Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Unaendeleaje Auntie?Nilikuwa kwenye serious relationship miaka 3 hivi na tulipanga tufunge ndoa mwaka huu baada ya kuwa mbali akaamua kurudiana na ex wake na mwisho akakubali kuwa kweli wamerudiana na kizuri zaidi alisema sijawahi mkwaza na hakuwa na sabbu ya msingi ya kunifanyia hivyo nikaona Riziki tu kumbe Ilikuwa imeisha maisha yaendelee.
Ila nilikuwa nawapenda sana yeye familia yake na hata mtoto wake na nilikuwa nawaona kama ndugu zangu kabisa lakini baada ya hayo sitaki mazoea nae kabisa niishi maisha yangu.
Shida ni kuwa analazimisha tuwe karibu na mm nilishakataa nishamblock mara kadhaa lakini atatafuta namba anipigie mara anitext nikaona nimuunblock tu
Ndugu zake Bado wananitafuta mara hivi mara hivi, naona wananirudisha nyuma Kila wakati. Mnipe mbinu mpya sitaki kusikia habari zao kabisa.
Njia nzuri ni kutokujibu chochote.
Mtu aliyehiari kukuacha usipoteze hata sekunde yako moja kujibu chochote kile.
Na nyie mbwa mnaowaacha wenzenu halafu mnajidai kupiga piga simu na kutuma vimeseji vya salamu aloo mkome.