Ushauri na Mbinu Mbalimbali Kuhusu Uendeshaji wa Biashara ya Kuosha Magari (Car Wash)

Ushauri na Mbinu Mbalimbali Kuhusu Uendeshaji wa Biashara ya Kuosha Magari (Car Wash)

Aiseee hongera,ukipata uhakika wa kijanà mwaminifu ,na sehem nzuri /open space ndo vigezo vya awali ktk hii biashara.

Kuhus bei tusubir wajuv
 
wakuu ina maana hamna anayejua chochote khs hii idea au ni wivu tu wa kutopeana michongo.....njooni huku wengi tutanufaika kwa hili
 
wanaouza hizi mashine pia karibuni ......
bei na aina zake... ni aina gani ambayo ni nzuri zaidi
 
Mashine ya nn mkuu wakati tafuta matambala mawili na brush kwa ajiri ya kusugulia makapeti na tairi na ndoo kwishiney
 
Tafuta compressor za Ingesol Rand (IR)-msouth huyu.. Bei zinarange 2m - 4m kulingana na ukubwa wa biashara yako!..Ukihitaji used nitafute 😀.
Kuhusu mashine ya kuoshea nazani kwa bei ya sasa unaweza pata hadi kwa 2M mpya ila ndogo!
 
Ebwana wasalam wana jukwaa,

Kama ada ya jukwaa hili uhai wake upo kwenye kureta vitu na majambo yenye tija kwa dhumuni la wote tuondokane na maisha haya ya kimaskini na kuweza kuishi maisha yenye tija.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuna vitu vingi vyenye tija na vinavyolipa katika maisha lakini vitu vingi, biashara nyingi zinazolipa zinahiataji pesa za kutosha kuwekeza hivyo kwa sisi maskini inakuwa ni vigumu sana kuweza hata kukalibia biashara hizo.

Lakini pia kutokana na uwezo wetu mdogo wa kimaskini na sisi kuna biashara zenye tija ambazo kwa level zetu tukijibana na kujitutumua tunaweza kuzifanya na kutoka kwenye haya maisha kwa njia yoyote ile moja ya biashara hiyo ni car wash.

Hakuna mjuzi sana wa mambo humu pia hakuna anayejua kila kitu ila hii haisababishi wewe kutokujua vitu kwa uchunguzi wangu hii biashara inalipa sana kutoka kwenye sources mbalimbali ila hapa nataka kujua tu je jumla mzima ya mtaji wa project hii ya car wash ukijumuisha vitu vyote.

Hapa nazungumzia mfano zile kidogo modern kama za kwenye shell mbalimbali mijini, napenda nijue hicho ili nianze movement zangu hivi sasa za kuzisaka hizo pesa sasa hivi.

Kwa anayejua anieleze tu minimum shilingi ngapi na maximum shilingi ngapi bila kuanisha nini na nini kinaitajika.

OCTOBER MAN

NAWASILISHA
 
Mazee hii mambo hili ikulipe vizuri inatakiwa iwe mjini kati tena upate eno la kutosha.

Kodi ya hapo sio ya kitoto
 
Bahati nzuri sana nnafanya biashara ya Car wash ila ina changamoto yake, haswa kipindi cha mvua kuna changamoto maana watu hawaoshi magar sana, pili vifaa kidogo ni ghali sema ukijipanga unanunua, kinachozingua zaid ni kodi asee wenye maeneo mjini wanatuua kwa bei kubwa
 
Bahati nzuri sana nnafanya biashara ya Car wash ila ina changamoto yake, haswa kipindi cha mvua kuna changamoto maana watu hawaoshi magar sana, pili vifaa kidogo ni ghali sema ukijipanga unanunua, kinachozingua zaid ni kodi asee wenye maeneo mjini wanatuua kwa bei kubwa

mtaj kwa jumla ulitumia saa ngapi mkuu ukijumuisha vitu vyote
 
Back
Top Bottom