Ushauri: Nichague ipi kati ya BMW X3 2013 au Subaru Forester 2013


Hili la kuangalia mtaani sikubaliani nalo kabisa….maana kusema ukweli sisi wabongo tunaigana sana….watu tuna nunua magari kwa kuiga tu na si kingine….ndio maana subaru xt nyingi mtaani,harrier,vangard nk kwa kuwa tunaiga iga na waoga wa maisha.
 
Kuna gari zimeanza kuingia sasa hivi zinaitwa Mitsubishi RVR na kuna nyingine inaitwa subaru impreza G4..Hiyo Subaru ni fuel economy vipi kwenye upande mwingine kama vile performance na reliability?
 

Chukua any of them ila zitokee Japan. If you can afford maintenance schedules za BMW chukua tuu. Gharama za genuine parts for both cars ziko similar
 
Aiseee bora hata ww hizo zilikuwa zinakaa baada ya muda ndio inakudai.

Kuna spea za kichina ukifunga kwenye BMW zitakachokufanyia utaona afadhali ile mbovu ambayo umetoa.

Kuna X3 ya N52 tulibadili Crankshaft position sensor. Kwenye hiyo engine hiyo sensor ipo chini starter motor. Ili uifikie lazima intake manfold litoke.

Kufunga ya kichina kwanza connector hata haishiki vizuri. Zile kashkashi za kurudishia intake manfold kuna muda connector inachomoka.

Kuja kuwasha loh, chuma unaweza ukatekenya hata sekunde 10 au 15 ndio ikawaka. Mbona tulirudisha hiyo sensor.
 
…kama ukiwahi kutoa dpf na kufanya dpf delete kabla haijaua cylinder head gasket na turbo. Na si comfortable sana kama hizo nyingine. Haya ni mapungufu yake
Nitakutafuta unipe somo la Sky Active 2.2L D ya hawa jamaa.

Nawatamani ila nasikia DFP ni kichomi kwa izo Diesel.
 
Ila nimegundua za petrol bei yake imechangamka kidogo kuliko za diesel, hv hyo automation hapa bongo inafanyika au ni mpaka huko mambele

Kuna jamaa anaitwa KANYEGELO anasema ashawahi kufanya hiyo dpf delete hapa bongo ila kuiondoa physically anaweza fanya fundi wengi tu. Ila ukiondoa ni lazima uiprogram kuidanganya kuwa dpf ipo bado au inafanya kazi vizuri.
 
3.0 consumption ni kubwa (petrol) pengine ni bora hata x5 zile za 2007-2009.
Naziona nyingi hizi 2.0, kama hutojali tatizo lake ni nini hasa?
 
watu wangejua utamu wa Subaru, wasingekua wanajiuliza... Subaru yoyote ichukue tu
Subaru nzuri ila pia ina "personality" zake😆🤣 vijana walioanza kuwa nazo "machekibobu" au "subaru boys" wenye tabia zao basi hufanya kila muendesha subaru kuonekana wa hivyo.
Yote kwa yote jinsi wanavyozikimbiza zinaonekana ni gari poa.
 
Ushauri mzuri sana BMW zinasumbua sana vichwa kwetu Africa, huwa naona afadhali Volkswagen na Audi.
 
Sahihi Mkuu nimekuwa nikiwaambia wanunuzi wengi bora kuchukua Volkswagen au Audi mifumo yake sio complex kama BMW na Mercedes.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi, kikubwa baada ya kutumia toyoda kwa muda na kusikia wadau wa bmw wanavyozisifia nikawaza sihaba kujaribu hizi brand nyingine.

Haswa ni kuwa na reliable, economical (kiasi) lakini pia gari zuri.

Vw tiguan/toureg pia sijui umahiri wake ukilinganisha na bmw x3.
 

Reliability kwenye BMW inawezekana ila kama utaipa gari pesa nzuri.

X3 ni economical ukilinganisha na fuel economy huko ndo nyumbani. Huwezi nafanisha na gari ya kijapani yenye specs sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…