weka namba mkuu tufanye biasharaNinaleta hizo mashine toka UK na Germany (used) na kuziuza hapo Dar na mikoa ya jirani. Chinese products zipo madukani hapo Dar lakini durability yake ni ndogo sana. Kuna vijana wanaosha magari makubwa kule Kurasini, walikuja kwenye yard yangu mara ya kwanza na walipoona ni used machine wakaziacha na kuamua kuingia madukani kununua mashine mpya za mchina kwa 2.5M Tsh, baada ya miezi miwili walikuja tena kwangu na mpaka sasa wanadunda mzigo kama kazi na wamekuwa wananipa oda mara kwa mara. Kwa sasa nina mashine mbili zimebaki pale yard. Ni PM tuwasiliane ili nikupe maelezo zaidi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nmecheka kwa uchungu sana. Daah yani ukianzisha mada za hivi hawaji kabisa. Bora wakuu mmeliona hiliAjabu mada sensitive kama hizi masaa mawili post hata hazifiki 15 ila sasa mwendawazimu mmoja aanzishe uzi hapa akizungumzia ukubwa wa makalio au udogo wa maumbile ya kiume ndani ya 30minute utakuta unasoma pages 4.
Sijui Watanzania maisha tunayachukuliaje!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nmecheka kwa uchungu sana. Daah yani ukianzisha mada za hivi hawaji kabisa, bora wakuu mmeliona hili
Aiseee kuna uwezekano hii biashara inalipaUSHAURI WA VIFAA VINAVYOHITAJIKA
Vifaa vinavyohitajika kwa kuanzia ni Pressure Washer hii bei yake inategemeana na ukubwa wa mashine yenyewe lakini niliwahi kuona moja Jengo la NHC posta Bei ikiwa ni laki sita kama miaka mitatu nyuma.
Kifaa kingine ni Vacuum hiki ni kwaajili ya kuvuta uchafu ndani nayo bei yake inategemea. Tatu MAJI unafikiria kazi au biashara hii basi ufikirie maji ya uhakika kama hakuna maji ya Dawasco basi kwa Dar kuna wale wanaouza kwenye Makenta.
Eneo ambapo biashara hii utaifanya hapa bei inategemea na eneo na mwenye eneo. Lakini pia kingine ni Sabuni maalumu za kuoshea magari hizi sifahamu wapo zinapatikana na bei zake sifahamu.
Vijana wa kufanya nao kazi ambao watakuwa wanaosha malipo mtakubaliana
Vitambaa vya kuoshea na kufutia magari
Polish na Airfresh
Baada ya hapo bei nadhani zinajulikana japokuwa zinatofautiana sehemu na sehemu lakini bei nayofahamu mimi ni Shilingi Elfu 10 kwa gari ndogo hizi Sedan, SUV hatchback nk.
Mengi nadhani wapo wanaoweza kuongezea kila la heri katika kulifanikisha hili
Watakuelekeza mpaka mjumbe wao wa nyumba 10Au hata huu huu uzi we sema una car wash yako, unahotaji wafanyakazi ila wawe mabinti wenye makalio makubwa na unaulizia wapi utawapata, utaona mtiririko wa mauzoefu [emoji28]
Asante mkuuPamoja n vitu vyote mara nyingi watu hupenda carwash yenye vijana waaminifu ukiacha simu unaikuta.
Pia carwash itaongeza ushawishi ukiwa na krestng place kenyw kuuza vnywaj na bites.
Usisahau anagalau sehemu ya kujaza kaupepo.
Changamoto ni zipi hasa?Location ndio kitu cha msingi hayo mengine yatafatia
Poleni mihangaiko wakuu.
Nina idea ya kuanzisha biashara ya kuosha magari (car wash) ya kisasa kati ya mikoa mitatu i.e Dar Es Salaam, Tanga au Pwani (Kibaha/Mlandizi) sasa ningependa kujua mlolongo wa gharama za uanzishaji lakini pia uendeshaji wake kwa maana ya (management) lakini pia bila kusahau Faida zake na changamoto zake. Binafsi Pesa ya capital itapatikana na ipo tu ya kutosha. Nakaribisha maoni na ushauri wenu wakuu. Ahsanteni!!!
Shukrani sana kwa mchango mkuu Ubarikiwe sana. Nadhani naaza kupata mwanga wa pa kuanzia.Sina sana experience. Ila naweza shauri kitu hapo.
Kwanza Uwe na pressure washer. Ukipata za umeme naona ni nzuri zaidi ukicompare na zile za kutumia mafuta.
Ukiweza kutega eneo la karibu na barabara nadhani itakuwa safi zaidi. Halafu unaweza ukaweka na huduma ya choo cha kulipia hapo hapo kwa ambao watakuwa sio wateja wako.
Penye wengi hapaharibiki neno. Wengine watakuja kujazia.
Ubarikiwe sana mkuu. Umenipa madini ya kuanzia. Shukaran sana.Kuhusu iyo biashara, Mtaji ni pressure washer na Eneo ( Paved area) issue ya kuandaa eneo tunaweza tusiwe na gharama bayana ila unaweza tafuta eneo la kukodi au kununua kisha ukasakafia kwa zege na kuweka Lanes kama 4 hivi kwa ajili ya kuosha magari watatu au manne kwa wakati mmoja. Tafuta bati, tengeneza cannopy vizuri mambo yawe sawa
Karibu mkuuUbarikiwe sana mkuu...umenipa madini ya kuanzia. Shukaran sana.