Ushauri Msiba wa mkwe na mdogo wake na maziko siku moja je aende kumzika nani

Ushauri Msiba wa mkwe na mdogo wake na maziko siku moja je aende kumzika nani

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wadau kuna ndugu yetu mmoja anapitia wakati mgumu sana mimi Jana kanipigia nimeongea nae nimeshindwa kwakweli kumpa ushauri hali iko hivi ana msiba wa mdogo wake anayemfuata uku akapata tena msiba wa mkwewe baba wa mkewe.

Kwa bahati mbaya maziko ni siku moja maeneo tofauti baba mkwe anaenda kuzikwa malinyi na mdogo wake anazikwa mtwara.sasa ndugu wapo wanamsikilizia waone ataenda kumzika mkwewe amuache mdogo wake au atamzika mdogo wake amuache mkewe akamzike baba yake peke yake?

Aiseee jamaa anaipita wakati mgumu sana.
 
Baba mkwe ana ndugu zake pia kama ilivyo ndugu yake alivyo na ndugu zake akiwemo yeye.

Binafsi ningeenda kuzika ndugu yangu, kama ni mengine yatajulikana kiliko kufurahisha mashemeji deep down naumia
 
Mbona simple tu: Mke atangulie kumzika baba yake yeye nae akamzike mdogo wake akimaliza ataenda kusalimia ukweni ... Yaani msiba wa damu yake auache kisa mkwe aache utoto! Mpe mkeo nauli atakuwakilisha kwenye mazishi na wewe nenda kwenu ukazike mdogo wako we vipi?! ...Alaaaa!
 
Uyo jamaa yako kaomba kabisa ushauri kwa jambo hilo?

Alafu cha ajabu zaidi na wewe ukashindwa kushauri kweli kabisaaa?

Nimesikitika sana mwanaume kuomba ushauri kwenye jambo kama hilo. Bahati mbaya aliemuomba nae kashindwa yaani nabaki nahuzunika huku nacheka.
 
Kwanza msiba umetokea nyumbani kwake alafu aende kuzika ukweni? Kwanza unamzika wa nyumbani kisha unaenda zika ndugu na majamaa huko.

Kwa sababu anaweza kwenda toa pole kabla ya matanga kuisha. Msiba sio kuzika tu hata matanga bado ni mda wa maombolezo unaweza enda shiriki hujachelewa. .
 
Back
Top Bottom