Lazima kuwe na sababu ya yeye kutokusema,
Kuna Mama alipokonywa mtoto na Mwanaume aliyezaa nae, mtoto alikua ana miezi 11, yule Mama alihangaika kuanzia Ustawi wa jamii hadi Mahakamani, kote aligonga mwamba basi akamuachia Mungu na kurudi kwao (Mikoa ilikua tofauti) baada ya miaka kupita, akaja akapata Mwanaume akamuoa hakumwambia kuhusu tukio lile yeye anasema alijaribu kulisahau hakuona sababu ya kulizungumzia tena, Mtoto alikuja kumtafuta Mama yake ameshakua mtu mzima na wajukuu akamletea, Mume ndio kujua hilo sakata lakini hakureact tofauti zaidi ya furaha familia imeungana tena.