Ushauri: Nimefungwa akili, natamani kutoka kimaisha

Twende kibiti tukalime ufuta na mihogo huko mimi nimenunua shamba juzi wanauza 100,000 -150000 kwa heka.
 
Pole sana Mkuu ila kwa ufupi ni tatizo LA kiuelewa unaweza kukamata mchawi kumbe siyo lakini kikubwa ni kuwa Na mpango mzuri Na usikubari kukaa Na hela mfukoni wala mipango ya kwamba nikipata hela kadhaa Ndo naanza rasmi huku ukiwekeza Pesa tambua ya kuwa Pesa huwa haikai wala kutunzika


Kikubwa ni kuamua Leo kama mpango wako ni kufungua mgahawa anza kuandaa vitu muhimu ,mahitaji Na vitu vyote vitakavyo takiwa kufungua vikiwa katika maandishi Na bei zake ikiwezekana Na muda maalum wakutimiza hilo lengo Lako

Sasa kitakachofuata hapo ni utekelezaji wa huo mpango kazi wako hatua kwa hatua kufuata lile lengo Lako uliloliandika kila unapopata hela nenda kanunue kitu mojawapo kati ya vile ,kila unapopata Pesa nenda kanunue kitu mojawapo kati ya ulivyoandika afu mwisho tafuta hela ya pango ukishalipia pango anza kufanya ya mgahawa kwa kuingiza mahitaji yote uliyonunua

Nimetoa mfano tu hapo lakini Fanya hivyo kwa kila lengo Lako ulilonalo usisubiri Pesa ikamilike Ndo uanze mradi utakesha sana hela haitunziki hata siku moja
 
Kweli wewe kufanikiwa bado saana, yaani uanze kulima na kufuga kuku huku biashara ikisubiri? Watu wanatoka kimeisha kupitia kulima na kufuga kuku, wakati wewe unaiona kama sio biashara,

Fursa umeiona lakini unashindwa kuitumia, nakushauri wekeza nguvu zako zoote kwenye kulima na kufuga, acha mawazo yakuona kama kufuga na kulima sio biashara ya maana.
 
Ukitaka kufanikiwa/kutoka katika maisha lazima uwe na tabia ya kufanya yafuatayo:
1)Usipende kufuata mfumo(social system),fanya kile ambacho wewe unaona ni sahihi na moyo wako umekipenda ila mradi usivunje sheria, kanuni na norms
2)Fanya zile kazi/shughuli ambazo ukifanya zinakupa rahaa na furahaa licha ya kupata na kipato juu
3)Unapotaka kufanya kazi/shughuli fulani usitangulize hela au faida mbele bali tanguliza kupata furahaa, utu,e.t.c
4)Kuwa jasiri wa kujaribu na ukishindwa usikate tamaa bali rudia tena na tena hadi uweze ila mradi kitu hicho unakipenda
5)Usipende kufanya biashara bali fanya ujasiriamali
6)Penda sana ku-take risk na rafiki yako mkuu awe risk
7)Kuwa na marafiki wenye mawazo ya kimapinduzi achana na marafiki wanaowaza kufungua duka, kuanzisha traditional farming e.t.c
8)Penda sana kufuatilia vipindi vya elimu ya dunia hii kwa njia mbalimbali kama vile kusoma vitabu, kusikiliza radio, kuangalia tv, kusoma magazeti, kusoma majaridi, kuperuzi internet
9)Fuatilia na kuwa na marafiki na watu waliofanikiwa
10)Jali sana mda
11)Ogopa na kimbia umbea
12)Usipende kusingizia kuwa huna mtaji, kumbuka mtaji wako mkubwa ni ubunifu wako wa namna ya kuweza kufanikisha jambo lako
13)Usipende kuona kuwa huna mda tena na mda umeshakutupa mkono.Kumbuka unaweza kufanya kitu hata kama una miaka mia ila mradi una uhai na akili inafanya kazi
14)Acha kuwa muoga wa kuanzisha na kufanya jambo
15)Amini ya kuwa mambo yote ambayo unaona watu wanafanya katika jamii bado hawajaweza kufanya vya kutosha na uamini kuwa wewe unaweza kufanya mapinduzi zaidi
16)Lazima ujue na kuamini kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya jinsia yako na kuweza kufanya na kufanikisha jambo fulani
17)Penda kushirikisha watu wenye mawazo ya kimapinduzi katika maisha yako ya kila siku
18)Changua kitu kimoja unachikipenda na kufa nacho hadi kifanikiwe badala ya kutangatanga mara leo hichi mara leo kile
19)Penda kufanya zile kazi/shughuli/jambo ambalo watu wengi hulikimbia na kuona halifai labda kwa sababu ni jambo gumu, au ni jambo lenye risk kubwa sababu shughuli kama hizo huwa na returns/faida kubwa
20)Heshimu na kuwapenda wanadamu wote
21)Jali afya yako
 
Owk,,,nmekuelewa,,,wazo lako limefanyiwa kazi na mbaya zaid na rafiki yako ambae ulimwamin akushauri labda na alikua na mtaji tayari,pole sana lakn mshukuru mungu maana amekufunulia tabia halis ya rafiki yako

Maadam umeshaingia ktk wazo la biashara nitakupa kanuni moja ambayo itakua msingi mkuu wa yote....

ILI USIKWAME POPOTE HAKIKISHA UNALENGA MAHITAJI YA WATU ZAID KULIKO UTAUZA NN ZAID...MAADAM UNA WAZO TAYARI HUO NI MTAJI WAKO TOSHA KULIKO HATA HELA ULIYONAYO.. HELA NI KUJURAHISISHIA TU MAMBO YAKO LAKIN SIO MSINGI NAMBA MOJA WA BIASHARA,WALA KIWANGO ULICHONACHO SIO KIDOGO JINSI UNAVYOFIKIRI,,,UNAWEZA KUA UNAFIKIRI MAKUBWA SANA NA KUONA HELA YAKO HAITOSHI LAKIN NJIA SAHIHI NI KUANZA NA HELA ULIYONAYO NA MAKUBWA YATAKUJA.

Jiamin,jisimamie imara,thubutu kujaribu,mshirikishe mungu na yote yatabaki historia kwako.....
Pole kama ushauri wangu una kichambo[emoji40] [emoji40] [emoji40] ila nmejaribu kuchomekea tu,,nitakupa tips matata za kibiashara jinsi wachangiaji watakavyokua wanaendelea kukupa mawazo na uzoefu wao... Naendelea kusikiliza mziki na sasa nasikikiza GANJA FARMER..ya marlone Usher [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwa jinsi ulivyojieleza hujafungwa kiakili hata kidogo ila kuna kitu na ni ugonjwa unaitwa taking self short na excursis

hii ni wewe mwenyewe kujidharau na kujiona huwezi fanya kitu fulani na excursis ni ile hali ya kuahirisha mambo yako kwa kujenga sababu zisizo na msingi
CHA KUKUSHAURI kama una uwezo wa kuishika million moja kuna biashara hizi

ila kwa wazo lako la kilimo nakushauri kwa kimanzichana bora ununue ardhi mwenyewe kule heka moja wanauza laki nne lakini kama huna chanzo makini nakushauri ukodi shamba hasa maeneo yenye maji ulime mboga mboga kama bamia au hoho
n.k huko Ruvu heka moja ni 50,000

cha zaidi nakushauri ingia kwenye ulimwengu wa kusoma vitabu ukuze ubongo wako katika kufikiri anza na The magic of thinking big written by DAVID SCHWARTZ
 
Ni huyu huyu miss natafuta au simu yake imevamiwa na house girl....


Amaaaa kweli Awamu hii no stone will be left unturned
 
sijaelewa mkuu
sijaelewa mkuu
okay,,let me water it down like this-

-the path to becoming rich or succesfull become easy once you get the process started.
It all starts at the beginning with small lifestyle changes.

You need to know where your money is going,take a good look at your INCOME,EXPENSE and SPENDING pattern.

Once you know your pattern,you can plan your spending,saving and INVESTING arround them to help you reach your goals.

Earn money,spend less than you earn,save,invest,REPEAT THE PROCESS,after that it is just a matter of time,even if it takes years.
THE PROCESS Really is that simple..
 
unaijua kampany yangu mkuu
Kuna mtu asiyeijuwa kampani yako wewe? Wewe si upo na kina Nifah,miss chaga,warumi na kilanja ni Hansemtanashati na wengineo nyote nawakutaga kwenye jukwaa lenu pendwa la cerebrities huko ni ubuyu tu unaliwa
 
asante mkuu
 
Mambo ni magumu sasa hivi. Biashara zenye afadhali ni law firms, accountants na za chakula. Uwe mwangalifu unapoamua kuwekeza pesa zako kwa sasa hivi. Tafuta biashara yenye investment ndogo lakini ambayo itaanza kulipa ndani ya miezi 2 au 3.

Kilimo ni kizuri lakini kina challenge zake, jiandae kupambana toka mbegu mpaka kuuza mazao.

All the best
 
mimi nauza vitenge java online na karibu kila siku nauza pea 5, au sita kila pea napata anzia 20000 alfu na kushuka haishuki 8000...
tigo pesa
umeme
vocha za aina zote tanzania hii
ving"amuzi
nimeajiriwa nauza karanga hapa ofisini
ni dalali yaani mtu akitaka line za uwakala namsakia na nakula vichwa
hapa job nikipata dili za kuuza kama efd machine na mashine zingine nakula commission 10%
haha

na kwasasa kule kitaa nataka nikauze
viazi kwa jumla na rejareja wale wamama wote wanaopika sambuza uswazi nawakamatia chini
sili kitimoto
lakini kuna mchaga mmoja kanipatia kasehemu tuuze kitimoto ntaanza jumamosi hahaha

ninampango wa kufungua bucha uchwara kitaa

yaani kwa kifupi mjini humu sitaki kulala njaa................
wala sioni aibu hehehe
 
Biashara ni changamoto. Unaweza jaribu mara ya kwanza ya pili nk ukashindwa huna sababu ya kukata tamaa jaribu tafuta hata watu wanaofanya biashara kama hiyo uulize wao wamefanyaje. Mashamba yapo hata huko mkuranga.
 
Miss twende tukalime mahindi moro' achana na dar kilimo cha kubahatisha ardh yote mchanga tupu.
 
Binafsi najua ili ufanye biashara inahitajika Nia,Mtaji na Udhibiti
Wengi hukwama kwenye nua.tunakuwa na nia ya kufanya biashara nyingi nyingi pasipo kuweka mkazo katika kitu kimoja kwanza.Ukiweka mkazo kwa kitu kimoja ni rahisi kukianza na kujiendeleza.Mitaji wengi ni rahisi kutafuta.Kuhusu usimamizi hii ni issue muhimu pia.usianze biashara bila kujua utaisimamia vipi na kwa control zipi.Haya ni mawazo yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…