Ushauri: Msaada kuhusu tabia ya wizi iliyokubuhu kwa kijana wangu

Wakuu muda huu rafiki yangu polisi aliniomba nimpeleke huyu dogo akaongee naye kwake ndio ninampeleka muda huu.

Kesho baba yake atakuja nimepiga simu na ndugu wengine.
Nimeazimia kwa moyo mmoja nimrudishe japo sikupenda hili lakini imenilazimu. Kesho kutakuwa na kikao...

Nitawajuza yote.
 
Mimi ktk maisha yangu nimeamua kuishi Kibinafsi (selfish) upuuzi wa kulea watoto wa watu sitaki. Wazazi wangu wamelea watu wengi sana ambao waliwasumbua sana ni vile wana uvumilivu na ulokole, the way walivyokua wanasumbua wazaz wangu NIMEAPA SITAKUJA KULEA AU KUISHI NA MTOTO WA NDUGU ZANGU HATA WAFIWE NA WAZAZ WAO... Ndugu acha kuharibu familia yako kwa kuishi na litoto jizi lenye wazaz fukuza kama mbwa arudi kwao. Hizo lawama za nduguzo zipotezee zisikusumbue. Sasa hivi utasikia ameuawa kwa wizi
 
Huyo mtoto aliletwa kwako akiwa na umri gani na Darasa la Ngapi? Tuanzie hapo .
Kama aliletwa akiwa mkubwa miaka 7 plus jua Wizi alianzia kwao. Na huenda ikawa ndiyo sababu Baba yake alikusukumia. Ningekuwa wewe ningeshamrudisha kwao tena napeleka mwenyewe. Na kwangu napiga stop. Ukiendekeza iko siku stakujia na majambazi. Kifupi Kwa umri huo jua akifika F4 tayari ni jambazi.
Tofauti na hapo kama bado unamhitaji huyo mtoto peleka rehabilitation centre kwa counselling. Pole Sana
 
We nae vipi? Mbebe mpelele kwa wazazi wake,kama ni kumsomesha msomeshe akiwa mbali
 
Ndiyo msimamo wangu!

Ada itatumwa huko, aishi na wazazi wake, waleane wao!
Nimelea watoto wa braza, tamaa tupu, tokea primary mpaka chuo mwizi mbaya zaidi mkubwa wa kike! Mdogo wa kiume naye tabia zile zile! Huyo nilimshtukia mapema, nikamrudisha kwao fasta!
Huyo binti ukimuona mpole mnyenyekevu, lakini ana mkono balaah, tumefukuza wadada wa kazi Kwa kuwatuhumu vitu hawakuwahi kufanya! Tunakuja kushtuka ni huyu binti, smart anatumia loophole ya wadada na wakaka wakiwa wengi hapo nyumbani!

Alikuwa anatuibia bila huruma!

Huwa sitaki hata kumuona! Kwa maumivu aliyotupa!
 
Naungana nawe, mamangu alinishawishi na mie niliona ni faraja Sana kulea watoto wa ndugu kama wazazi wetu enzi hizo!
Ila usumbufu walioupata, ndiyo niliyosoma naupata tena mara 2 yake,

Msaada utawakuta huko majumbani kwao, kwangu likizo siku 3 zinatosha, sitaki kesi! Waweza ua bila kukusudia!
 
Mwache tu aendelee kuiba, walimwengu tutamfunza adabu tu....it's just a matter of time.
 
Mkuu nikuulize kwenye ukoo wenu kuna tabia ama vinasaba vya wizi? Kwanini kaka yako kakupa wewe ukae na mtoto wake? Kuna kisa kimoja kilitokea ukoo wa jamaa yangu mmoja ni wastaarabu sana tena sana, mjomba wake katika kuhangaika huko akawaletea mtoto. Tabia za yule mtoto na ile familia ni tofauti sana. Ikabidi wakate shauri kupata ukweli wakaenda kupima vinasaba ikaja kutambulika yule mtoto sio wa yule mjomba. Ebu fanyeni hivyo unaweza kukuta mmeingiza kizazi sio chenu.
 
mrudishe kwa baba ake akafanyiwe tiba mila za kwao atakuwa kabeba tabia mbaya za wazee wenu,uyo atakuja kupigwa na watu afe tu,

Utapiga utaua ila tabia itabaki pale pale kuna tatizo ktk ukoo wenu. Pia mtafutie shule za watutkutu atanyooka

Siku mtegeshee pesa ukamate ed handed unamlamba mikwaju ya mgongoni tu yakutosha,hakikisha anajikunja kama nyoka,
Au unalipakaza panga tomato alafu unamlamba nalo ubapa mgongoni au ile rangi ya nyama na maji
 
Hawataki watasema mimi ni mchoyo na mbinafsi huyu ni kama mwanangu
Umesema Ni Kama mwanao...

Sio mwanao Ni Kama tu..sasa mrudishe kwa wenye mwana wao!

Au tuseme Ni wako Ila hujasema hapa..

Ni ngumu Sana kumrekebisha wewe.. yatazuka mengi tu!
 
Mchukue na baba yake uishi nae ili aone mambo anayofanya mwanae afu mshauriane nini cha kufanya
 
Yani mtoto sio wako..!
Anafanya wizi wa kiasi hiki?
..pole sana...nadhani ukimrudisha kwa mzazi wake utakuwa na amani sana
 
Nimeongea na dogo hapa sasa hivi nimemwambia nimrudishe kwa baba amekataa kabisa analia anadai nimsamehe harudii tena lakini alishaomba msamaha mara nyingi Sana

naumia Sana nampenda huyu ni damu yangu kabisa.
Huna haja ya kuongea nae, huyo unamchukua kama mnaenda kutembea ukiwa na furaha tele ukifika unamkabidhi na kurudi zako!
 
Malezi hayako vizuri mkuu, kwa siku mama/baba anakaa mara ngapi na watoto na kuzungumza nao, pamoja na kuwaasa?
 
Umenikumbusha rafiki yangu mkameruni, shemeji yake alizaa akamtelekeza mwanae akawa chokoraa yeye kwa huruma akaenda akamchukua akamlea akamsomesha mpaka kidato cha pili dogo akakataa shule akampeleka ufundi wa kuchomelea dogo akawa tundi halafu kibaka, kibaka tena wale wanaiba bajaj na pikipiki.
Ukikutana naye mchana innocent tena sharobaro flani ila ukikutana naye akiwa kazini anaweza hata kukuua.
Mwisho akadakwa na polisi wakati wanampeleka awaonyeshe eneo la tukio akiwa na pingu aliruka kwenye gari akakimbia.
Baba yake huyo aliyemtelekeza eti anamlaumu jamaa kuwa amemharibia mtoto wakati jamaa ni very strict kajitahidi kadri alivyoweza kumlea.
Kulea watoto wa watu kunaambatana na lawama nyingi. Kuna muda kama wazazi wako hai wabebe mzigo wao
 
Malezi hayako vizuri mkuu, kwa siku mama/baba anakaa mara ngapi na watoto na kuzungumza nao, pamoja na kuwaasa?
Mkuu mara nyingine ni kwa kudra tu, unaweza fanya kila kitu lakini bado mtoto akawa ndivyo sivyo, utaskia wanasema huyu kamfuata mjomba wake yule aliyechomwa moto 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…