Ushauri: Nataka kutafuta "Fundi Juma" mwenye uzoefu wa kujenga ghorofa ili kupunguza gharama

Ushauri: Nataka kutafuta "Fundi Juma" mwenye uzoefu wa kujenga ghorofa ili kupunguza gharama

Unachekesha mkuu. Naongelea from experience tena hapo ni ghorofa 1 ukitaka lipendeleze minimum weka 300m bei ya kununulia kiwanja haihusiki hapo mkuu. Ningekuwa mhaya au kina Dotto ningetuma picha hapa nikuonyeshe ninapoishi
Usi-generalize. Mil 300, au chini ya mil 300 inatosha vizuri Sana. Na sio 300 tu mm nasema mil 200 inatosha na ghorofa linakua zuri tu

Hapa nasema usigeneralize sababu inategemea na aina ya mchoro
Ningekuwekea picha za ghorofa la mil 200, Ila mambo ya mtandaoni haya inakua sio powa.

Ghorofa ni gharama, Ila please msitishe sana na kuongopea watu
 
Habari wakuu,
Mungu akipenda, mwakani natamani kuanza ujenzi wa nyumba ya ghorofa moja.
Mpaka sasa, nimefanya michoro yote, architectural na structural designs.

Naomba ushauri kwa watu wenye uzoefu, nataka kutafuta fundi Juma ambaye ana uzoefu kujenga ghorofa, anisaidie kujenga ili kupunguza gharama. Nataka kujua kama kuna mtu hapa ameshawahi kujenga kwa kutumia fundi wa kawaida.

Pili, naomba msaada kuju makisio bila finishing kwa nyumba ya 98sqm.

Asante kwa muda wenu.
Mkuu wapigie hawa jamaa ni kampuni ya ujenzi wanaitwa MAGATA&H CO.LTD ofisi zao zipo kigamboni mjimwema no zao 0754665045 au wachek instagram wanatumia magata_ltd watakufanyia kazi yako kwa ubora na kwa bei nafuu
 
Habari wakuu,

Mungu akipenda, mwakani natamani kuanza ujenzi wa nyumba ya ghorofa moja. Mpaka sasa, nimefanya michoro yote, architectural na structural designs.

Naomba ushauri kwa watu wenye uzoefu, nataka kutafuta fundi Juma ambaye ana uzoefu kujenga ghorofa, anisaidie kujenga ili kupunguza gharama. Nataka kujua kama kuna mtu hapa ameshawahi kujenga kwa kutumia fundi wa kawaida.

Pili, naomba msaada kuju makisio bila finishing kwa nyumba ya 98sqm.

Asante kwa muda wenu.
Fundi aliyejenga ghorofa ya Mwijaku 0717 544 702 Yusuf, swali la kizushi architectural na structural drawings imekugharimu TSH ngapi mkuu kama hutojali?
 
ushauri wangu kama unajenga gorofa achana na mafundi michael, wala fundi juma utakuja kulia kilio kisichokuwa na jina
Mtafute fundi mchundo ( technician) wale waliosoma dit, arusha tech au must kama kumpata engineer ni garama maana hawa wako more practical zaidi.

Epuka kutumia fundi wa kawaida kwenye ujenzi kama wa gorofa kama utakuwa na fundi wa kawaida ni lazima awe chini ya usimamizi wa mtu technical maana structure na stubility ya goroma inahitaji mtu mwenye knowledge ya structural design kuweza kutransform mawazo ya structural engineer kutoka kwenye mchoro/ karatasi kuja kwenye site. hii ndo sababu gorofa nyingi kukosa ubora hasa zilizopo dar. mtu unachorewa mchoro vizur wenye details unakutana fundi anakushaur ondoa nondo size fulani bila taratibu zakujua endapo marekebisho yoyote yatafanyika kutoka kwenye plan iliyokisudiwa lazima structural engineer athibitishe.
siku hizi kila mtu anataka kuwa engineer tujaribu kuheshimu professional za watu.
 
Usi-generalize. Mil 300, au chini ya mil 300 inatosha vizuri Sana. Na sio 300 tu mm nasema mil 200 inatosha na ghorofa linakua zuri tu

Hapa nasema usigeneralize sababu inategemea na aina ya mchoro
Ningekuwekea picha za ghorofa la mil 200, Ila mambo ya mtandaoni haya inakua sio powa.

Ghorofa ni gharama, Ila please msitishe sana na kuongopea watu
ukiona mtu anataja garama ya nyumba hovyo either ni gorofa au yakawaida huyo hajui protokali za ujenzi. ujenzi sio arts iwe na general principal hivyo haitaji kukariri kwakua kuna factor nyingi sana zinaweza kusema garama halisi. nyumba ukiijenga leo million 200 hiyo nyumba ukaijenga mtaa mwingine haiwezi kuwa garama sawa hata iwe mji mmoja ila mitaa tofauti garama za material sehemu fulani ni tofauti kutokana na availability so huwezi ukajua general garama za nyumba kwa kubuni tu kama majibu ya A,B,C,D katika mtihani wa sanaa
 
Yes ni kweli
 
Yes tumia fundi maiko ila hakikisha unampa kazi ya kusimamia civil engineer mzoefu unakuwa unamlipa consultation fees kila akija site kwako kutoa ushauri. La sivyo utalia bila kupigwa
 
Habari, nakushauri kama utaweza tumia waffle slab,Kuna jirani angu amejenga gorofa kwa garama ndogo sana aliwapata jamaa wanaotumia hizo waffle sikufich nilipenda kuanzia muonekano wa hizo waffles na pia namna ilivyookoa garama maana formwork yake haikuhitaji marine bords na hata idadi ya nondo alitumia chache sana.ushauri kama utapenda kupunguza garama tumia aina hiyo ya slab waffle
 
Kutumia local fundi kujenga ghorofa ni kweli inaokoa gharama, lakini hakikisha awe na uzoefu, pia kuwe na msimamizi anayeweza kumsimamia fundi. Fundi hata awe mzoefu vipi bila kusimamiwa na mtu anayejua(mtaalamu) huwa wanafanya makosa mengi sana
Gharama inategemea na aina ya jengo(drawings)

Swali langu kwa nn watu mnapenda ghorofa? Sijaona sababu sana
Prestige, hata Mimi nataka nijilipue huko mbeleni.
 
Prestige, hata Mimi nataka nijilipue huko mbeleni.
Huko huko mbeleni utaona una mzigo mkubwa sana
Ghorofa zuri but Kuna wakati inafikia linaboa na kukuchosha hasa pale umri ukisogea mambo ya usafi ndani na nje ni changamoto hata uwe na dada wa kazi/houseboy. Maintenance yake huwa ni kuchosha akili tu
 
Na sometime unakuta una eneo zuri ila dogo sasa ukifanya cost benefit analysis unaona bora ujilipue tu ujenge kighorofa ubakie na nafasi ya parking na mambo mengine.
Bongo ni vice versa wenye maeneo makubwa ndio hujenga ghorofa sababu ndio wanaafford kununua maeneo makubwa. Makabwela wenye high density plots huwa hawajengi maghorofa

NB: kkoo special case
 
Ukijenga ghorofa wewe ni 1% ya watanzania, kulingana na takwimu za NBS Majengo ya ghorofa Tanzania hayafiki Laki 5 !Hapo ukiondoa NHC, NSSF, JESHI, POLICE NK. unaweza kubaki na nusu yake Hivyo kwa Tanzania Ghorofa ni la wachache
 
Huko huko mbeleni utaona una mzigo mkubwa sana
Ghorofa zuri but Kuna wakati inafikia linaboa na kukuchosha hasa pale umri ukisogea mambo ya usafi ndani na nje ni changamoto hata uwe na dada wa kazi/houseboy. Maintenance yake huwa ni kuchosha akili tu
Raha ya ghorofa mgeni anakaa sebule moja chini huko wewe unapata chai sebule ya juu, hata kama anakudai anaweza kuondoka bila kukuona hata wezi wakikuvamia watahangaika kujua unalala wapi
 
Habari wakuu,

Mungu akipenda, mwakani natamani kuanza ujenzi wa nyumba ya ghorofa moja. Mpaka sasa, nimefanya michoro yote, architectural na structural designs.

Naomba ushauri kwa watu wenye uzoefu, nataka kutafuta fundi Juma ambaye ana uzoefu kujenga ghorofa, anisaidie kujenga ili kupunguza gharama. Nataka kujua kama kuna mtu hapa ameshawahi kujenga kwa kutumia fundi wa kawaida.

Pili, naomba msaada kuju makisio bila finishing kwa nyumba ya 98sqm.

Asante kwa muda wenu.
Mtafute fundi Michael anauzoefu zaidi
 
Raha ya ghorofa mgeni anakaa sebule moja chini huko wewe unapata chai sebule ya juu, hata kama anakudai anaweza kuondoka bila kukuona hata wezi wakikuvamia watahangaika kujua unalala wapi
Ghorofa zuri kwa wenye pesa za uhakika sasa na huko mbeleni, kwa ambae hana pesa ya uhakika ghorofa ni mateso
 
Gharama yake??
 
Attachments

  • IMG_20240819_185620.JPG
    IMG_20240819_185620.JPG
    136.1 KB · Views: 24
Back
Top Bottom