Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

sepema mtafte mzee ongea nae kistaarabu...mwambie unajua anamchepuko ...

basi achepuke kwa akili asimkere bi mkubwa, kama vp bi mkubwa akipata tatizo lawama zitamwangukia yeye
 
mnaosema kuna kitu mzee kakosa kwa bi mkubwa ni upuuzi mtupu

mwanaume hata akiwa mzee kuchepuka ni kama jadi yao.... atachepuka tu

otherwise apate kisukari na presha mshedede ulale doro ndo atatulia

Kwa hivyo kama ni jadi yetu unamshauri mdau afanye nini labda.
Ni kweli kuchepuka ni suala mtambuka, kuna sababu nyingi tu, na inawezekana sio kosa la mke, mimi nimewahi kuchepuka na ukweli mke wangu hakua na kasoro yoyote na nilikua nampenda na bado nampenda, hili la kuchepuka sio rahisi kumzuia mwanaume, ni udhaifu tunaopambana nao kila siku, ila mara moja moja uzalendo hutushinda na kuachia.

Wanawake wa siku hizi kwa namna mnajiachia kwetu sisi wanaume, yaani wengi mnajitongozesha live bila siri tena, halafu kwa ambavyo mnapendeza, mavazi na mlivyo sexy yaani wanaume tunapata tabu sana, ukigeuza macho huku huyu kaachia maziwa nje nje yaani cleaverage, huyu mapaja kayabana yapo nje nje huyu hivi yule vile na vyote hivyo mnajua vinavyotuvutia kwenye hisia za ngono.

Bora mzee wa huyu mleta mada, yeye amechagua mchepuko mmoja akatulia kwake, kunao wanaruka ruka kwa wengi tu.
 
Pole sana ila usimchukue mama yako vaa moyo wa ujasiri muulize huyo mzee wako kuhusu hizo tuhuma usikie atajibu nini lakini ajabu huyo baba mkubwa wako nae hakubali kama anachapiwa ni jambo la ajabu maana ilibdi iwe kesi ya UKOOO hiyo... usikurupuke

Huenda anafaidika na hela anazohongwa mkewe na baba wa huyo kijana.

Kuna wanaume kipato chao ni cha mashaka hivyo kumtegemea mkewe ilimradi wale.

Au Pia huenda huyo mwanamke amewaroga wote wawili mume wa ndoa na mchepuko wote atakuwa amewaweka ndani ya chupa wasifurukute.

Hapo kazi yake ni kubwa sana kumponya huyo Mwanaume bana wa Mleta mada.

Hata muongee naye vipi bila kutolewa ndani ya chupa alimowekwa kufungua akili yake hataweza kumuacha huyo Mwanaume abadan iwapo anampa pesa n.k.
 
Mtafute huyo mwanamke anaechepuka na mzee wako, mpige mkwara wa kufa mtu na vitisho kibao na uhakikishe mnakua pekeenu ili asiwe na ushahidi wa kukushitaki popote. Muonyeshe kua uko serious ikiwezekana fanya hivo hivo kwa mume wake anaemtetea.
Baada ya muda leta hapa mrejesho.
 
Wakuu salaam,

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama fulani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada za kuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.

Mara ya mwisho mama kajaribu kumweleza mume wa huyo mchepuko kila kitu ila cha ajabu mzee yule kaamua kumtetea mkewe kuwa hana hizo tabia na hawezi kutoka kimapenzi na mzee wangu.

Upo ushahidi wakutosha kuwa mzee anatoka na huyo mama. Baada ya kuvumilia kwa miaka mingi mama ameamua anipigie simu kunishirikisha jambo hilo. Amenambia ameamua kunishirikisha mimi kwani ni kijana wake mkubwa na kwa hali ilivyo anaweza kupoteza maisha kwa pressure hivyo niangalie nini naweza kufanya.

Nimefikiria kumchukua bimkubwa niishi nae ila nahofia familia itajigawa. Ndugu wa mzee wameongea lakini mzee habadiliki kabisa, ndio kwaanza anachochea makaa kwenye treni. Nimefikiria kumvaa baba nimweleze kuhusu hilo tatizo nakwamba aache mara moja ila nahofia reaction yake. Wakuu; huu msala na utatua vipi ili ninusuru hii ndoa ya wazee wangu ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 30 Sasa.

Mwisho: Ukihisi huwezi kuchangia naomba usome nakupita. Kama itakulazimu kuchangia kwa kutukana, naomba hayo matusi yaelekee kwangu ila sio kwa wazazi.

Wasalaam!
Polee sana
Ingia kwenye maombi
 
Atakuwa naye ni mchepuko wa mume wa mtu mahala sio bure.

Kuna michepuko nimeshai note humu kupitia michango yao,

Eti mtu anathubutu kuandika michepuko inatunza ndoa ?!

Inashangaza sana
Unashangaa kwa vile wewe bado ni mtoto.....kua uyaone!

Ndani ya ndoa kuna mambo, wanaume tunavumilia mengi.
 
Kwani mama yako ndo mara ya Kwanza kuchepukiwa na baba yenu?

Sioni km ni busara kushtakia hii ishu kwako na km anakiri kuwa amekuwa mchepu wake kwa muda mrefu,,

Mi nikiwa na kijana mkubwa wa umri wako siwezi kuhangaika na michepuko ya mume kabisa, adhabu yake ni kuhamisha mapenzi, nguvu na akili nitawekeza ktk watoto wangu, wajukuu wakiwepo ama ndg wa familia nk,, home sitoki ila ndo nakuwa bize na malezi vizuri na akirudi zile za kubeep akuu namtizama tu, chumba chake atakikuta,,

Hakikisha unamtunza mama yako vizuri hii wazee wengi huwanyong'onyeza na kama hajazaa kwa mchepuko baada ya muda atarudi tu,, mzee mpe heshima yake km kawa ila usijitoe kipesa kwake

Kirahisi hivyo?

Wewe umeolewa unaishi na mume
Au wewe ni mchepuko?

Unazijua athari na madhara yatokanayo na mume kuchepuka?

Yani rasilimali za familia ( fedha, muda,
Zipotelee kwa mchepuko mazima wewe utachukulia poa?

risks za kiafya, ulozi , mafarakano n.k )

Na ukute wewe hela yako itumike kwenye maendeleo ya pamoja lakini hela zake yeye ziishie kuweka michepuko mjini na kuwa je Gea nyumba wewe utafurahi?!

Eti mimi niangalie watoto tu ? Kwani huo ndio ulikuwa msingi wa agano la ndoa ?
 
Mpaka kuchepuka nje, ina maana huko ndani kuna kitu anakikosa, au anapangiwa magoli.

Cha kufanya, kama una kipato; watoe 'out' baba na mama uwapeleke mbali, uwalishe na uwanyweshe vinywaji, huku ukiwaambia umuhimu wa umoja walionao.

Kisha walipie 'lodge' au hotel walale huko huko; wao wenyewe watamaliza kero zao.

Sometimes tena mara nyingi hamna lolote zaidi ya tamaa tu
 
Sijaona tatizo hapo,unaweza kumbana mzee afu wewe kesho ukachepuka.

Wanawake wanatakiwa wakubali kuwa mwanaume hawez kuwa na mwanamke mmoja.

Na kitaalamu huwa wanasema mwanamke ikifikisha miaka 35+ hamu ya tendo inaanza kupungua,sasa kwanini mzee aanze kuhangaika kuomba tunda kwa mtu ambae labda hataki kutoa.

Kitu ambacho sitakagi kabisa kuwaingilia wazee wangu ni kwenye hayo mambo ya kufurahisha miili yao,mwacheni mzee amalizie uzee wake kwa furaha

Tafuta kujua zaidi uelewe, studies reports from that kuanzia umri huo ndipo kasi ya mwanamke kwenye mambo ya mapenzi huongezeka,

Tafuta kufahamu zaidi
 
Afu changamoto ya kumpiga huyu mchepuko mkwara nikwamba naye nimama mtu mzima, watoto wake tunaheshimiana Kama ndugu.Nahofia kuanzisha mgogor Kati yahizi familia mbili.
Pia rejea pale ambapo mume wa huyu mama anamtetea mkewe kuwa hafanyi hizo Mambo.
Kwa upande wangu,huenda nisiwe sahihi lkn kitendo cha mume wa huyo mama kukataa kuwa mkewe Hana Tabia hizo,napata picha kuwa huenda Mzee ana tatizo hivyo hawezi mridhisha mkewe,kwahiyo kuficha aibu mke asiende kuchapwa nje na kutangaza aibu yake huenda ni Bora akaliwa na ndugu yake WA karibu,unajua wazee WA zamani haya mambo kwao sio ishu,na kuna baadhi ya Mila wakiona mkeo hapati ujauzito,unatafutiwa Safari halafu huku nyuma ndugu yako anakuja kumla mkeo na kupata Mimba, safii Tu ndugu Kwa ndugu.

Pili nakubaliana na wachangiaji wenzangu baadhi Yao,wewe kama mtoto kuongea na Baba yako sio adabu,ni Bora ushirikishe watu wazima wenye hekima waongee na Baba yako, ebu jifikirie wewe binafsi uko ktk hiyo Hali hlf mwanao anakuambia hayo mambo je utachukuliaje?

Mwisho ikishindikana kabisa,mdanganye mama kuwa umeongea na Baba yako,amekusiliza Tu lkn hajasema chochote,hapo mama ataona umefanya ulichoweza na ataona uko upande wake.
 
Achana na mambo ya wazazi wewe.

Kivipi wakati mchuma janga hula na wakwao ?

Mama yake akiugua presha na kupoteza maisha hasara itakuwa ya nani kama sio ya Mleta mada na nduguze ?

Pesa anazomaliza huyo mzee kuhonga huo mchepuko unaonaje kama huyo mzee angezitumia kwa maendeleo ya familia yake ?

Je unajuaje huenda huyo mchepuko ndie anayeleta mafarakano na amani kutoweka ndani ya hiyo ndoa ?

Hilo ni jambo la kuchughulikiwa haraka kumuokoa huyo Mzee ili apone na akili yake imrejee ajitambue.
 
Ndugu,

Licha ya upendo mkubwa uliyonao kwa mama yako, nikushauri tu hili jambo ni la kuliendea kwa akili na sio mhemko.

Moja; huna mamlaka juu ya mahusiano ya baba yako na huyo mwanamke mwingine, kama ameshindwa kuwasikia na kusitisha mahusiano baada ya kusemwa na mkewe pamoja na ndugu zake, unadhani una nafasi kubwa sana ya kumshawishi huyo mzee?

Mbili; usianzishe chuki na baba yako kwa kuwa tu ana mahusiano nje ya ndoa na kwa namna moja yanamuumiza mama yako. Wewe ni mtoto wa kiume; endelea kutafuta suluhu bila kuharibu mahusiano yao.

Tatu; kamwe usithubutu kumuuliza mzee wako juu ya hayo mahusiano; endelea kutafuta suluhu bila kumuuliza huyo mzee. Hapa ni vyema ukatumia wazee wenzake na sio wewe mtoto aliyekuzaa mwenyewe.

Nne; fanya uchunguzi binafsi juu ya hilo jambo na sio kuamini moja kwa moja maneno ya mama yako; alisema mzee Kikwete ''za kuambiwa changanya na za kwako''

Mwisho ; japo si kwa umuhimu; yaone mahusiano ya baba na mama yako kama mahusiano ya watu binafsi; mapenzi yana mengi; kuna siku watakuja kupatana huku wakipeana huba zito na wewe utabaki unashangaa usijue namna ya kuwatazama.

Nimekueleza haya kutokana na uzoefu mbalimbali.

Uwe na siku njema.
Huu ndo ushauri rafiki! Busara kwanza kabla ya hisia.
Mahusiano ni zaid ya kukaa pamoja under one roof!
Nitoe kisa cha kweli ataelewa.
Familia ya kihaya ya watoto 6 me na ke. Uzeeni baba na mama huko kijijini wakatengana tena bila kusalimiana kila mmoja kwake kwa miaka 5 hiv.. Watoto wote wako vizuri 4 wako ulaya na USA kwa mfumo uliozoeleka wa ndugu kupeana connection mashirika makubwa.
Watoto wanawasapoti wazazi kila mmoja kivyake.
Sasa wakakubaliana December moja wote wawe Tz wawarejeshe wazaz pamoja mana maisha yamekaa sawa pote isipokuwa hili linawauma. Waliamin kila kitu cha kulimaliza wanacho, elimu, busara, pesa, kujitambua, ushawishi, nguvu n.k.
Mzee akasema hataki kikao cha namna hiyo na hatak kumwona mama yao. Wakakomaa.
Akasema nyie ni wanangu hayawahusu. Wakakomaa. Wa kike na kiume.
Akasema sasa jpili mlete mama yenu hapa. Kikao ni familia tu.
Akasema kwa kihaya."Nyinainywe akanyima emana olula nekyekundo!" (Mama yenu alininyima k kwa makusud kwa muda mrefu)
Kwa mila za kihaya ilikuwa ni lugha ya kuwakomoa wajumbe wa kikao(watoto) kias kwamba walitafutana pa kupita! Maana hamuwez kujadili kwanini mama ulimnyima mzee k.
Kikao kiliisha bila sign out!
Hata yule major wa JWTZ ana kifua kama faru hakustahimili!
...SI KILA KITU KINAHITAJI INTERVENTION YAKO, MENGINE YOU JUST SIT BACK AND WATCH!
 
Acha UNOKO,,,, Yajue ya kuzingatia..

Sababu ya Baba ako kuchepuka hata akikuambia huwezi fanya lolote,,, May be ananyimwa ishu za unyumba na Mke wake...

Ni bora ukafanya yako Mkuu,,,,, achana na wazee.... Na kwanza sio Nidhamu... Labda kama Baba anamfanyia Mama Violence(KUMPIGA) hapo sawa...

Otherwise YAJUE YA KUZINGATIA ILI UACHANE NA YASIYOKUHUSU
 
Kirahisi hivyo?

Wewe umeolewa unaishi na mume
Au wewe ni mchepuko?

Unazijua athari na madhara yatokanayo na mume kuchepuka?

Yani rasilimali za familia ( fedha, muda,
Zipotelee kwa mchepuko mazima wewe utachukulia poa?

risks za kiafya, ulozi , mafarakano n.k )

Na ukute wewe hela yako itumike kwenye maendeleo ya pamoja lakini hela zake yeye ziishie kuweka michepuko mjini na kuwa je Gea nyumba wewe utafurahi?!

Eti mimi niangalie watoto tu ? Kwani huo ndio ulikuwa msingi wa agano la ndoa ?
mume kauanza mchepuko miaka mingi ukashindwa kudhibiti mwanao ndo ataweza! Tena wa kiume,, hebu usinichekeshe,

Msimamo wangu katika hali km hii kwwnye mahusiano huwa ni moja kati ya mawili, kupuuza kwa kutafuta suluhu na kusamehe,, ama kutosamehe na kufanya umafia kwa wabaya wangu,, ila kwa umri wa huyo maza nikiwa ndo mie ningempuuza mwanaume kwa kufanya mambo yangu km nilivyoandika toka mwanzoni,

Kuwaka, kufoka, kulia na kuumwa katika hili hakukusaidii kitu zaidi utapata kiharusi na ukifa hawaachani
 
Wakuu salaam,

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama fulani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada za kuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.

Mara ya mwisho mama kajaribu kumweleza mume wa huyo mchepuko kila kitu ila cha ajabu mzee yule kaamua kumtetea mkewe kuwa hana hizo tabia na hawezi kutoka kimapenzi na mzee wangu.

Upo ushahidi wakutosha kuwa mzee anatoka na huyo mama. Baada ya kuvumilia kwa miaka mingi mama ameamua anipigie simu kunishirikisha jambo hilo. Amenambia ameamua kunishirikisha mimi kwani ni kijana wake mkubwa na kwa hali ilivyo anaweza kupoteza maisha kwa pressure hivyo niangalie nini naweza kufanya.

Nimefikiria kumchukua bimkubwa niishi nae ila nahofia familia itajigawa. Ndugu wa mzee wameongea lakini mzee habadiliki kabisa, ndio kwaanza anachochea makaa kwenye treni. Nimefikiria kumvaa baba nimweleze kuhusu hilo tatizo nakwamba aache mara moja ila nahofia reaction yake. Wakuu; huu msala na utatua vipi ili ninusuru hii ndoa ya wazee wangu ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 30 Sasa.

Mwisho: Ukihisi huwezi kuchangia naomba usome nakupita. Kama itakulazimu kuchangia kwa kutukana, naomba hayo matusi yaelekee kwangu ila sio kwa wazazi.

Wasalaam!
Very rare mtoto kumweka mtu kati mzazi wake... Inatafsiriwa kuwa ni dharau. Hata mama hakutakiwa kukushirikisha wewe. Na wamam wengi hufanya hivi lakini mwisho wake huwa si mzuri..!!

KAMA UNAWEZA MTAFUTE MTU MZIMA ZAIDI YA BABAAKO AU WENYE UMRI SAWA YEYE NDO AKAFANYE HILO UNALOTAKA KULIFANYA... !!! Wewe mwenyewe usithubutu kumkalisha chini babaako..!! Huwaga haina mwisho mwema
 
Mchukue mama yako uishi naye umuache huyo baba ahangaike kuchungulia maumbile ya kike atakavyo. Kama kwa umri huo huyo baba alipaswa kutulia na kuwatunzia heshima yenu maana si vyema watoto kusikia habari kama hizo kuhusu baba yao lakini hajafanya hivyo basi ujue ni tabia yake na hataacha. Leo mtamkanya mmoja kesho ataanza na mwingine.

Hii hali ilishanikuta kwa mama yangu nikaichukulia simple lakini sasa najuta maana depression na sonona ilichangia sana kifo cha mama.
Ushauri wangu kwa mleta mada asisimame upande wowote katika ili aweke akiba ya maneno, namna sahihi ya kuongea na mzee ajaribu kumwuliza mzee kwa kuanza kueleza ujio wa mamake, na aulize ikiwa kuna shida yoyote kati yao. Akishamsikiliza mzee ndo aone namna ya kushauri, kuliko hii kesi ya kuskiliza upande mmoja.

MWISHO SUALA LA MAHUSIANO KWA MAANA YA NDOA HUMALIZWA NA WANANDOA WENYEWE hakuna cha mjumbe, mtoto, shehe, Nabii, Askofu, Mchungaji wala hakimu.
 
Wakuu salaam,

Mara kadhaa mama amekuwa akimtuhumu mzee kujihusisha kimahusiano na mama fulani ambae ni shemeji yake. Mama amejaribu kufanya jitihada za kuwaachanisha kwa njia ya mazungumzo lakini wamegoma kuachana kabisa.

Mara ya mwisho mama kajaribu kumweleza mume wa huyo mchepuko kila kitu ila cha ajabu mzee yule kaamua kumtetea mkewe kuwa hana hizo tabia na hawezi kutoka kimapenzi na mzee wangu.

Upo ushahidi wakutosha kuwa mzee anatoka na huyo mama. Baada ya kuvumilia kwa miaka mingi mama ameamua anipigie simu kunishirikisha jambo hilo. Amenambia ameamua kunishirikisha mimi kwani ni kijana wake mkubwa na kwa hali ilivyo anaweza kupoteza maisha kwa pressure hivyo niangalie nini naweza kufanya.

Nimefikiria kumchukua bimkubwa niishi nae ila nahofia familia itajigawa. Ndugu wa mzee wameongea lakini mzee habadiliki kabisa, ndio kwaanza anachochea makaa kwenye treni. Nimefikiria kumvaa baba nimweleze kuhusu hilo tatizo nakwamba aache mara moja ila nahofia reaction yake. Wakuu; huu msala na utatua vipi ili ninusuru hii ndoa ya wazee wangu ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 30 Sasa.

Mwisho: Ukihisi huwezi kuchangia naomba usome nakupita. Kama itakulazimu kuchangia kwa kutukana, naomba hayo matusi yaelekee kwangu ila sio kwa wazazi.

Wasalaam!
Mimi nadahani umechukua maamuzi ya haraka ya kumchukua mamako, tafuta chanzo cha tatizo kwanza hapo ndo utapata kujua uhalisia wa hili jambo. Ndoa lazima ibebe amani na furaha, nyumba lazima iwe ni sehemu ya pumziko lakini endapo itageuka kuwa kero lazima mtu atatafuta suluhisho japo la muda mfupi. MWISHO SUALA LA MAHUSIANO KWA MAANA YA NDOA HUMALIZWA NA WANANDOA WENYEWE hakuna cha mjumbe, mtoto, shehe, Nabii, Askofu, Mchungaji wala hakimu.

Angalizo kwa kuwa wewe ni kijana wa kiume na umeoa pia, kumbuka asilimia kubwa ya wanawake wakifika umri fulani wanaona tena mwanaume si chochote bali watoto wake, na nadhani hii ni nature hata watoto tunapopata kazi tukajenga nyumba mara nyingi mzazi wa kwanza kututembelea ni mama na si baba. Lakini pia nakukumbusha hakuna mgogoro usiokuwa na sababu, tafuta sababu ya mgogoro na pia tambua kile anachokitafuta mamako kiko mikononi mwa Mungu na si wewe. Akubali kufuata hekima na ufahamu, atafute ni wapi arekebishe ili ndoa yake iwe na furaha. Kadili mnavolipanua hili mnazidi kuchochochea kuni,
 
Boy sikia, usikae na Baba yako.
Nenda kaa na mama yako, mwambie Baba Yuko kifungoni, aya anayoyatenda sio matakwa yake, kwahyo mtulizze Kwanza mama Kwa namna hiyo.

Kisha kaeni muone mnamsaidia vipi, kumbuka hapo anayetakiwa kubanwa na huyo mama yako wa nje aka mchepuko wa Baba yako. Acha kudili na Baba yako, ww dili na mama yako mzaz Kwa kumtuliza, alafu unganisheni nguvu mudili na huyo mama,

Mzingueni Kwa kutumia akili sio makelele, huo mchepuko utaona Baba yako ni mchungu mkifikia hiyo hatua mchepuko atamuacha Baba na hiyo ndio itakuwa salama yake.

Maana inavyoonekana mchepuko sio wa mchezo, nazan unaona hata mume wake Hana mashaka, maana ata huyo mume wa mchepuko Yuko kifungoni. Kwahyo mchepuko kawafunga kwenye penzi lake Baba yako na mume wake,

SIJUI UMENIELEWA???
Fanyia kazi hayo utakuja kunishukuru
Hii inaukweli mkuu.Nahis yule mama anatumia dawa kuwapumbaza Hawa wazee
 
Back
Top Bottom