Ushauri: Ndugu yangu hakubaliani na hali ya mtoto wake ilhali mtoto wake ashaikubali, pesa zinapotea na ni mwepesi kudanganyika, kipi kifanyike ?

Ushauri: Ndugu yangu hakubaliani na hali ya mtoto wake ilhali mtoto wake ashaikubali, pesa zinapotea na ni mwepesi kudanganyika, kipi kifanyike ?

Mkuu, hii kitu watu hawatokuelewa, kwamba unasikia honi, sauti za wanyama, ila unashindwa kuelewa maneno anayotamka mtu.

Nina sensorineural hearing loss ya masikio yote, plus Osteoma katika tundu la sikio la kushoto.

Nilisomea afya ya binadamu, siku nilivyopewa majibu ya usikivu, nilimwambia mzee mapema sana, hapa nitafute ishu nyingine tu ya kufanya, niachane na maswala ya afya.

Quinine ni ujinga sana, na cha ajabu ni kwamba bado kuna hospitali/vituo vya afya vya watu binafsi wanatoa.

Mwamba asikate tamaa, atafute ishu nyingine ya kufanya.
karibu huku mkuu

 
Mkuu pole sana ila hawa mama zetu wanatufanyia mengi sana mema ambayo hatuwezi kuyalipa. Tuzidi kuwaonesha upendo na kuwajali tuna mengi sana ya kushukuru Mungu kwa ajili ya hawa mama zetu kwa wanavyojali na kutuhangaikia hasa kwenye vipindi vigumu kimaisha. Ni kina mama wachache sana huwa hawajali watoto wao.
Ni kweli. Lakini na wamama waharibifu wala nyama za watoto nao wapo. Ukipata mama mwema ni wa kumshukuru Mungu na kumfanyia mema yasiyo mithilika mpaka kuingia kwake kaburini.
 
Mwache ahangaike nae tu...uchungu wake sio sawa na wako afterall pesa za kwao
 
Ukiwa na shida muombe Mungu atakujibu, asipokujibu jua kuna sehemu umekosea au hauna imani.
Kuwa tegemea wachungaji ni kosa kubwa,wale kazi yao ni kueneza injili ili kila mtu amjue Mungu,sasa wamejigeuza kuwa miungu
 
huyu ni mama mdogo wangu na nipo karibu sana na mtoto wake ambae huwa ananiambia vitu vingi.

Ni kwamba mtoto wa mama mdogo alipokuwa mdogo akiwa na umri wa miaka 9 aliumwa malaria, hali yake ilikuwa mbaya sana ikabidi apigwe sindano za quinine (kwinini)

Hii dawa kama mtakumbuka hapo zamani kwa waliowahi kutumia hii dawa ilikuwa inaziba masikio kwa kiasi flani lakini kesho yake yanarudi, ila kwa wengine hasa wale wanaochoma sindano edapo kipimo kikizidi hii kwinini ishafanya wawe viziwi kabisa ama kuwa na usikivu hafifu unaozidi kufifia kadri miaka inavyoenda.

ndicho kilichomkuta mtoto wa mama mdogo, akiwa na miaka 9 ndio alipigwa hizo sindano, alipofika darasa la saba tukaanza kuona hasikii fresh, na hapo ndipo napowaletea mkasa wangu.

ni tangu kipindi hicho hadi sasa kwa miaka takribani 10 mama mdogo kapitia mengi sana akiwa kama mama na hili nami naujua uchungu wa mama lakini imefika steji kwamba na mimi nmeamini wanawake ni rahisi sana kudanganyika.

Hopitalini huko alishaambiwa chanzo walimpa dawa lakini hazikumsaidia - Muhimbili, Kcmc, nairobi, india, Uingereza

yeye mtoto kashakubali hali yake, wana vikundi vyao vya wenye tatizo hilo na ana shughuli zake lakini shughuli ipo kwa mama yake.

Wachungaji feki

Mama mdogo akisikia tu kuna mchungaji mkubwa kaja mkoa anaoishi anaenda kwa wachungaji kuwapa hela hizi laki 2 hadi laki 5 kwajili ya kumuombea mtoto wake,, nilikuwa siamini haya mambo lakini hapo mwaka jana tu kuna mchungaji maarufu kabisa alikuja huo mkoa, kuna maombi maalum ya mtu moja moja ndani ya hema ni shilingi laki 4 kwa mtu moja.

Wachungaji baadhi yao wanafanya mazingaombwe ya wazi wazi nae mama mdogo anaamini kirahisi, kuna mmoja alienda nyumbani kwao huwa inasemekana anatembea na kemikali flani anachovyakwenye vidole, akianza kukuosha sehemu yoyote ya mwili maji yanabadilika rangi yanakuwa ya zambarau, yani hapa mama mdogo akili zilimruka akiamini ni uchawi unatoka, mme wake alipoona hivyo akardi chumbani kumwambia hayo mazingaombwe lakini wapi.

Mashehe wanaopandisha majini

Hapa ilibidi wasafiri kabisa kwenda huko Tanga, huyo shehe ni mshirikina anapandisha majini anaanza kumshirikisha Mungu kwenye tabibu zake, niliambiwa kila ikifika jioni kuna kufushwa dawa, hii ilikuwa kwa wiki nzima,

Waganga wa kienyeji:

Hapa palishafanyika hadi tambiko kkupigia magoti mizimu ilhali ni watu hao hao wanaenda nyumba za ibada

...............................................................

MUHIMU: Kijana kaniomba wazo la biashara, nipeni mawazo yenu >> hapa B]
Nna binam yangu naye alikumbwa na huu mkasa, tulihangaika sana hadi siku moja tuko msibani mzee mmoja aliomba aimbe wimbo na hitaa lake, katika kusalimiana akagindua dogo hasikii, akauliza alizaliwa hivi tukampa mkasa wote. Next week alikuja na majani flani akayafinyanga na mate kiganjani akamkamulia akarudia wiki km 3 dogo mzima hadi leo. Ila mdingi ndo alifariki mwaka jana
 
Mkuu, hii kitu watu hawatokuelewa, kwamba unasikia honi, sauti za wanyama, ila unashindwa kuelewa maneno anayotamka mtu.

Nina sensorineural hearing loss ya masikio yote, plus Osteoma katika tundu la sikio la kushoto.

Nilisomea afya ya binadamu, siku nilivyopewa majibu ya usikivu, nilimwambia mzee mapema sana, hapa nitafute ishu nyingine tu ya kufanya, niachane na maswala ya afya.

Quinine ni ujinga sana, na cha ajabu ni kwamba bado kuna hospitali/vituo vya afya vya watu binafsi wanatoa.

Mwamba asikate tamaa, atafute ishu nyingine ya kufanya.
Pole sana mkuu.

Sent from my SM-N916S using JamiiForums mobile app
 
Kuna kupigwa tena hapo kuwa makini, waleta ushuhuda wa kupona washaanza.
 
Me nilicho gundua una wivu na pesa za mamako mdogo... Usimpangie mtu matumiz ya pesa zake... Halafu hakuna kitu kinauma kama kuona mwanao anapitia changamoto fulani lazima upambane kwa gharama yoyote ile kumsaidia mtoto... Kama una mtoto utanielewa kama huna endelea kuona maza mdogo anahangaika bure...
 
Ninacho kiona hapo ni hustle za mama kwa mwanae! Acha aendelee kumpambania mwanae.
 
Back
Top Bottom