Ushauri: Nimemaliza chuo, nina mtaji wa 2M. Naweza kufanya biashara gani?

Kati ya mawazo yote matatu hamna wazo bora, yote yatakusumbua ukizingatia mtaji wako ulivyo, aina za biashara na eneo lenyewe ni Geita. Tafuta mawazo mengine achana na haya kabisa
 
Soma kwa makini hadi mwisho mambo kujenga hayo ni mawazo ambayo nayafakiria maybe for 6 years to come but kwa now kama nilivosema mwishoni nataka kufanya kibiashara kidogo kidogo cha kunikwamua kimaisha ili nisiwe tegemezi Tena home
Basi kama una exprience yoyote ya ushonaji nunua mashine mbili za ushonaji chukua flame ya biashara nunua vitenge na vitambaa tafta leseni ya biashara. Baada ya hapo nenda halmashauri kaombe fedha ya vijana na wanawake pale halmashauri ya mji utajisajiri kwenye mfumo wao muhimu uwe pia na akaunti benki mambo mengine yatafata mwezi wakumi na mbili utakuwa na mtaji mzuri wakuendeleza ulipoa anzia hikiwa ni pamoja na kupanua mtaji.
Ukiona hyo biashara uwezi kama kwenu mna eneo la kutosha nunua ngano mafuta sukari mafuta masufuria na vitu vingine vinavyo itajika kufungua kakiwanda kadogo kakuzugia kutengeneza mandazi yale makubwa ya miatatu na miambili. Tengeneza pack kwenye mifuko wape boda boda wawili wawe wanakusambazia. By the way nipo geita tunaweza kuongea zaidi tukionana ukikwama.
 
Nashukuru nitafanya research kwenye vitafunwa
 
Nakushauri utafute mtu mzoefu kwenye biashara ambayo unaiweza ungana nae hasa kama una ndugu au rafiki wa karibu piga nae kazi upate uzoefu ukishakuwa konki utajitegemea

Nina shuhuda nyingi za watu niliomaliza nao chuo wakaweka pesa kuja kuingia kwenye game zikakata na wasiweze kurudi tena au kukaza sometimes biashara bila kushikwa mkono kutoboa ni kazi sana

NB usiwekeze hela yote labda kama unahofu huwezi kuitunza kinamna yoyote ile
 
Ni naweza kuhifadhi kwa vile lengo langu tu ni kujitegemea kwa kipato atleast nikifika 25 years niwe tayari naweza kushika hela ya mwnyw Bila kuomba kwa mtegemezi unaelewa baadhi yetu sisi tulikwenda Chuo wala tukakomaa na kusoma tu Bila kufanya chochote ndo tunashtuka dakika za mwishoni
 
Basi ikiwezekana fanya ivo, chukua nusu ya hiyo pesa muombe ndugu yako au rafiki ako akushike mkono kwenye biashara anayoifanya(iwe unaipenda) hadi pale utakapojua chungu tamu za hiyo biashara ndio uweze kujitegemea

Hapa simaanishi lazima muwe mutual bali hata kwa kukupa muongozo na trips mbalimbali za biashara husika
 
kwa huo mtaji unaweza ukaanza biashara ya utengenezaji wa vyakula vya kuku kitaalamu( poultry feed manufacturing) , DSM wafugaji wa kuku ni wengi. Ukitengeneza chakula kizuri na bei ikiwa nzuri , utapata wateja. Tafuta flemu weka biashara. Unaweza ukaanza kutengeneza kg 500. Unachanganya na mkono kwa kutumia spade( koleo). Pia umaweza ukafanya biashara ya mafuta ya kupikia hasa alizeti. Unanunua mafuta dodoma unauza Dar. Kwenye kutengeneza vyakula vya kuku ninaweza kukusaidia poultry feed formula za broiler, layers na dual purpose chickens pia nikakupa elimu namna ya utengenezaji wa vyakula vya kuku kitaalamu( nutritional balanced poultry feed). Hivi vitu nitakupa bure kabisa bila gharama yoyote
 
Chukua 1m betia mechi moja ya uhakika huku 1m ikiwa hakiba
Team za uhakika
1,Madrid
2,man city
3,simba
4,AL maidishu
 
Nitayafanyia kazi
 
Fanya hivi... Fungua duka la nguo za kike na mikoba ya mtumba
(Wewe utakaa Dukani, halafu tafuta kijana mmoja ambaye hana aibu muajiri, yeye atakuwa anauza nguo za ofisini mnadani kwa bei ndogo... Maana najua wakazi wengi wa huko wanapenda nguo bei rahisi

Then mimi ntakuwa nakuagizia mitumba kwa Bei ya Dar (maana mbali na ww pia pia ninataka kufungua ofisi hapo Geita Katoro...mama na dada zangu wanaishi hapo)

Ntakuagizia mtumba grade A.... Na nguo za watoto zinatoka sana huko kwenu!! Biashara ikiwa nzuri huko, ntakuingiza uwe sehemu ya ofisi yetu kwahyo utapata mzigo kwa bei ndogo zaidi
(Kwa maelezo zaidi njoo Whatsapp 0692667472)

Note: ofisi yetu inataka kupanua wigo kwenye soko la mikoani🤝
 
asikudanganye mtu hiyo 2m nenda pale kitambaa cheupe utakutana na watu wenye madili ya maana ukikosa pale nenda sehemu yoyote ya starehe ila iwe kubwa hapo hutakosa mishe au mawazo ya kuja kuwa tajiriiiiiii....


ukikosa kabisa hiyo 2m kasaidie yatima Mungu atakubariki 🤣🤣🤣
 
Saso aseee wapo vizuri sana namayai yai uwa makubwa
 
Mkuu
Kwenda Tena? kitambaa😂Sina insurance ya Kure cover mtaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…