Imwase
JF-Expert Member
- Jun 14, 2017
- 500
- 506
- Thread starter
- #181
Shukrani sana mkuu kwa elimu uliyonipa.Nitaufanyia kazi ushauri wako.Ushauri Wangu ni huu
Elewa umri aliyopo binti yako kitaalamu unaitwa adolescent kwa tafsiri nyepesi anahama kutoka utoto kwenda utu uzima kukiambatana na mabadiliko ya kimwili na kihisia…….Vitu vingine siwezi viweka wazi sana vinaweza tumiwa forum kwa manufaa ya sexual predator au ma-pedophilia (Watu wenye kuvutiwa kingono na watoto wadogo).
Katika umri huo kuna kuwa na udadisi sana wa kujitambua “Yeye ni nani” na lazima hawe na msimamizi au guider hadi atakapopita umri huo kufikia 20s.
Binti yako kwa sasa ana umri wa miaka 14 na haushi na mama yake lakini nilitaka kujua baada ya kutengana na mama yake mahusiano yenu au ugomvi wenu umewaathiri watoto kina namna gani? Je unawaruhusu kuonana na mama yao hasa hao wa kike? (Samahani si lengo la kuingilia familia yako) ila ningefurahi kujua to what extent there some impact to her.
Elewa kingine ingawa hujachelewa sana barehe hasa binti hao huanzia miaka 11 muhimu sana “BABA NDIYO MPENZI WA KWANZA WA BINTI YAKE” (simaanishi sexual contact HAPANA) Je umeitumia nafasi hiyo kwa namna gani?
Tangia akiwa mdogo. Pengine kinamsumbua bintiyo ni self-image yaani anaonekana vipi mbele za wenzake na yeye ni somebody mbele ya teens wenzake muhimu sana kama hakuipata hiyo taswira kutoka kwa Mwanaume wa Kwanza tangia anazaliwa (Baba YaKE) sasa pasipokujua yaani “libido” inampeleka kwa other man au teens wenzake.
Jitahidi sana kujenga mahusiano na mwalimu wakike shuleni anaposoma au ungemtumia mama yake kwa hilo hasa wa darasani kutakuwa na good monitoring ya bintiyo anapokuwa shuleni.
Halafu weka mazingira ya kuanza wajua rafiki zake mtaani na hata shuleni huwafahamu wao na wazazi wao na si vibaya na mahali wanapoishi. Hiyo ni mission muhimu kwa kila mzazi hata kama unabanwa na shughuli gani hao ni watoto wako si wa house girl au wapangaji wenzako
Jitahidi na ni nani wa kumpa Elimu kwa karibu sana na very serious kuhusu Reproductive health ni vizuri mama yake akachukua nafasi hiyo.
Makosa Makubwa wanayofanya wazazi wanadhania labda kwa kuwa mtoto anakula basi ndiyo kumlea hii chart fupi sana kuhusu malezi ya mtoto
Mwili: Chakula Mavazi na Malazi mazuri
Nafsi: Maneno Chanya na kumtia nguvu ya kujiamini wakati wote “yeye ni nani” na discipline ya maisha na adhabu juu ya matendo mabaya nb kuchapwa anapokosea hasa wakati hajafikia Barehe
Roho:Hamjue Muumba wake na awe committed anapokuwa na rafikize au mbali na wazazi basi Mungu Yupo na anamuona hata katika vile anavificha kwa siri….
(Ukali wa baba unamfanya mtoto afanyie maovu mbali ambapo baba hawezi kuona lakini hukimsaidia hawe na hofu ya Mungu mahali popote Mungu anamuona hatajitenga na maovu)
Sitaweza funguka kwa sana sababu kwa maelezo niliyoyaokota katika threads hii yamenipa maswali ya namna hiyo vingine nikiviweka sana public kama nilivyoomba radhi kuna hatari ya Sexual Predator na Pedophilia wakachukulia advantage kwa Maangamizi ya Binti zetu ambapo kwa sasa wakipata Mimba “NO MORE SCHOOL”
Again thank you sana sana
Najisikia fahari kuwa MTANZANIA