Mimi hapa nilikua na uzani wa 126kg na kitambi chote nje nje, ila leo hii mara yangu ya mwisho kupima nilikua na 82kgs, maana kwamba nimepunguza sana, yote hii kwa jitihada za kama miaka mitatu.
Kwanza kabisa aliyekuambia uepuke wanga alikupotosha, ni muhimu sana mwili ukapata carbs, kimsingi ni ujue aina gani za carbs ambazo zinaweza kusaidia, kwa mfano epuka mikate mikate maana yenyewe ni simple carbs, inakua digested upesi na kusababisha njaa mapema.
Kula complex carbs kama magimbi, yanakushibisha na kukupea nguvu wala hutamani chakula haraka.
Kula mboga mboga kwa wingi na pia matango na maji mengi.
Ukiepuka wanga kabisa mwili utakua mnyonge mnyonge na mzembe hadi hata kufanya kazi ndogo unapata shida, hata mazoezi yatakushinda.
Kingine, usitegemee matokeo ya haraka, itachukua muda kabla uone au kuhisi chochote, ila komalia humo humo.