Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Hizo gari zimefanywa kama kitu cha ajabu sana kwa wamiliki kiasi kwamba wanapigwa sana kwenye maintanance. Hio fursa iko siku ntaitumia.
 
Hapo umeeleweka.
 
Hizi BMW zioneni hivi hivi tu asee, nilipasua Headlight nikataka kununua mpya nilivyoambiwa bei ya Taa mpya mwenyewe nikakimbilia Ilala kwenda kubadilisha lens kwa laki na nusu nikaweka na mastika chomba kikarudi kwenye ubora wake

Mvua si ikavyesha bhana headlight ikaanza kuingiza mvuke, Yani ule mvuke kidogo tu uloingia ndani Taa kwenye Dashboard ikawaka....hapa nina Mpango wa kununua Taa mpyaView attachment 2454161
 
Unaishi nchi gani?.
 
Kwa bwana Jesse, ndio huyo unaesema ni Mzungu?
 
Oil za Mjerumani ni 10kkm wanazoshauri sasa kusema oil 3k km kubadilisha. Napata ukakasi ila sio big deal. Kimfaacho mtu chake na mimi sio fundi makanika

Hii huwa ni maneno ya kibiashara tu hayo...

Mimi natumia Liqui Moly na namwaga oil wastani wa km 3000, lakini huwa nakuta oil ni chafu na imepungua sana tu...
 
Kwa bwana Jesse, ndio huyo unaesema ni Mzungu?

Jesse ni Automax na ni mchina mbongo, garage yake ipo karibu na Garda...lakini hawa jamaa nina experience nao mbaya washaua injini na gearbox kwenye gari yangu, washawahi badilisha battery ya gari, washaua hydraulic lever za bonnet

Atlantic ni wengine kabisa wapo huku karibu na Hekima...
 
Bro unajua kazi ya sensor wewe?

Unajua maana ya Fault?

Kwa hiyo tairi kupungua upepo halafu TPMS sensor ikakuambia low pressure hiyo siyo fault?
Alichomaanisha Bob sambeke ni kuwa vitu vingine ni visababishi vya tatizo haviwezi kuonekana kwenye sensa isipokuwa sensa itakuonesha baada ya kupata tatizo.

Mfano kuna msumari upo karibu na tairi, ukifanya ukaguzi kabla utaweza kuutoa na sio kusubiri uukanyage tairi litoboke ili upewe taarifa kwenye dashboard.
 
Jesse ni Automax na ni mchina mbongo...
Okay. At least jamaa bei zake sio kali kama hao Atlantic na anakupigisha story kuhusu gari yako, unaondoka na uelewa sio kama hao Atlantic, wamemuongezea jamaa maswali badala ya kumpunguzia wasiwasi. Elfu 60 ilikuwa ni karibu filter 2
 
Wanakaza kichwa? Inaeza kuwa hata kamba au liwaya flani , au li tawi la mti Niko chini ya gari sometime hata chatu anaweza fika kwenye Bonet kufata joto la engine! Je hapo dash itaonesha hivo vitu? Ukute kamba imejizungusha kwenye otoneta dash itaonesha? Au mpaka tatizo litokee

Sina bmw ila ukaguzi Ni muhimu
 
Ni swala la muda tu, I hope mjerumani atafanya improvement kwenye Sensor kutambua hatari zijazo kabla hazijatokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…