Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,650
- 6,015
Habari wana jamvi.
Kijana wenu nikiwa na umri wangu wa miaka 33 kamili, nimedhamiria kwa hiyari yangu mwenyewe, bila kushurutishwa wala kushawishiwa na mtu yeyote; kuacha kula kabisa vyakula vyenge wanga. Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni kama mahindi, mpunga, mihogo, viazi, magimbi, ngano, mtama n.k
Inaaminika kisayansi vyakula hivi vikitumika kwa wingi vinasababisha sana kitambi na unene, kisukari na magonjwa ya moyo.
Juzi Jumatatu, 21.03.22 nikaanza movement yangu bila kuwa na mpango maalum. Asubuhi sikujua ntakula nini...mpaka imefika saa 5 sijala kitu. Sehemu za kula zote zina vitafunwa tulivyovizoea maandazi, chapati, vitumbua, mikate, viazi, mihogo and the likes. Ikafika saa 7 njaa inauma vibaya sana mpaka nikahisi kutetemeka mwili.
Nikajisemea cha kufia nini? Nikala zangu dona safi, nyama, maharage na spinach. Baadae nikawa nakunywa tu maji.
Sasa najiona kabisa sina plan na sielewi hii game inachezwaje. Najua humu kuna wazoefu wa haya mambo. Naomba mnisaidie wenzangu msiokula wanga ama heavy meals mnafanyaje?
Mnakula nini hasa? Na mliishindaje njaa hizi siku za mwanzo mpaka tumbo lizoee? Maana ile juzi nilihisi mpaka kizungu zungu.
Mimi napenda sana nyama iwe ya kuku, ng'ombe, mbuzi, kuku n.k. Ndio udhaifu wangu mkubwa.
Nipeni ushauri wadau. Hili ndio lengo la uzi.
Asanteni.
NB: sina ugonjwa wowote unaonizuia kula chochote.