Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Hata Mimi nilihisi hakupaswa kunambia.Ila ndohivyo kashanambia..likitokea baya atahisi sikufanya chochote kumsaidia.
[emoji54][emoji54]Usiogope hakuna baya lolote hapo kwa sasa!!
 
Tatizo umelijua sasa kesi kama hizi zinahitaji uwe na evidence yakujitosheleza may be kam picha ya mzee wako akiwa na uyo mmama wanaenda guest n.k
 
Mzee anatumia kilevi.Inaeza kuwa njia nzur Ila changamoto nipale atakapokubaliana namimi kwa kuongozwa na kilevi kichwani.Kesho au keshokutwa anaweza aendelee
Basi nikushauri hili swala liwekeni kikao cha ukoo jaribu kuzungumza na ndugu wengine ... mwekeni kitako mwelezeni kwa umri aliyo nao hapaswi kufanya ivo pia mama aeleze ukweli I awezekana sababu ya mzee kuchepuka kuna mambo amekosa .... yani valia njuga jumla jumla vaa ujasiri
 
Pole sana.

Cha muhimu pata taarifa kwa mtu mwingine, hao uliosema walimkalisha Mzee Kikao. Ili ujiridhishe kuwa ni kweli hili suala lipo. Na ujue lipo kwa ukubwa gani..

Baada ya hapo ndipo uone namna ya kumweleza Mzee wako, isiwe mazungumzo emotional bali umwambie kuna tetesi umezisikia Juu yake na huyo 'Mmama' na kwamba unahisi au unaona kuwa zinamuumiza Mamako..

Ikiwezekana; kiume mwambie, hata kama hayo mambo yapo basi ajitahidi isilete Madhara kwenu kama Familia maana litawaumiza hata ninyi wanawe. Naamini atakuelewa na atazingatia ushauri wako.

Usithubutu kutumia hasira, wala emotion kwenye mazungumzo yenu. Maana huwezi jua anapewa nini mpaka anawapuuza wote wanaomshauri..
 
Mwite mzee wako uongee naye kwa upole,heshima na upendo,mueleze madhara ya yeye kufanya vile.Ila ukifoka tu umeharibu.
Siyo rahisi Kama unavyoandika hapa.Mtu kuacha Tabia aliyoizoea msukumo unaanzia ndani yake.Maneno ya kuambiwa peke yake hayajawwhi kumfanya mtu aache Hilo jambo
Tena Mzee anaweza kuona anamvunjia adabu na wakaishia kugombana.Ampige mkwara mzito huyo mchepuko ndy solution.Wanawake Wana Tabia ya woga

Tena amwambie huyo mwanamke ''mamaangu akifa Kwa presha Kwa ajili yako nami nakuua''
 
Kesi za mapenzi haziwezi malizwa na vikao vya ukoo
 
Halafu unapoomba ushauri usimpangie mtu cha kuchangia vinginevyo jambo lako usingeleta humu.. tafadhali.
 
Mkubwa hapangiwi.. kama anaweza oa kama mke wa pili sio mbaya kuliko kuchepuka.. alasimishe kama itawezekana.
 
Ungeanza kwa kumshauri mamako apunguze presha na akubali tu kwamba kuna 'Bi. Mdogo' kwenye ndoa yao. Kuzungumza na babako kuhusu michepuko yake au hata ndoa yake ni a big NO(kulingana na mila, tamaduni zetu, za Nyúba ya Múmbi).

Hilo sio jukumu lako ni la wazee wenzake, ambao unaweza ukawashawishi wajaribu kuzungumza naye tena. Ila kujihusisha moja kwa mmoja italeta madhara mengi zaidi. Maanake hata ukitumia busara ya hali juu, bado itakuwa ni kwamba mmeungana na mamako kumdhulumu mzee.
 
pole sana ila usimchukue mama yako vaa moyo wa ujasiri muulize huyo mzee wako kuhusu hizo tuhuma usikie atajibu nini lakini ajabu huyo baba mkubwa wako nae hakubali kama anachapiwa ni jambo la ajabu maana ilibdi iwe kesi ya UKOOO hiyo... usikurupuke
Sio acha akamle kimasikhara
 
Mchukue mama yako uishi naye umuache huyo baba ahangaike kuchungulia maumbile ya kike atakavyo. Kama kwa umri huo huyo baba alipaswa kutulia na kuwatunzia heshima yenu maana si vyema watoto kusikia habari kama hizo kuhusu baba yao lakini hajafanya hivyo basi ujue ni tabia yake na hataacha. Leo mtamkanya mmoja kesho ataanza na mwingine.

Hii hali ilishanikuta kwa mama yangu nikaichukulia simple lakini sasa najuta maana depression na sonona ilichangia sana kifo cha mama.
 
Sepema pole sana ila haya mambo usikurupuke ni vigumu kujua ni nini mzee kakosa kwa mama yako lakini pia ina ugumu sana wewe kumueleza mzee hali halisi hata kwa heshima na adabu bado kwake ataiona dharau tu .Sasa ufanye nini ?

Ndugu mambo ya wazazi ni vigumu sana kutatuliwa na watoto hivyo fanya hivi mtafute mzee wako muombe kikao yeye mwenyewe pasipo kumshirikisha yeyote ila yeye tu .

Kaa na mzee wako sasa kama mwanaume mwenzio , mpe madhara ya kuchepuka huku mama yako akiwa anaona live na wanakijiji pia , hivyo katika hitimisho mueleze mzee wako ya kuwa ninyi wote ni wanaume na kuchepuka hakuepukiki kwa kiasi fulani ila sasa muombe abadili mfumo wa uchepukaji kutoka kuwa wazi kwa jamii inayomzunguka mpaka iwe ni siri ya yeye na mchepukaji mwenzie , baada ya hapo muombe na umshukie hata magoti chini ya kuwa akakiri kwa mkewe na kumueleza sasa kaachana na mchepuko na hatorudia tena hivyo yuko na yeye tu .

Kwa kufanya hivyo afya ya mama kimapenzi itahimarika mara dufu hivyo atapata tena hiyo presha ila ukweli wote unaujua wewe na baba yako .

Mwisho mkuu , ikiwa mama yako atajihisi kuwa mwenyewe kuna mabadiliko mzee atayaona kwa mama yako hivyo kama kwa mchepuko alitamani , nakuhakikishia si mda ataachana na mchepuko wake ili aendelee kumfaidi mama yako ila ikiwa basi ajaachana na mchepuko basi itakuwa alipapenda sana pia kwa mchepuko hivyo aiendeleze hiyo siri mpaka kifo.

Ushauri tu [emoji120][emoji120]

TEKERI
 
Kuna ndugu yangu wakike alijaribu kuongea nahuyo mama (mchepuko)na akamuonya kuwa akae mbali na mzee.Dadangu huyo alitumia lugha za vitisho ikabidi nimtulize kuwa asitumie maneno makali cz likienda kisheria anaweza awe matatani.Pa2 na mikwara hiyo bado tu hawajaachana
 
Hakuna cha kukosa, Mwanaume kuchepuka ni kama nature.
Huwezi shindana na Asili...
 
Acha kuingilia maisha ya wazazi wako!!
hizo ni shida zao sio zako EBOO!
ingilia kwenye maisha ya wazazi wako pale panapokuwa na shida za kiuchumi ama magonjwa ili usaidie lkn kuweka pua yako mbele mbele kwenye maswala kama haya huo ni ushuzi!
Hata baada ya mzazi mmoja kunishirikisha sipaswi kuingilia mkuu?
 
Tatizo umelijua sasa kesi kama hizi zinahitaji uwe na evidence yakujitosheleza may be kam picha ya mzee wako akiwa na uyo mmama wanaenda guest n.k
Ujue mwanzo mzee alibananishwa na maza akakubali kuwa nikweli na wakaombana msamaha yakaisha.Sas kumbe mzee hakuacha badala yake akawa tu amebadili mbinu kidogo.
So hapa sio kwamb inahitajika ushahidi mkuu,mzee alikubali mwenyewe.
 
Asante mkuu.Hiki kikao Cha ukoo unashauri sisi Kama watoto au tuwaachie wazee? Kukufahamisha tu nikwamba ndugu waupande wa mzee wamefanya kila wanaloweza ndo ikabidi bimkubwa anishirikishe
 
Pangeni fumanizi kwa mzee wako na huo mchepuko wake,yaani muwafumanie live na mangoma na matarumbeta,

Siku ya kwenda kuwafumania mchukueni na mume wa mchepuko wa mzee wako na Mother wako awepo na mjumbe wa mtaa awepo,huo ndio utakua mwisho wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…