Ushauri: Nimepewa RB kwa kosa la kufanya fujo kanisani

Kwani mjomba wewe ndio mchungaji? Mbona unaonekana una uchungu sana?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hata mimi kila nikisoma comment zake nikawa nawaza hivyo hivyo. Atakuwa pia ni muumini kindaki ambae humwambii kitu, au ni mmona wa wachungaji
 
Mbona una hasira sana na mtoa mada?? Wewe ni mchungaji nini?? Umesoma vizuri kwamba aliambiwa maziwa yameisha na akatoa hela yakaenda nunuliwa watoto wakanywa lakini bado walikuwa wanalia??

Je ni mwanamke mwenye akili ambae anaacha watoto wa miezi 4 bila maziwa anajua yameisha yeye anakaa masaa 10 kuombea watu ni mama au ni katili??

Je unajua kwamba kwa watoto wadogo chini ya miezi 6 anatakiwa kunyonya ziwa la mama tuu labda kuwe na sababu iliyo nje ya uwezo kiafya?? ( sio sababu ya upuuzi kama ya mke wa mleta mada).

Mwisho kabisa unajua kwamba kwa mtoto mdogo hata we na miezi 7 kuendelea ( ameanza kunywa uji na maziwa ya kopo) hakuna mbadala utakaomaliza kiu yake ya maziwa ya mama yake zaidi ya kunyonya??

Hakuna mama mwenye akili timamu anayeacha watoto wachanga masaa 10+ yeye yupo kanisani, hata makazini kuna break za kunyonyesha pia.
 
Kwa hiyo kama lina usajili mahakama itarunga vifungu vipya vya sheria? Maana hilo unalosema wewe hata kifungu cha sheria hakipo, bunge halijatunga sheria unayoitaka wewe. Kama hujui usitishe watu, kwanza KUFANYA FUJO ni kosa dogo sana na linasikilizwa mahakama ya mwanzo, hata sio wilaya, na wapi ulisikia mahakama ya mwanzo imemfunga mtu mwaka mmoja?
 
Mchungaji wa mchongo we muhuni tu kama wahuni wengine
 
Kwa huu uandishi wako tu ushadhihilisha wewe ni hamnazo
 
Hakuna kosa la UJAMBAZI Tanzania. Wewe unaejua sheria niambie kosa hilo ni CRIME, CIVIL au MINER?
Kila kosa lina vithibitisho vyake ili likamilike kua kosa.
Mfano. WIZI. Ili kosa la wizi likamilike lazima kuwe na vitu 3 vifuatavyo-:
1) Kitu kiwe KINA HAMISHIKA.
2) Kitu kiwe KINA MMILIKI.
3) Kitu kiwe na THAMANI
Hivi kikikamilika ndio kosa linasimama, ndio maana kakuna kesi ya kuiba nyumba wa shamba. Sasa wewe unaambiwa kosa ni KUFANYA FUJO wewe unasema ujambazi. Una akili kweli?
 
Update ya mwisho: Kanisa limefungwa 😂 nitafurah kusikia hvyo sanaa, siyapend hayo makanisa mm bas tuh
 
kwa sisi tunaojua kusoma picha, hakuna chochote kilichotokea hapo, na huna hata uwezo kwenda south. ila umeleta hii mada ili kuponda makanisa ya kiroho kwasababu una chuki nayo na umeweka mkeo iwe kama ndio pambio la kufikisha ujumbe wako. wewe kama unachukia makanisa ya kilokole, ni wewe, Tanzania kuna uhuru wa kuabudu, na mkeo ana uhuru wa kuabudu. pamoja na kwamba, kama ingekuwa kweli, anatakiwa kuwa na hekima, na inategemeana anasali kanisa gani, kama ni hayo ya wauza mafuta, shauriana naye kwa upole na amani, ataelewa, ila kama ni walokole wale wa tangu siku zote, it is just a matter of time hata wewe utakuwa mlokole, inaweza kuwa kwa hiari yako au kwa lazima. kuna watu wengine huwa wanaokoka kwa hiari ila wengine wanaokoka kwa fimbo. kuna mmoja wa aina yako alikuwa anawachukia walokole sana, ila kuna siku dawa zote zilidunda, pesa alipukutisha, waganga alimaliza wote, akajikuta anamwambia wife wake "NAOMBA KANIITIA YULE MCHUNGAJI WAKO ANIOMBEE". baba yangu mzazi alikuwa mbishi na alikuwa hataki twende church, ila alikuja kuugua akaita mchungaji, nashukuru Mungu dakika zake za mwisho alimpokea Yesu, hiyo ndio furaha yangu manake nilikuwa nampenda sana. hata wewe kuna siku ipo utaokoka kwa fimbo na utakuja hapa kutoa ushuhuda. acha kiburi cha uzima.

kuhusiana na mchungaji huyo aliyekuja kuuliza kuna nini, inaonyesha hayo ni yale makanisa ya matapeli, mchungaji wa kilokole, kwa heshima ya yule mama (mkeo) na kulinda ushuhuda mbele ya waumini, wala asingekuja kwa namna hiyo, angekuomba tu kwamba naomba tukayamalize nje. na ni lazima anakufahamu vizuri sana na kanisa lote watakuwa wanakujua na wanajua mshirika mwezaoi yaani mkeo anaishi na mtu msumbufu. hivyo kama alikuja kwa namna hiyo basi ana mapungufu. na hata akiwa na mapungufu haiwafanyi wasiwe wameokoka (kama wapo kanisa sahihi).watakuombea na utaokoka tu. mark my words.
 
I'd yako nyingine ni @chapwa24 ?
South Africa ni kitu gani mzee? Unataka nikuwekee tickets za flights nilizoruka nazo US,Canada, Brazil,Russia?
Sibishani na mtu mwenye I'd mbili.
 
Kwa ujinga huu unaoufanya mtatuharibia ndoa zetu sana rudini nyuma mjitafakari visa hivi ni vingi sana hasa kwa makanisa ya mlipuko. Mnajazana ujinga tu na miujiza hamjielewi hata hivyo nawapongeza wachungaji wa taasisi imara. Mimi ni mhanga wa visa kama hivi hivi kwann hamna akili au kwa kuwa wanawake kudanganywa ni rahisi. Harafu makanisa haya wamejaa wanawake sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…