USHAURI: Nani asimame kati ya Baba mlezi na Baba mzazi kwenye send off na harusi!!

Ya Iringa ifanyike na ya Dar ifanyike.
 

Hapana wote hawashirikishe, kisha ifanyike kwa baba mlezi
 
Kutia mimba bila matunzo ya mtoto ni ufedhuli. Anayestajili Zawadi na kuandaa send off ni Baba mlezi. Baba mtoa mbegu na kusepa aalikwe kama mgeni tu. Ila ingekuwa Mimi ningemkalisha na Baba mlezi wote high table Ila sifa zote kwa mlezi wangu. Iwe fundisho kwa wagawa mbegu wote. Hivi Mimi Zogwale nitaachaje mtoto wangu bila kumtunza na kumsomesha? Hata kama mama yake tumetengana au kuzaa tu pembeni yaani mtoto namtunza Sawa kabisa na mtoto ndani ya ndoa hata kama siishi naye. Funza adabu huyo Mbwa mgawa mbegu maana ni Mbwa na kuku au wanyamaa wa kiume pekee hawatunzi watoto Kwa asili yao. Japo wapo jogoo wachache wanajali vifaranga
 
Afanye kwa baba mlezi maana ndio aliyemlea. Huyo mwingine ni sperm donor tuu. Uzuri wa watoto wa siku hizi kama baba ulimwacha udogoni ukubwani naye anakupa doubt.
Nakazia na spanner Pipe Range kabisa . Funza adabu sperm donors
 
Duh, hapo kweli kazi ipo.
Jamani wanaume mjifunze. Msikimbie majukum hata kama una tofauti na mzazi mwenzio ujue mtoto hana hatia. Kitanda hakizai haramu.
 
Huyo Binti anaelewa maana ya Baba?

Kama anaelewa basi hakukuwa na sababu ya kujiuliza.

Baba ni yule anayehusika na majukumu ya baba na nafasi yake Kwa mwanae kama mwanaume.

Mwambie atuwekee namba ya baba mlezi tuanze kumtumia zawadi zingine wakati anasubiri ampe gari.
 
Mtu haitwi baba kisa amekulea kama ni hivyo wajomba kibao wangestahili hiyo Title.

Mtu anaitwa baba ikiwa amekusababishia wewe kuwepo duniani kifupi mbegu imetoka kiunoni mwake.

Sasa unajiuliza nini peleka kwa baba mwenyewe afurahie uwepo wako
Baba yeye alifurahia uwepo wa mwanae? Alisimama kama baba Kwa mwanae?

Kuna mtoa mbegu na Kuna baba tujifunze kutofautisha.
 
Watu wemgi wanamshauri kuwa Aende kwa Baba mzazi.
Kwa sababu ni mzazi mwenye mtoto.
Kifupi shughuli.zote zifanyike.aliko.mama yake mzazi full stop

Posa ,mahari ziende straight kwa mama mzazi na nduguze na send off ifsnyike.kwa mama yake

Kuzaa sio issue hata tumbili huzaa

Kutunza ndio kitu muhimu

Huyo baba mzazi aalikwe tu kuhudhuria hayo matukio yanayofanyika kwa mama yake
 
Mtu haitwi baba kisa amekulea kama ni hivyo wajomba kibao wangestahili hiyo Title.

Mtu anaitwa baba ikiwa amekusababishia wewe kuwepo duniani kifupi mbegu imetoka kiunoni mwake.

Sasa unajiuliza nini peleka kwa baba mwenyewe afurahie uwepo wako
Na zawadi ya alphard je kwa Baba mlezi
 
Tumeshachoka kuwashauri kitu kimoja kila siku.

Kwenye complication ya Wazazi swala la mahari linasimamiwa na wajomba, msijitafutie laana ambazo baadaye mtaona mmelogwa kumbe hamna akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…