Ushauri: Niendelee kubaki Private institution au niende nikafanye kazi ya mtu binafsi

Ushauri: Niendelee kubaki Private institution au niende nikafanye kazi ya mtu binafsi

oooza

Member
Joined
Sep 12, 2024
Posts
5
Reaction score
4
Habarini wana jamvi.

Kutokana na vijana wengi waliopata nafasi za kuajiriwa kwa mikataba ya muda maalum katika mashirika binafsi hujikuta kuendelea kuomba nafasi sehemu zingine huku wakiwa bado wapo katika mikataba yao ya awali.

Binafsi nimejikuta nimesomea fani ya Ujenzi nikiwa chuo as a professional na nimebahatika mwaka jana kua registered katika fani yangu jambo lililonifanya kuja kuomba ushauri hapa ni kutokana kua na chaguo la pili ambalo ni geni katika kufanya comparison na hili nililokua nalo sasa hivi. Machaguo yenyewe ni haya:-

(1) Kuendelea sehemu niliyopo (Private sector) ambayo mkataba wake ni wa miaka miwili miwili lakini inakua renewable mpaka sasa nimerenew mara 1. Au

(2) Kwenda kufanya kazi ya Private Individual (tunaeza muita layman katika masuala ya ujenzi miradi mikubwa) anamradi wake wa ujenzi ambapo anahitaji msimamizi wa site kwa upande wake as a Project Manager na anatakiwa awe full time hapo.

Kilichonifanya kuja hapa ni kuomba ushauri katika risk factors zinazohusiana na option ya pili na nikienda kufanya nae negotiation nitilie mkazo kwenye aspects zipi ili niweze kupunguza risk kimkataba na kimaslai. Ninachokihitaji ni ku calculate risk na sio kuavoid risk.

Natanguliza shukrani.
 
Pata kwanza pesa za kutake risk mkuu usijpe poteza vyote.

Na uzoefu muhimu
 
Salary zipoje ? Zinaelekeana ama ? Baki hapo pa kwanza
Nilivyo msikiliza nikikubali nitakuwa na power kubwa ya kucontrol site kimkataba.
Salary almost the same ila kutakuwa na bonuses mbalimbali tofauti na huku ambapo nilipo. Bonus zilizopo siyo rasmi ni zakutokana na ujanja wa porini.
 
Kama jamaa anafanya miradi ya Gavo.

Changamoto kubwa ni kucheleweshewa malipo na Gavo

Je, atakubali kukulipa wewe ingali hajalipwa na Gavo(amecheleweshewa)
 
Kuna mengi muhimu lazima upime ambayo wewe utaona ni faida kwako huku bado unabeba pesa yako

Ambayo hayatakupa mzigo unapotaka kufanya kazi

Ambayo hauna muda wa kupanfiwa kazi inaweza kukufata pia kama una mengine unafanya wewe binafsi kwamba utapata muda day time kufatilia

So pima pima pima..
 
Back
Top Bottom