Ushauri: Nataka kuacha kula wanga kwa mwaka mzima

Nna kilo 75, na uzito huu sijazidi wala kupungua kwa miaka karibia 3 sasa.
 
Vyakula vya wanga ndio source ya energy kwenye mwili wako .

How are u going to survive without carbs?
Mi sili wanga napata nguvu kutoka kwenye vyakula vya mafuta kama nyama ,mayai ,maziwa na mazoezini walaji wa wanga nawashinda
 
Asije kuwa kama mtoto wa willy smith baada ya kuamua kuwa vegetarian akapata utapi wa mlo mpala wazazi kuingilia kati kumuokoa
Vegetarian sio mfumo sahihi unakosa virutubisho vingi hasa protein
 
Nani kakukaririsha hayo matango Pori mkuu? Kwa hiyo Kwa uelewa wako uadhani sukari haihitajiki mwilini?
Mwili unazalisha sukari wenyewe inayotoshekeza mahitaji ya mwili, mimi sili sukari kabisa
 
Haya niambie ni chakula gani hicho?
Mimi si wa kwanza kuacha kula wanga. Na nimekuita hapa unishauri. Kama unaona nakosea unasema nipunguze. Sio kuleta kashfa mkuu. Tuheshimiane.
Mi niko na wewe siumwi lakini sili wanga, sijasubiri nipate kisukari ndio nibague vyakula hata profesa janabi wa jk cardiac institute hali wanga na anashauri watu waache
 
Kuna huyu jamaa wa apple aliamua kuishi maisha yake yote akiwa anakula matunda tu, alikufa.

Ishu ni kwamba kila aina ya kirutubisho mwili unakihitaji so kuamua kustick na aina fulani tu ya virutubisho hapo ni kujiandalia kifo.
Kama alikula matunda tu hakua sahihi sababu hayaleti enegi yoyote lakini kuacha wanga ni idea nzuri sababu kazi ya wanga ni kuleta energy ambayo utaipata kwenye mafuta
 
Sio kweli kuna mtumishi mwenzetu ni mtu mzima mama wa 50 hivi kafuata lishe ya dr boaz mkumbo bila kufanya zoezi lolote na amepungua kilo 23
 
Hahaaa ukiacha sukari unapata madhara? Hii kali nadhani ulikua na shida nyingine mi nimeacha sukari 2018 na afya yangu inazidi kuimarika
 
Dr boaz amesaidia wengi sana nikiwemo mimi, nimepata elimu kubwa kupitia yeye mwanzo nilikua sijui kua wanga na sukari inaweza kuleta ugumba
 
Kitimoto hakina shida mi nakula sana, mfollow dr boaz mkumbo atakusaidia sana
 
Sio kweli mi nimeacha wanga na nina nguvu za kutosha na mazoezini walaji wa wanga mbona nawazidi msome dr boaz mkumbo amesaidia wengi kwa elimu yake ya kuacha wanga na sukari, by the way kila mtu atachagua mfumo anaoona unafaa sababu miili inatofautiana mimi nikila wanga hata kidogo matokeo yanachukua muda mrefu na baadae nanenepa sana, na baada ya kuacha wanga sipati njaa za mara kwa mara kama mwanzo
 
Kama una mke utasaidiwa kula mzigo,punguza wanga lakini usiache kabisa.
 
Eti tuache kutumia Mafuta ya Karanga,Soya au korosho,halafu sababu hatoii kisa tu ni mbeguu. Hapana aisee...

Tutatumia mafuta ya mimea Kwa wingi ya wanyamaa tutatumia kidogo.
Mafuta ya mbegu mengi hayahimili moto mkali yanazalisha sumu zinazoitwa free radicals na pi mengi yana omega 6 fatty acids nyingi kuliko omega 3,mazuri ni siagi, samli, nazi, olive oil
 
Mbona mi nimeepuka wanga
 
United States wanaongoza kulima mahindi karibu acres 90+M wanalima tu mahindi lakin ugali unaongoza kuliwa sana huko usukumani hamna hata maeneo ya kulima hayo mahindi ndo ujue kuwa ugali siyo kitu kizuri
Hujaeleweka. Fafanua
 
Principally, wanga huongeza nguvu katika mwili na ikiwa nyingi mwilini, mwili hubadili wanga kuwa mafuta/fats/lipids for storage purposes. Kwa hiyo kula wanga kulingana na uhitaji wa mwili wako. Km unafanya kazi za nzito wanga lazima ule wanga wa mwingi ili mwili uweze kuzalisha nishati ya kutosha kuwezesha kumudu kufanya kazi nzito. Ila km shughuli zako ni laini huhitahi kula wanga mwingi. Mlo/diet hutegemea sana na shughuli ya mtu afanyayo. Ila hitimisho wanga hauepukiki by anyhow.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…