Ndugu yangu huku JF ukiomba ushairi sometimes unaweza kuvujwa moyo..
Gari lolote linapotengenezwa linapitia vigezo vingi sana ili likidhi mahitaji ya standards za kimataifa..
Gari lolote lile unaweza kusafiri nalo bila shida ili mradi liwe zima na ufuate utaratibu.
Tatizo linakuja pale ambapo mtu yupo safari ndefu na passo....brevis inampita mlimani jamaa wa passo anaanza kufukuza...hapo lazima kichemshe.
Gari kama passo kwa udogo wake nakushauri usizidi 110kph kwa safari ya mbali na RPM maximum iwe 3 ila muda mwingi hakikisha RPM ipo chini ya 3 then acha gari ichanganye yenyewe....wenye prado zao waache waende utafika tu.
Ukizingatia hayo kwa passo utasafiri kwenda mbali tu na kurudi salama.
Sent using
Jamii Forums mobile app