Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Ushauri namna ya kufanya Service BMW X3

Bila shaka ni yule wa karibu na HK Hospital! Yaani hawa jamaa ukienda na vitu vyako, wananuna!

Nishasema humu, kama una Euro make, inabidi ujiongeze haswa kwa suala la kuijua gari yako, nini inataka na wapi utapata vifaa na lubricants. La sivyo utageuzwa gari la mshahara!
Hizo gari zimefanywa kama kitu cha ajabu sana kwa wamiliki kiasi kwamba wanapigwa sana kwenye maintanance. Hio fursa iko siku ntaitumia.
 
Huwa namwaga oil baada ya km 3000 Ila hata kama napitiliza Hadi km 4000 haina shida Sana kwasababu oil bado inakuwa iko vizuri Tu.. kumbuka kuna watu wanaenda Hadi km 7000 Ila Mimi ambaye nimepata elimu kupitia hapa JF naishia km 4000 na hiyo ni TOTAL OIL 5W - 40 full authentic
Hapo umeeleweka.
 
Hizi BMW zioneni hivi hivi tu asee, nilipasua Headlight nikataka kununua mpya nilivyoambiwa bei ya Taa mpya mwenyewe nikakimbilia Ilala kwenda kubadilisha lens kwa laki na nusu nikaweka na mastika chomba kikarudi kwenye ubora wake

Mvua si ikavyesha bhana headlight ikaanza kuingiza mvuke, Yani ule mvuke kidogo tu uloingia ndani Taa kwenye Dashboard ikawaka....hapa nina Mpango wa kununua Taa mpyaView attachment 2454161
IMG_20221220_154734_727.jpg
 
Vitu muhimu vya kuzingatia kwa BMW.

Gari lina km ngapi?

Unalipeleka service kwa BMW authorized dealer?

Mimi X3 langu lilivyokaribia 100,000 miles, at just about 90,000 miles nililitosa nikachukua X5.
Baada ya hapo niliona litanisumbua tu.

Halafu service siku zote kwa authorized dealer.

Halafu vitu vyote by the book, kuanzia petroli mpaka oil vile vile iliyoandikwa kitabuni.

Hapo utalifurahia BMW.
Unaishi nchi gani?.
 
Google Atlantic ipo Mikocheni Coca-cola karibu na GSM iliyoungua, halafu Rudi hapa uniambie kama ni wa mtaani, Picha linaanza nilivyoenda kwa mara ya kwanza nimekabidhi funguo reception naona mzungu ndio anakabidhiwa funguo akaishughulikie gari maana ndio ilikuwa imetua Bongo

Niliacha milion 1 na laki 2 kuchekiwa tu Kila Kitu kama Kiko sawa na vilivyo badilishwa ni oil filter na Air filter basi
Kwa bwana Jesse, ndio huyo unaesema ni Mzungu?
 
Oil za Mjerumani ni 10kkm wanazoshauri sasa kusema oil 3k km kubadilisha. Napata ukakasi ila sio big deal. Kimfaacho mtu chake na mimi sio fundi makanika

Hii huwa ni maneno ya kibiashara tu hayo...

Mimi natumia Liqui Moly na namwaga oil wastani wa km 3000, lakini huwa nakuta oil ni chafu na imepungua sana tu...
 
Kwa bwana Jesse, ndio huyo unaesema ni Mzungu?

Jesse ni Automax na ni mchina mbongo, garage yake ipo karibu na Garda...lakini hawa jamaa nina experience nao mbaya washaua injini na gearbox kwenye gari yangu, washawahi badilisha battery ya gari, washaua hydraulic lever za bonnet

Atlantic ni wengine kabisa wapo huku karibu na Hekima...
 
Bro unajua kazi ya sensor wewe?

Unajua maana ya Fault?

Kwa hiyo tairi kupungua upepo halafu TPMS sensor ikakuambia low pressure hiyo siyo fault?
Alichomaanisha Bob sambeke ni kuwa vitu vingine ni visababishi vya tatizo haviwezi kuonekana kwenye sensa isipokuwa sensa itakuonesha baada ya kupata tatizo.

Mfano kuna msumari upo karibu na tairi, ukifanya ukaguzi kabla utaweza kuutoa na sio kusubiri uukanyage tairi litoboke ili upewe taarifa kwenye dashboard.
 
Jesse ni Automax na ni mchina mbongo...
Okay. At least jamaa bei zake sio kali kama hao Atlantic na anakupigisha story kuhusu gari yako, unaondoka na uelewa sio kama hao Atlantic, wamemuongezea jamaa maswali badala ya kumpunguzia wasiwasi. Elfu 60 ilikuwa ni karibu filter 2
 
Alichomaanisha Bob sambeke ni kuwa vitu vingine ni visababishi vya tatizo haviwezi kuonekana kwenye sensa isipokuwa sensa itakuonesha baada ya kupata tatizo.

Mfano kuna msumari upo karibu na tairi, ukifanya ukaguzi kabla utaweza kuutoa na sio kusubiri uukanyage tairi litoboke ili upewe taarifa kwenye dashboard.
Wanakaza kichwa? Inaeza kuwa hata kamba au liwaya flani , au li tawi la mti Niko chini ya gari sometime hata chatu anaweza fika kwenye Bonet kufata joto la engine! Je hapo dash itaonesha hivo vitu? Ukute kamba imejizungusha kwenye otoneta dash itaonesha? Au mpaka tatizo litokee

Sina bmw ila ukaguzi Ni muhimu
 
Alichomaanisha Bob sambeke ni kuwa vitu vingine ni visababishi vya tatizo haviwezi kuonekana kwenye sensa isipokuwa sensa itakuonesha baada ya kupata tatizo.

Mfano kuna msumari upo karibu na tairi, ukifanya ukaguzi kabla utaweza kuutoa na sio kusubiri uukanyage tairi litoboke ili upewe taarifa kwenye dashboard.
Ni swala la muda tu, I hope mjerumani atafanya improvement kwenye Sensor kutambua hatari zijazo kabla hazijatokea
 
Back
Top Bottom