuri na muhimu. Why? Biashara ni Ujuzi, Utundu, Uzoefu, Sanaa na Sayansi. Wazo la kibiashara linaweza kujibu hitaji la Kisayansi(Mbinu za kupata faida) katika biashara, lakini halijibu mahitaji hayo mengine manne ya Biashara.
USHAURI WANGU.
1/Kama una biashara yoyote ile ndogo unaifanya kwa sasa, basi tumia huo mtaji wa kipesa kuikuza zaidi.
2/Kama hujawahi kufanya biashara, basi anza kufanya biashara yenye mtaji mdogo sana ili kupata UJUZI, UTUNDU, UZOEFU na USANII katika biashara. Usiogope kupata hasara katika hili, na ili kuepuka maumivu, mtaji wake uwe mdogo sana.
3/Kwa mazingira yaliyopo sasa hapa Tanzania, sio wakati mzuri sana wa kuwekeza pesa zako kwenye Biashara yenye kuhitaji mzunguko mkubwa wa kuuza na kununua.(Wafanyabiashara wengi kwa sasa wanalia sana), njia nyepesi kabisaa kwa sasa ni kulinda mtaji wako wa kipesa kwa kuwekeza kwenye Real Estate(Viwanja na Nyumba). Hakuna namna tena, ndio mahali salama zaidi pakukimbilia.
Kwa mtaji wa Milioni 20, Unaweza kupata Viwanja hata Vitatu(ukubwa wa Mita 20X20) maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar, Arusha na Mwanza.
Kwa mikoa mingine unaweza kupata zaidi ya hapo.
Ama unaweza kununua shamba la Miti michanga lenye ukubwa wa Ekari zaidi ya Tano katika mikoa ya Iringa na Njombe. Utavuna miti baada ya miaka Minne au zaidi. Faida yake ni kubwa sana(Mara mbili au Tatu ya mtaji uliouweka).
Ni hayo tu kwa leo......
[/QUOTE]bei ya mazao ni pasua kichwa haieleweki hasara nje njeKuna tofauti kubwa sana kati ya mkulima na mfanyabiashara wa mazao, upo hapo? watu lazima wale hata kama kuna ugumu wa maisha wa namna gani, mazao faida yake ni ndogo lakini yanatoka sana na hayana changamoto nyingi zaidi ya kulipa ushuru wa halmashauri husika basi, biashara zingine TRA, TFDA, Zimamoto, Umeme, Mlinzi, leseni nk. Ok we ndiyo mwenye maamuzi mkuu.
acha utapeli we mbona hujatoka? Umri ndio mdudu gani babu wa Loliondo ametajirika akiwa na miaka zaidi ya 70Nitafute kama unataka kutoka,,ila use tayari kuacha kazi kama una umri usio zidi miaka 35 na uwe umefanya kazi kwa zaidi ya miaka 8
we nunua kiwanja au gari ya kutembelea tu, biashara kama unafanya kazi unaweka mtu wa kuisimamia umeumia, watu wanasimamia biashara zao 24hrs na bado wanafilisika ijekuwa wewe unaeshinda ofisini?NILICHOJIFUNZA NI KUA WATANZANIA WENGI WANAPENDA CRITICIZE HATA BILA KUJUA UPANDE WA PILI HAYA MAWAZO NI MAPANA SNA NA NTAYAFANYIA KAZI MKOPO BADO SIJACHUKUA ILA NAJARIBU KUWEKA WAZO TU KWE AKILI ZA WATU...HV LETS SAY WEWE MDA HUU UMEPATA HICHO KIASI UTAFANYIA NN....MAJORITY YA WATTU NILIOKAA NAO HAWAKUA NA MAJIBU MOJA KWA MOJA HII INAONYESHA ULE MSEMO NADHAN ALIKUA WAZIRI MKUU WA ISRAEL AU DONALD TRUMP KUWA WAAFRIKA WENGI HAWAFIKIRII ZAIDI YA MIAKA 3 MBELE...NANYI JIULIZENI MKIPATA HIYO AMOUNT MTAFANYIA NN INAWEZA WAPANUA MAWAZO...NASHUKURU WALAIOWEZA NIJIBU MAJIBU MAZURI
New Holland sio tractor nzuri inawahi sana kuchoka na spare zake gharama sana, ugonjwa wake mkubwa ni diff, atafute Massey mtumba, ila hiyo mil 30 haiwezi kutosha sababu ili apate hela nzuri anahitaji jembe zuri, na jembe zuri chapa samaki ni 8mil jipya, vile vile inabidi awe na hela ya kukodi shamba kwa ajili ya tractor yani shamba litakalo hudumia tractor huwezi kutegemea hela ya wakulima peke yake lasivyo tractor litakaa juu ya mawe,unalima kwanza shamba ulilokodi la kwako halafu ndio unaenda kwenye mashamba mengine ya watu kuwalimia hapo utapata faida maradufuUngekua na kama 30m ungepata tractor New Holland nzuri tu kwa mtu umkabidhi ndugu yako unaemuamini akufanyie kazi morogoro ndani ya mwaka tu usingekosa angalau 20m kwenye tractor bado nawew ungeamua kulima mashamba yako...
Mkuu username yako siku hizi mtaani haitumiki kabisa,laki imekuwa kama milioni vile, shikamoo lakiacha utapeli we mbona hujatoka? Umri ndio mdudu gani babu wa Loliondo ametajirika akiwa na miaka zaidi ya 70