Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

sepema mtafte mzee ongea nae kistaarabu...mwambie unajua anamchepuko ...

basi achepuke kwa akili asimkere bi mkubwa, kama vp bi mkubwa akipata tatizo lawama zitamwangukia yeye
Asante kwa Ushauri.Kila anaenishaur naona anamsaada mzuri.Changamoto ni wadau kutofautiana msimamo.Wengine wanashaur niongee na mzee huku wengine wakisema nisithubutu.
 
Huu ndo ushauri rafiki! Busara kwanza kabla ya hisia.
Mahusiano ni zaid ya kukaa pamoja under one roof!
Nitoe kisa cha kweli ataelewa.
Familia ya kihaya ya watoto 6 me na ke. Uzeeni baba na mama huko kijijini wakatengana tena bila kusalimiana kila mmoja kwake kwa miaka 5 hiv.. Watoto wote wako vizuri 4 wako ulaya na USA kwa mfumo uliozoeleka wa ndugu kupeana connection mashirika makubwa.
Watoto wanawasapoti wazazi kila mmoja kivyake.
Sasa wakakubaliana December moja wote wawe Tz wawarejeshe wazaz pamoja mana maisha yamekaa sawa pote isipokuwa hili linawauma. Waliamin kila kitu cha kulimaliza wanacho, elimu, busara, pesa, kujitambua, ushawishi, nguvu n.k.
Mzee akasema hataki kikao cha namna hiyo na hatak kumwona mama yao. Wakakomaa.
Akasema nyie ni wanangu hayawahusu. Wakakomaa. Wa kike na kiume.
Akasema sasa jpili mlete mama yenu hapa. Kikao ni familia tu.
Akasema kwa kihaya."Nyinainywe akanyima emana olula nekyekundo!" (Mama yenu alininyima k kwa makusud kwa muda mrefu)
Kwa mila za kihaya ilikuwa ni lugha ya kuwakomoa wajumbe wa kikao(watoto) kias kwamba walitafutana pa kupita! Maana hamuwez kujadili kwanini mama ulimnyima mzee k.
Kikao kiliisha bila sign out!
Hata yule major wa JWTZ ana kifua kama faru hakustahimili!
...SI KILA KITU KINAHITAJI INTERVENTION YAKO, MENGINE YOU JUST SIT BACK AND WATCH!
Huu ni mfano bora sana; mambo ya mahusiano hasa ya wazazi wako ni ya kuyakalia mbali sana.

Mimi binafsi baada ya kuona memnhi duniani; huwa siingilii wala kutoa ushauri kwa mahusiano ya mtu yoyote yule.

Kuna visa na ugomvi wa mambo ya ajabu sana kwenye mahusiano.
 
Huenda anafaidika na hela anazohongwa mkewe na baba wa huyo kijana.

Kuna wanaume kipato chao ni cha mashaka hivyo kumtegemea mkewe ilimradi wale.

Au Pia huenda huyo mwanamke amewaroga wote wawili mume wa ndoa na mchepuko wote atakuwa amewaweka ndani ya chupa wasifurukute.

Hapo kazi yake ni kubwa sana kumponya huyo Mwanaume bana wa Mleta mada.

Hata muongee naye vipi bila kutolewa ndani ya chupa alimowekwa kufungua akili yake hataweza kumuacha huyo Mwanaume abadan iwapo anampa pesa n.k.
Hili lakuhonga pia lipo mkuu.Unaambiwa kun wakat mzee anachota mchele,maharage,na unga anampa huyo mchepuko Yaani maza wangu kakasirishwa na mengi
 
Pole sana mkuu. Mimi nitakupa experience yangu nilichofanya. Nikipata taarifa kama hizi kuwa mzee ana mahusiano na mmama fulani na mahusiano yale yalianza kuathiri ustawi wa familia yetu. Baada ya kupata ushahidi usiotia shaka nikafanya ka urafiki wa kinafiki na yule mama.

Kuna siku nikapita kazini kwake muda ambao alikuwa anafunga kuelekea kwake. Kwa kuwa hakuwa na gari nikajipendekeza kumpa lifti nikidai nami naelekea maeneo ya kwake. Kwenye gari linikuwa na wana watatu ambao "wameshiba" kwelikweli.

Kuingia tu akawekwa mtu kati. Hapo ndipo nikamweleza A-Z na nikamwambia wana wangeweza kumfanya chochote wanasubiri amri yangu tu.

Bi mmama alilia sana na kuomba msahama kuwa hatarudia na akaahidi kumwacha mzee kwa namna yoyote. Baada ya msamaha wake nikamwambia nikisikia hiyo habari kuwa amemwambia mzee atakutana na jambo baya mno maana wale mwana wameshamfahamu na wanajua kazini kwake.

Hii mbinu ilisaidia sana kuokoa mahusino ya pale home maana bi mmama alimwacha mzee na ananiogopa mpaka kesho.
 
My hypothesis kwa hilo tukio

1. Mume wa huyo mama ana kisukari na uzee tayari so has got nothing to loose as far as mkwanja wa mshua wako una flow he doesn't bother to ask anything

2. Mshua wako na huyo mzee wote wamerogwa na huyo mmama
 
Wakuu salaam,

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama fulani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada za kuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.

Mara ya mwisho mama kajaribu kumweleza mume wa huyo mchepuko kila kitu ila cha ajabu mzee yule kaamua kumtetea mkewe kuwa hana hizo tabia na hawezi kutoka kimapenzi na mzee wangu.

Upo ushahidi wakutosha kuwa mzee anatoka na huyo mama. Baada ya kuvumilia kwa miaka mingi mama ameamua anipigie simu kunishirikisha jambo hilo. Amenambia ameamua kunishirikisha mimi kwani ni kijana wake mkubwa na kwa hali ilivyo anaweza kupoteza maisha kwa pressure hivyo niangalie nini naweza kufanya.

Nimefikiria kumchukua bimkubwa niishi nae ila nahofia familia itajigawa. Ndugu wa mzee wameongea lakini mzee habadiliki kabisa, ndio kwaanza anachochea makaa kwenye treni. Nimefikiria kumvaa baba nimweleze kuhusu hilo tatizo nakwamba aache mara moja ila nahofia reaction yake. Wakuu; huu msala na utatua vipi ili ninusuru hii ndoa ya wazee wangu ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 30 Sasa.

Mwisho: Ukihisi huwezi kuchangia naomba usome nakupita. Kama itakulazimu kuchangia kwa kutukana, naomba hayo matusi yaelekee kwangu ila sio kwa wazazi.

Wasalaam!
Hilo sio lako... Kaa kimya kwani umeshalipokea...Ukiona unahitaji kufanya kitu lipeleke kwa mzee wa heshima rafiki yake au ndugu yake mkubwa ndio afanyie kazi
 
Ungeanza kwa kumshauri mamako apunguze presha na akubali tu kwamba kuna 'Bi. Mdogo' kwenye ndoa yao. Kuzungumza na babako kuhusu michepuko yake au hata ndoa yake ni a big NO(kulingana na mila, tamaduni zetu, za Nyúba ya Múmbi).

Hilo sio jukumu lako ni la wazee wenzake, ambao unaweza ukawashawishi wajaribu kuzungumza naye tena. Ila kujihusisha moja kwa mmoja italeta madhara mengi zaidi. Maanake hata ukitumia busara ya hali juu, bado itakuwa ni kwamba mmeungana na mamako kumdhulumu mzee.
Maoni mujarabu....Mtoa mada asidhani katika miaka 30 ya ndoa hilo ndio jambo la kwanza kuwatokea wazazi wake....Yamepita mengi kwa hiyo hata hilo asidhani yeye anaweza kulibeba kwa busara zake...
 
Hili lakuhonga pia lipo mkuu.Unaambiwa kun wakat mzee anachota mchele,maharage,na unga anampa huyo mchepuko Yaani maza wangu kakasirishwa na mengi



Duuuh [emoji2357][emoji2297][emoji2296] jamani! [emoji24]

Fikiria inauma kiasi gani ?! Mama yako ana kila sababu ya kujisikia vibaya juu ya hayo mahusiano ya baba yako na huo mchepuko.

Hata Vijana wengine huwa wanachukua vyakula, mafuta ya kupikia , sukari , sabuni, n.k. nyumbani kwa wazazi wao kwenda kuhonga mademu na kuibia hela wazazi wao na wanachuo wenzao kwenda kuhonga mademu zao.

Wengine wanaibia wanachuo wenzao hadi laptops wakauze wahonge mademu.

Inauma sana Yani mama yako namuelewa tu.
 
Mbinu ya kutumia ni kumpa pongezi baba yako na kumpa big up nyingi kwamba ameopoa pisi kali, baba atafurahi sana. Usiwe fala..ukifanya hivyo utakua kipenzi cha baba.
 
My hypothesis kwa hilo tukio

1. Mume wa huyo mama ana kisukari na uzee tayari so has got nothing to loose as far as mkwanja wa mshua wako una flow he doesn't bother to ask anything

2. Mshua wako na huyo mzee wote wamerogwa na huyo mmama
Hii namba2 namimi nimehisi hvy.
Namba1 Sina uhakika na afya ya yule mzee kwamb anasukari au la.Hilo la mchepuko kupewa mkwanja namzee wangu silipingi.
 
Pole sana mkuu. Mimi nitakupa experience yangu nilichofanya. Nikipata taarifa kama hizi kuwa mzee ana mahusiano na mmama fulani na mahusiano yale yalianza kuathiri ustawi wa familia yetu. Baada ya kupata ushahidi usiotia shaka nikafanya ka urafiki wa kinafiki na yule mama. Kuna siku nikapita kazini kwake muda ambao alikuwa anafunga kuelekea kwake. Kwa kuwa hakuwa na gari nikajipendekeza kumpa lifti nikidai nami naelekea maeneo ya kwake. Kwenye gari linikuwa na wana watatu ambao "wameshiba" kwelikweli.

Kuingia tu akawekwa mtu kati. Hapo ndipo nikamweleza A-Z na nikamwambia wana wangeweza kumfanya chochote wanasubiri amri yangu tu.
Bi mmama alilia sana na kuomba msahama kuwa hatarudia na akaahidi kumwacha mzee kwa namna yoyote. Baada ya msamaha wake nikamwambia nikisikia hiyo habari kuwa amemwambia mzee atakutana na jambo baya mno maana wale mwana wameshamfahamu na wanajua kazini kwake.

Hii mbinu ilisaidia sana kuokoa mahusino ya pale home maana bi mmama alimwacha mzee na ananiogopa mpaka kesho.
Ulitumia umafia mzuri.
 
Mbinu ya kutumia ni kumpa pongezi baba yako na kumpa big up nyingi kwamba ameopoa pisi kali, baba atafurahi sana. Usiwe fala..ukifanya hivyo utakua kipenzi cha baba.
Vipi nikiwa kipenzi Cha baba alafu nikampoteza mama?
Unashauri nimwite baba kabisa ili nimpongeze kwa hilo?
Hata hvy nashukur kwa Ushauri wako.
 
Vipi nikiwa kipenzi Cha baba alafu nikampoteza mama?
Unashauri nimwite baba kabisa ili nimpongeze kwa hilo?
Hata hvy nashukur kwa Ushauri wako.
Baba yako kama ni mstaafu tayari muache ale mema mzee. Mwanaume hajaumbiwa mwanamke mmoja, hizi kanuni wameleta tu watawala wa dunia.
 
Ni ngumu mtu kuacha Tabia Kwa kusikiliza ushauri peke take,na umesema Mzee wako ameshauriwa na mkewe aache na amekuwa mgumu.....Kifupi ktk mahusiano anayeacha mwanamke,mwanaume haachi kirahisi km mwanake hajaamua ,hasa km utelezi anauoata kirahis kutoka Kwa huyo mchepuko

Ushauri wangu; Mfate huyo mchepuko mke wa babaako mpige mkwara mzito Sana,km ile mkwara ya Baba ubaya wa kwenye gazeti, mshinikize aachane na babaako la sivyo utamfanyia kitu kibaya sn ambacho hajawai kufanyiwa kwenye maisha yake,alafu mchimbe mkwara mwingine kwamba asimwambie Mzee wako kuhusu wewe kmfata ukamoiga biti waachane,ajifanye Tu ameamua mwenyewe kubaki na mumewe njia kuu.

Nakupa mwezi hlutakuja kutoa ushuhuda hapa wameachana
Hahahahha hili biti la kitoto utampiga mwanamke mtu mzima ambaye ananufaika kifedha na hazina ya babaako 😂😂😂?

Kitachofuata siku ya mechi ijayo huyo mchepuko ataropoka yote na wote watakupuuza tu. Mzee atakuona boya kwa sababu lazma umeambiwa hio ishu na maza ako
 
mume kauanza mchepuko miaka mingi ukashindwa kudhibiti mwanao ndo ataweza! Tena wa kiume,, hebu usinichekeshe,

Msimamo wangu katika hali km hii kwwnye mahusiano huwa ni moja kati ya mawili, kupuuza kwa kutafuta suluhu na kusamehe,, ama kutosamehe na kufanya umafia kwa wabaya wangu,, ila kwa umri wa huyo maza nikiwa ndo mie ningempuuza mwanaume kwa kufanya mambo yangu km nilivyoandika toka mwanzoni,

Kuwaka, kufoka, kulia na kuumwa katika hili hakukusaidii kitu zaidi utapata kiharusi na ukifa hawaachani
Tena ukifa ndo anahamia kabisa pale home..!! Sasa sijui atafoka..!?
 
Sometimes tunaendekeza midomo sana,
Hapo naunga mkono hoja..!! Unajuwa huyo mtaka kumshauri babaake ana stori ya kwa mama yake tu..!! Hajui nini kimemfanya baba aamue hayo..!! Na kwa bahati mbaya, kwa jinsi wanaume tulivyo, AKIMUULIZA atazuga tu, wala hatasema chanzo halisi..!! Usikute mwamba kabaniwa unyumba miaka kadhaa, sasa jambo kama hili anaweza akamwambia mwanae?
 
Back
Top Bottom