sepema pole sana ila haya mambo usikurupuke ni vigumu kujua ni nini mzee kakosa kwa mama yako lakini pia ina ugumu sana wewe kumueleza mzee hali halisi hata kwa heshima na adabu bado kwake ataiona dharau tu .Sasa ufanye nini ?
Ndugu mambo ya wazazi ni vigumu sana kutatuliwa na watoto hivyo fanya hivi mtafute mzee wako muombe kikao yeye mwenyewe pasipo kumshirikisha yeyote ila yeye tu .
Kaa na mzee wako sasa kama mwanaume mwenzio , mpe madhara ya kuchepuka huku mama yako akiwa anaona live na wanakijiji pia , hivyo katika hitimisho mueleze mzee wako ya kuwa ninyi wote ni wanaume na kuchepuka hakuepukiki kwa kiasi fulani ila sasa muombe abadili mfumo wa uchepukaji kutoka kuwa wazi kwa jamii inayomzunguka mpaka iwe ni siri ya yeye na mchepukaji mwenzie , baada ya hapo muombe na umshukie hata magoti chini ya kuwa akakiri kwa mkewe na kumueleza sasa kaachana na mchepuko na hatorudia tena hivyo yuko na yeye tu .
Kwa kufanya hivyo afya ya mama kimapenzi itahimarika mara dufu hivyo atapata tena hiyo presha ila ukweli wote unaujua wewe na baba yako .
Mwisho mkuu , ikiwa mama yako atajihisi kuwa mwenyewe kuna mabadiliko mzee atayaona kwa mama yako hivyo kama kwa mchepuko alitamani , nakuhakikishia si mda ataachana na mchepuko wake ili aendelee kumfaidi mama yako ila ikiwa basi ajaachana na mchepuko basi itakuwa alipapenda sana pia kwa mchepuko hivyo aiendeleze hiyo siri mpaka kifo.
Ushauri tu [emoji120][emoji120]
TEKERI