USHAURI: Nini cha kufanya kama mwenza wako alikuficha kuwa ana mtoto, Ukaja kujua baada ya miaka zaidi ya 10 baadaye?

Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Itakuwa alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha alikuwa kamchoka mkewe, na kaachana na huyo ataenda kumuoa mwanamke mwenye watoto 3 huku kaacha mke mwenye watoto wake 4, maajabu haya.
 
Thread 'Agundua mumewe ana mtoto wa nje baada ya ndoa'
Agundua mumewe ana mtoto wa nje baada ya ndoa

Nimeikuta hii
Thread nimegundua binadamu haswa mwanaume ni kiumbe MNAFIKI SANA.
Comments zinanichekesha sana

Eti leo mwanaume alificha mtoto alafu mke hataki kuelewa wanasema ana roho mbaya ila huku wanasema mme amwache mke kwasababu alificha mtoto. Stupid kabisa
Ni wabinafsi kwelikweli.
 
Itakuwa alikuwa anatafuta sababu ya kumuacha alikuwa kamchoka mkewe, na kaachana na huyo ataenda kumuoa mwanamke mwenye watoto 3 huku kaacha mke mwenye watoto wake 4, maajabu haya.
Fanya makosa yote; usivunje "trust" ya mtu. Imagine unaishi na mtu miaka 15 na amekuficha kabisa kuhusu mtoto wake; alikuwa na mpango wa kuficha hadi lini? Hivi huyo mwanaume ataendelea kumuamini mkewe kweli?
 
Umeanza mihemko isiyo na sababu.
Pili tusijadili mambo kimazoea ya kiswahili.

Mwanzo wa mahusiano una mambo mengi.

Kuna mwanamke mkianza mahusiano anakutaka uwe wazi kwake kama umewahi kuoa au kuzaa nje.

Kwa moyo mkunjufu unamweleza ukweli.

Naye anakwambia hajawahi kuolewa wala kuzaa, baada ya miska 15 ukagundua alizaa na alikuficha kwanini udimwache?

Mwanzoni ukiniambia hata una watoto wawili kwa uwazi huo mimi nitakuoa.

Napendezwa na mwanamke muwazi, makosa kila mtu hufanya.

Lakini kitendo cha kumficha binadamu aliyetoka kiunoni mwako, si unaweza kumficha mmeo jambo lingine kubwa?
Ongea uhalisia uache hasira
Utamuoa vipi wakati masingle momy wanatukanwa na kusimangwa kila kukicha.
 
Ila wanaume huwa mnanishangaza jambo moja. Nyinyi mnazaa na michepuko yenu ilhali mpo kwenye ndoa, wake zenu wanakuja kujua mkishakufa. Mbona hawa vimbi mashavu kama mnavyovimba nyinyi??? Wengine mnawaletea kabisa nyumbani, na wanawapokea maisha yanaenda. Sasa huyu wa zamani kabla ya ndoa mnaumia nini. Wanafki nyinyi muwe mnatunza energy mnayoyafanya yakirudi kwenu mvumilie
Nakwambia yaani mwañamke analaumiwa utazani kazaa akiwa kwenye ndoa, na hapo hapo huenda hata yeye ana mtoto wa nje, nayeye amwachie watoto wake 4 awake nao.
 
Shangaa na wewe, mijanaume ya Kiafrika hua ni mibinafsi sanaaa, hii habari ingekua ni mwanaume ndie kaleta mtoto na Mwanamke ndie kataka talaka ungeona vile wanamshambulia Mwanamke na kumuita majina yote ya ajabu,

Mambo ya mtu na mtoto wake wao wanaguswa na nini eti kwanini kanificha kwani aliwahi kuulizwa?
Ndiyo ungesikia wanawake wana roho mbaya, nasema naye amwachie watoto wake wote .
 
Umesema sahihi Mkuu, ndiyo maana inashauriwa usifanye maamuzi ukiwa katika hali ya Furaha sana ama Hasira kali.

Huwezi kuja kuvunja ndoa wakati mna watoto wa miaka 20 plus, wameshindwa hata kukaa chini na kuyajenga.

Mie ilishanitokea nika abort mission, kesi yangu ilikua tofauti kidogo na hii. Hata hivyo nafikiri kama hiyo Hali ingetokea Sasa hivi, huenda ningefanya maamuzi tofauti kabisa na niliyofanya wakati ule.

Kesi yangu ilikua hivi, nilikutana na dada tuliyesoma wote tukiwa na urafiki wa kawaida Hadi tunamaliza shule. Sikuwahi kuwa na mpenzi Wala Ile one night stand, ni full Jesus Boy.

Nikaja kukutana na huyu binti wakati huo tayari nipo kazini, of course tukajikuta tumeendeleza urafiki wa kawaida, shida ikaja mwenzangu akawa anatengeneza mazingira ya kwenda mbele zaidi ikiwezekana Hadi ndoa. Nikaona kama Wazo zuri, ila nikataka tujipe muda wa kufahamiana pia sikutaka jambo la " kimasihara" kabla ya ndoa.

Nikagundua alikua na mtoto japo yeye hakuwahi kuniambia. Kuna siku nokamweleza jambo la mtoto nilitaka atoe hofu awe huru na ajue kwamba mtoto haikua shida kwangu.

Nilimpenda sana yule mtoto na Hilo alilifueahia. Shida yangu nikataka kujua mazingira ya baba wa mtoto, nilitaka Hilo likae sawa Kwa sababu lazima tujue mtoto ataishi kwetu au Kwa baba yake.

Hapo Sasa ndio sarakasi zikaanza. Nikapewa taarifa zisizo sahihi, kwamba baada ya ujauzito mambo yalikua si shwari Kwa vile Binti alikua chuo na baada ya hapo hakikuendelea chochote kati Yao.

Sasa kumbe namie nafsi ikawa inakataa, ikabidi nitumie mbinu za mafunzo ya sungusungu ( local FBI training) in intelligence...
Hapo ndio kujua kwamba Hawa watu walikua wakiishi huko kama Mme na Mke na jamaa alikua anamsomesha, walikua nchi nyingine na Binti alikua amekuja nchini kusalimia jamaa na kusherehekea Sikukuu za mwisho wa mwaka.

Nilichokua sana Kwa hizo taarifa, mbaya zaidi jamaa tukawaziliana nae kiroho safi akasema huyu ni Mke wake akanitumia emails zenye taarifa na ushahidi mwingi tu kuthibitisha Masai yake. Wakati huo Binti na Mama yake wamekataa katakata kumtambua huyo jamaa.

Siku hiyo nimeomba tukutane restaurant Moja Mimi, kaka mtu, Binti na Mama yake baada ya chakula nilitoa zile emails, nikaziweka mezani, nikaenda kulipiza bills nikarudi kuwaaga ukimya ukiwa umetawala.

Hapo tayari wazee walishaenda kupeleka posa ilikua tupangiwe kwenda kutoa mahari.

Huo ndio ukawa mwisho wa hiyo project.
Ni jambo lilinivuruga sana, uzuri nilikua likizo vinginevyo ningeharibu kazi za watu.
 
Ni kweli alifanya kosa kubwa sn la kuficha ukweli,Ila kwa wa huyo mtoto wa nje na idadi ya hao watoto wa ndoa angesamehe tu maisha mengine yaendelee mtoto wa ujanani miaka 20 huyo si tegemezi Tena mkubwa wangeendelea kulea tu hao waliopo.
 
Nakwambia yaani mwañamke analaumiwa utazani kazaa akiwa kwenye ndoa, na hapo hapo huenda hata yeye ana mtoto wa nje, nayeye amwachie watoto wake 4 awake nao.

Wanaume tuna ubinafsi wa kupitiliza. Hata kama ametoka Kwa mchepuko, ikibainika mke kaleta mambo meusi meusi atafanya maamuzi mazito kana kwamba kisa lake ni dogo kuliko alilofanya Mke.
Na Jamii yetu watakua upande wa mwanaume.
 
Umeishi na mtu kwa miaka 15, mmezaa watoto 4, unakuja kumuacha kisa hakukwambia kua aliwahi kuzaa kabla!!?

Ukisikia kutafutiana sababu ndio huko sasa.
Shida sio kuzaa, shida ni kudanganywa kwa muda wote huo. Hata ningekua mimi hiyo ndoa ingekufa hata kama tungekuwa tumeishi 30 years

NDOA NI UTAPELI
 
Kuna Mwanaume mmoja naye alimficha Mke wake hivi hivi, mwisho wa siku yule Mwanamke akagundua alilia sana sana Mume na wakwe wakaomba msamaha yakaisha mpaka sasa hivi wako kwenye Ndoa yao wanaishi vizuri.
 
Mie ilishanitokea nika abort mission, kesi yangu ilikua tofauti kidogo na hii. Hata hivyo nafikiri kama hiyo Hali ingetokea Sasa hivi, huenda ningefanya maamuzi tofauti kabisa na niliyofanya wakati ule.

Kesi yangu ilikua hivi, nilikutana na dada tuliyesoma wote tukiwa na urafiki wa kawaida Hadi tunamaliza shule. Sikuwahi kuwa na mpenzi Wala Ile one night stand, ni full Jesus Boy.

Nikaja kukutana na huyu binti wakati huo tayari nipo kazini, of course tukajikuta tumeendeleza urafiki wa kawaida, shida ikaja mwenzangu akawa anatengeneza mazingira ya kwenda mbele zaidi ikiwezekana Hadi ndoa. Nikaona kama Wazo zuri, ila nikataka tujipe muda wa kufahamiana pia sikutaka jambo la " kimasihara" kabla ya ndoa.

Nikagundua alikua na mtoto japo yeye hakuwahi kuniambia. Kuna siku nokamweleza jambo la mtoto nilitaka atoe hofu awe huru na ajue kwamba mtoto haikua shida kwangu.

Nilimpenda sana yule mtoto na Hilo alilifueahia. Shida yangu nikataka kujua mazingira ya baba wa mtoto, nilitaka Hilo likae sawa Kwa sababu lazima tujue mtoto ataishi kwetu au Kwa baba yake.

Hapo Sasa ndio sarakasi zikaanza. Nikapewa taarifa zisizo sahihi, kwamba baada ya ujauzito mambo yalikua si shwari Kwa vile Binti alikua chuo na baada ya hapo hakikuendelea chochote kati Yao.

Sasa kumbe namie nafsi ikawa inakataa, ikabidi nitumie mbinu za mafunzo ya sungusungu ( local FBI training) in intelligence...
Hapo ndio kujua kwamba Hawa watu walikua wakiishi huko kama Mme na Mke na jamaa alikua anamsomesha, walikua nchi nyingine na Binti alikua amekuja nchini kusalimia jamaa na kusherehekea Sikukuu za mwisho wa mwaka.

Nilichokua sana Kwa hizo taarifa, mbaya zaidi jamaa tukawaziliana nae kiroho safi akasema huyu ni Mke wake akanitumia emails zenye taarifa na ushahidi mwingi tu kuthibitisha Masai yake. Wakati huo Binti na Mama yake wamekataa katakata kumtambua huyo jamaa.

Siku hiyo nimeomba tukutane restaurant Moja Mimi, kaka mtu, Binti na Mama yake baada ya chakula nilitoa zile emails, nikaziweka mezani, nikaenda kulipiza bills nikarudi kuwaaga ukimya ukiwa umetawala.

Hapo tayari wazee walishaenda kupeleka posa ilikua tupangiwe kwenda kutoa mahari.

Huo ndio ukawa mwisho wa hiyo project.
Ni jambo lilinivuruga sana, uzuri nilikua likizo vinginevyo ningeharibu kazi za watu.
Pole sana Mkuu.

Ndiyo maana maandiko yanasema Ukiijua kweli nayo kweli itakuweka Huru.

Haijalishi utajisikiaje, ila ni vyema kusema ukweli japo kuna wengine huwa hawapendi kuambiwa Ukweli.

Kuna ndoa fulani, Mume akataka kujua Idadi ya wapenzi aliowahi Mke wake kuwa nao kabla yake.

Mke akasema vyema aanze Mume kutaja idadi ya wapenzi wake kwanza, Mume aka hesabu akapata Idadi ya Wapenzi 12

Ikafika Zamu ya Mke kutaja idadi ya Wapenzi wake aliowahi kudate nao.

Mke baada ya kuhesabu akapata Wanaume 102 waliwahi kumdate.

Ndoa yao iliishia pale pale
 
Wanaume tuna ubinafsi wa kupitiliza. Hata kama ametoka Kwa mchepuko, ikibainika mke kaleta mambo meusi meusi atafanya maamuzi mazito kana kwamba kisa lake ni dogo kuliko alilofanya Mke.
Na Jamii yetu watakua upande wa mwanaume.
Hapo ataenda kuoa .mwanamke mwenye watoto
 
Usikute baadae atajutafakari na kuona alifanya maamuzi ya haraka.

Mie nilishapewa muongozo kwamba, naweza kuleta hata Kijiji kizima Cha watoto waliopatikana awali kabla hatujawa pamoja, lakini taarifa yoyote ya mtoto au ujauzito uliopatikana tukiwa wote hapo hakuna mjadala ndio itakua tumefikia tamati.

Mambo ya mahusiano magumu sana.
 
Hata mimi siwezi, wakaoane huko huko na siwezi lea kabisa na hilo nalisemaga wazi tu
 
Back
Top Bottom