Usimlazimishe mtu kubadilika. Umekiri ulimkuta hivyo, ukampenda hivyo hivyo mpaka ukamtia na mimba. Bado yuko hivyo na bila shaka ataendelea kuwa hivyo. Nilitegemea, hata hivyo, kwamba baada ya kukuzoea kidogo angeanza kufunguka kwako maana mtu hata awe mkimya namna gani lazima kuna mtu (au watu) ambao amewazoea ambao ukimkuta anapiga nao stori mpaka unaweza kushangaa kama ni yeye kweli. Kama siyo wewe mwandani wake, ni nani sasa? Labda kama wewe ni kauzu yaani siriazi 24/7 na ameshindwa kukuzoea. Au tu basi personality zenu hazisomani utafikiri mfumo wa TPA na TRA... yaani ni zero emotional connection!
Basi kaa naye. Mwambie kuwa wewe ni rafiki na mshikaji wake na asikuogope. Na kwamba unatamani sana muwe na emotional connection kama inawezekana. Muwe mnashirikishana mapito yenu kama wenza, wazazi na marafiki. Kwamba uko msikivu...and you care. Na umaanishe na umuonyeshe kwa vitendo.
Maana usikute binti wa watu ana trauma za utotoni huko (na kwingineko); na alishajikalia kimya mazima hajali kitu tena. Ni ile mtu kuumizwa mpaka moyo ukapondeka kabisa kabisa. Mpeleke kwa therapist wakaongee huko kuhusu chanzo cha tatizo hilo na akiweza kufunguka huko unaweza kushangaa mpaka utakuja hapa kufungua uzi ukiomba ushauri kuwa mke wako anaongea sana!
β‘οΈβ‘οΈβ‘οΈ Na please usituletee singo maza mwingine huku mtaani maana tulionao wanatosha. Tafuteni suluhisho la tatizo hilo pamoja huku mkiwa katika ndoa. Kama mnapendana kwa dhati mtatoboa tuππΏ