Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Wakuu salaam,

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama fulani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada za kuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.
Usiingilie ugomvi usiokuhusu,ww huyo ni mamaako,ila kwa babaako mi just mwanamke( angekuwa kijana kumwita demu/mpenzi etc)mamaako huo kwake ni wivu wa mapenzi ambao hata ww kama unampenzi unao,cha muhimu kama kijana wa kiume wa kiafrika mkumbushe mzee acheze salama kama ni kweli ila atunze heshima yke na ya familia kama hawezi basi aachane naye au atafute mwingine wa mbali

La mwambie unajua mama anajua issue hivi na hivi keahiyo zinamuumiza jitahidi kufanyia mbali au kutokumuonesha waziwazi, otherwise mamaako ana play victim game kama walivo wanawake wengi kuwashirikisha watoto matatizo ya ndani ili aonewe huruma,ila suala la michepuko kwa wanaume wa kiafrika ni kawaida usiingilie ugomvi wa wapenzi hata kama ni wazazi wako!
 
Sawa
 
Sikushauri kuingilia swala hilo bro. Mambo ya Baba na mama sio ya kuamuliwa na watoto tena haswa ya kimahusiano. Mama yako atafute hata msimamizi wa ndoa yao au mchungaji aliewafungisha ndoa huyo ndio baba yako ataeza kuwaelewa. We utaenda kumfundisha nini baba ako akuelewe.
 
Huo mziki siyo level yako kijana! Achana nao kabisa usijepata laana!
Mwambie mama hiyo kesi aimalize mwenyewe. Kwanza mama yako hana adabu hakupaswa kukwambia mtoto wake mambo hayo...MAMBO YA WAKUBWA WAACHIE WAKUBWA!
 
Huo ujasiri wa kumuuliza baba utumie kumuuliza mama anakwama wapi mpaka kazidiwa nahuyo mchepuko wa dingi
 
Asante mkuu.Hiki kikao Cha ukoo unashauri sisi Kama watoto au tuwaachie wazee? Kukufahamisha tu nikwamba ndugu waupande wa mzee wamefanya kila wanaloweza ndo ikabidi bimkubwa anishirikishe
Huyo mchepuko anampa nini mzee wako hadi hajitambui?
Ushauri wangu: Tafuta baharia moja ulipe mpunga safi likamtongoze huyo mchepuko halafu muweke mtego wa kufumania mpige picha za kutosha umpelekee babako. Kwa kawaida wazee wakichapiwa michepuko huwa wanabwaga manyanga immediately. Mchezo utaishia hapo.
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ukijua sababu why baba mkubwa wako anamtetea mkewe na hasemi kitu utajua uanzie wapi kuna kitu hukijui .
Kuna uwezekano wanasaidiana kindugu!!! Chunguza vizuri.
Yawezekana:
  1. mtoa mada na nduguze wametokana na mchango wa baba mkubwa. Baba yao alivyogundua akaamua naye ale shemejiye. Baba mkubwa anakosa guts za kulalamika kwakuwa naye kazalisha huko kwa nduguye. Na ili kuzima soo, akiambiwa shida hiyo anamtetea mkewe ili kupunguza makali ya aibu.
  2. Mdogo mtu ndiye mzalishaji wa familia ya kaka yake, na kaka yake analijua hilo. Lakini akiulizwa anamtetea mke wake ili kuficha aibu
  3. Baba wa mtoa mada anayajua maovu ya mkewe, lakini ameamua kunyamaza ili kumsitiri mkewe na kuepusha kuvunja familia. Mama anatafuta sympathy kwa watoto kwa njia ya kufichua makosa ya mumewe, ili watoto wamwone baba yao kuwa ni mtu mbaya. Pengine watoto wakijiongeza wakachunguza upande wa pili watayajua hayo mama yao aliyomtenda baba yao hadi akaenda kuliwazwa na shemeji yake. Kuna shemeji wengine ni wana huruma sana, unaweza kumsimulia shida yako akakuhurumia hadi akaamua kukusaidia kabisa kabisa.
 
Asante mkuu. Pia mshauri kijana sepema kuwa kuna methali isemayo "hujafa hujaumbika". Yeye ni wa kiume na ameoa. Habari hii ya baba yake itakuja kutokea pia kwenye ndoa yake, mkewe atawaaminisha watoto kuwa sepema ana ubaya kadha wa kadha (si lazima iwe uzinzi, lakini linaweza kuwa jambo fulani tena la kweli), na watoto watalipokea na kumchukia baba yao.
Chunga sana sepema , hao watoto wako unaowahangaikia leo, kuna siku itakuja mkeo atawapelekea mashitaka juu yako, na utakumbuka kuhusu shitaka hili alilokuletea mama yako kuhusu baba yako.
 
Ule utam huwa ni siri ya mtu kuna vya kuficha ila mapenzi na huyo anaemtetea mkewe mchunguzeni vizuri akili iko sawa atakashtuka manyoya haya hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…