Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Ushauri: Nitumie mbinu gani kuongea na baba aachane na mchepuko wake?

Pangeni fumanuzi kwa mzee wako na huo mchepuko wake,yaani muwafumanie live na mangoma na matarumbeta,siku ya kwenda kuwafumania mchukueni na mume wa mchepuko wa mzee wako na Mother wako awepo na mjumbe wa mtaa awepo,huo ndio utakua mwisho wao.
😀 😀 😀 😀 😀kumfumania mzee wako unadhani aibu itakuwa ya nani...
 
Pole sana.

Cha muhimu pata taarifa kwa mtu mwingine, hao uliosema walimkalisha Mzee Kikao. Ili ujiridhishe kuwa ni kweli hili suala lipo. Na ujue lipo kwa ukubwa gani..

Baada ya hapo ndipo uone namna ya kumweleza Mzee wako, isiwe mazungumzo emotional bali umwambie kuna tetesi umezisikia Juu yake na huyo 'Mmama' na kwamba unahisi au unaona kuwa zinamuumiza Mamako..

Ikiwezekana; kiume mwambie, hata kama hayo mambo yapo basi ajitahidi isilete Madhara kwenu kama Familia maana litawaumiza hata ninyi wanawe. Naamini atakuelewa na atazingatia ushauri wako.

Usithubutu kutumia hasira, wala emotion kwenye mazungumzo yenu. Maana huwezi jua anapewa nini mpaka anawapuuza wote wanaomshauri..
Nashukuru mkuu.Kama Mungu akinipa ujasiri wakumweleza mzee,unashauri niende kabisa kule kijijini au nitumie njia ya simu.Niko mkoani mbali na nyumbn
 
Siyo rahisi Kama unavyoandika hapa.Mtu kuacha Tabia aliyoizoea msukumo unaanzia ndani yake.Maneno ya kuambiwa peke yake hayajawwhi kumfanya mtu aache Hilo jambo
Tena Mzee anaweza kuona anamvunjia adabu na wakaishia kugombana.Ampige mkwara mzito huyo mchepuko ndy solution.Wanawake Wana Tabia ya woga

Tena amwambie huyo mwanamke ''mamaangu akifa Kwa presha Kwa ajili yako nami nakuua''
Afu changamoto ya kumpiga huyu mchepuko mkwara nikwamba naye nimama mtu mzima, watoto wake tunaheshimiana Kama ndugu.Nahofia kuanzisha mgogor Kati yahizi familia mbili.
Pia rejea pale ambapo mume wa huyu mama anamtetea mkewe kuwa hafanyi hizo Mambo.
 
Halafu unapoomba ushauri usimpangie mtu cha kuchangia vinginevyo jambo lako usingeleta humu.. tafadhali.
Mkuu sikupanga chakuchangiwa.Huwa kun watu huwa wanamaneno yakuumiza badala yafaraja.
Hata hivyo niwie radhi Kama umekereka kwa nilivyotoa angalizo
 
Mkuu hii battle ni ngumu, usijaribu kumtamkia baba yako lolote kuhusu haya mahusiano.

Kama una akili, cheza na huyo mchepuko(japo si vizuri).

Tumia mbinu za kijeshi na kiintelijensia!! Bila kuathiri uhusiano wa Baba na Mama.
Nakazia [emoji4][emoji106]
 
Mchukue mama yako uishi naye umuache huyo baba ahangaike kuchungulia maumbile ya kike atakavyo. Kama kwa umri huo huyo baba alipaswa kutulia na kuwatunzia heshima yenu maana si vyema watoto kusikia habari kama hizo kuhusu baba yao lakini hajafanya hivyo basi ujue ni tabia yake na hataacha. Leo mtamkanya mmoja kesho ataanza na mwingine.
Hii hali ilishanikuta kwa mama yangu nikaichukulia simple lakini sasa najuta maana depression na sonona ilichangia sana kifo cha mama.
Pole kwako ndugu.Haya mambo yanavuruga akili Sana.Wkt mwingine unajikuta nawew unachangamoto binafsi zakindoa then unakutan nachangamoto zandoa ya wazazi.Zote zinakuhitaji.
 
sepema pole sana ila haya mambo usikurupuke ni vigumu kujua ni nini mzee kakosa kwa mama yako lakini pia ina ugumu sana wewe kumueleza mzee hali halisi hata kwa heshima na adabu bado kwake ataiona dharau tu .Sasa ufanye nini ?

Ndugu mambo ya wazazi ni vigumu sana kutatuliwa na watoto hivyo fanya hivi mtafute mzee wako muombe kikao yeye mwenyewe pasipo kumshirikisha yeyote ila yeye tu .

Kaa na mzee wako sasa kama mwanaume mwenzio , mpe madhara ya kuchepuka huku mama yako akiwa anaona live na wanakijiji pia , hivyo katika hitimisho mueleze mzee wako ya kuwa ninyi wote ni wanaume na kuchepuka hakuepukiki kwa kiasi fulani ila sasa muombe abadili mfumo wa uchepukaji kutoka kuwa wazi kwa jamii inayomzunguka mpaka iwe ni siri ya yeye na mchepukaji mwenzie , baada ya hapo muombe na umshukie hata magoti chini ya kuwa akakiri kwa mkewe na kumueleza sasa kaachana na mchepuko na hatorudia tena hivyo yuko na yeye tu .

Kwa kufanya hivyo afya ya mama kimapenzi itahimarika mara dufu hivyo atapata tena hiyo presha ila ukweli wote unaujua wewe na baba yako .

Mwisho mkuu , ikiwa mama yako atajihisi kuwa mwenyewe kuna mabadiliko mzee atayaona kwa mama yako hivyo kama kwa mchepuko alitamani , nakuhakikishia si mda ataachana na mchepuko wake ili aendelee kumfaidi mama yako ila ikiwa basi ajaachana na mchepuko basi itakuwa alipapenda sana pia kwa mchepuko hivyo aiendeleze hiyo siri mpaka kifo.

Ushauri tu [emoji120][emoji120]

TEKERI
Ushauri nimeupokea mkuu.Kuna shangazi yangu(dadaake baba)nilimdokezea.Kwa kuwa nimtu wa dini Sana alichonijibu nikwamba anafunga nakuomba kwa ajili ya hilo jambo na soon Mungu atatenda muujiza.
 
Inaonekana mzee kwenye makuzi yake kuna stage aliiruka ndio kaamua kuiishi sasa uzeeni.
Yani ni balaa me wawili walihama na nyumba kabisaa...mmoja alikuwa na mchepuko anajulikana mpaka na watoto na hao watoto ni watu wazima wana maisha yao lakini huyo mzee hakushtuka hata... wazee wetu ni jambo la kawaida labda case hii sababu huyu mchepuko ni ndugu ila inanishangaza why mme wake hareact???
 
Nilishawahi kushuhudia kesi mbili kama hizo kijijini, ya kwanza mwaka 2010 mtoto mkubwa aliyemaliza form 6 alienda kumpa kipigo heavy yule mchepuko wa baba yake. Baba akataka ampe kipigo mke wake, matokeo yake watoto wakachangia na mama wakampa kipigo mzee.
Walikaa karibia miezi miwili bila kuongea lakini mwisho familia ilikaa vizuri.

Kisa cha pili baada ya baba kuwa na mchepuko, mtoto mkubwa wa baba akaanzisha uhusiano wa mapenzi na mtoto wa mchepuko wa mzee.
Mzee alivyogundua akajisemea yanini! akajiondoa mwenyewe bila shuruti.
 
Back
Top Bottom