USHAURI: Nataka kusafiri na Passo ya Piston 3 ina CC 990, nitaenda umbali wa Km 400

USHAURI: Nataka kusafiri na Passo ya Piston 3 ina CC 990, nitaenda umbali wa Km 400

Wakuu naombeni ushauri, nina safari kidogo kama ya KM 400 kwa siku moja ila sijawahi kusafiri na hiki kigari, ushauri tafadhali...
Unakwenda uzuri kabisa mkuu...
Jambo la msingi ni hakikisha umefanya service ya kawaida kwenye Ingine, pia hakikisha tyre bearings zipo poa (hapo unaweza ukatumia kutikisa kila tairi baada ya kunyeyu kidogo na jeki)
Hakikisha una spare tyre, wheels spanner, fire extinguisher, pembe tatu reflectors, leseni, kadi ya gari na fuata sheria za barabarani.
Nakutakia safari njema mkuu.
 
Nimewahi tokanayo musoma to Dsm non stop na kako powa kabisa mpaka leo hii sasa wewe to km 400 unakuja humu unalialia mwanaume mzima kweli??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaomba ushauri kwa kuwa hajawahi kusafiri na hiyo gari na sio kulialia. Ulivyosema ulisafiri na gari ya aina hiyo MSM- Dar ilitosha kabisa kumuonesha gari ina uwezo.
 
Ndugu yangu huku JF ukiomba ushairi sometimes unaweza kuvujwa moyo..
Gari lolote linapotengenezwa linapitia vigezo vingi sana ili likidhi mahitaji ya standards za kimataifa..
Gari lolote lile unaweza kusafiri nalo bila shida ili mradi liwe zima na ufuate utaratibu.

Tatizo linakuja pale ambapo mtu yupo safari ndefu na passo....brevis inampita mlimani jamaa wa passo anaanza kufukuza...hapo lazima kichemshe.

Gari kama passo kwa udogo wake nakushauri usizidi 110kph kwa safari ya mbali na RPM maximum iwe 3 ila muda mwingi hakikisha RPM ipo chini ya 3 then acha gari ichanganye yenyewe....wenye prado zao waache waende utafika tu.

Ukizingatia hayo kwa passo utasafiri kwenda mbali tu na kurudi salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom