Ushauri: Rafiki yangu ni msaliti na mnafiki nimfanyeje?

Ushauri: Rafiki yangu ni msaliti na mnafiki nimfanyeje?

Charlez kanumba

Senior Member
Joined
Nov 2, 2024
Posts
187
Reaction score
501
Nisiwachoshe sana, tabia za huyu rafiki yangu ni hizi.

*Ananizungumzia vibaya kwa masela nikiwa mbali, inafika point anawaambia wajaribu kuanzisha ugomvi na mimi halafu yeye atawalipa pesa.

*Anamponda na kumkosoa kila mwanamke nitakae kuwa nae katika mahusiano ila nikiachana na huyo mwanamke yeye anaanzisha nae mahusiano.

*Hapendi kunitafuta, ila akisikia kuwa nimepewa mchongo wa pesa na mtu, atahakikisha anamjua huyo mtu then ataanza kunigombanisha nae kwa kumwambia maneno mabaya kuhusu mimi.

_Ni rafiki yangu sana huyu msela na hayo matimbwili yake najitahidi sana kuyakwepa ila sasa nimeshindwa, nahitaji ushauri wenu wadau.🙏🙏
 
Wewe na huyo rafiki yako wote mnaonekana bado mna akili za kitoto,ndio nyie vijana wa elfu mbili bila shaka,

Endelea kukua kwanza,jibu la uchukue hatua gani,utalipata mwenyewe tu,

Hapa hata tukikushauri,ni kazi bure tu.
 
Nahitaji namna ya kumkwepa bila kukwazana maana ni rafiki yangu wa karibu sana
Wewe ndio tatizo kubwa kwasababu ni MNAFIKI, rafiki gani wa karibu unayeshindwa kumwambia ukweli badala yake unakimbilia Jamii Forums!?,kama ni rafiki yako kwanini usimweleze aache hiyo tabia!?,. Hapa kuna mawili aidha wewe ni mtoto wa 2000 au huelewi maana ya mtu kuwa rafiki yako wa karibu. Urafiki wa karibu unatoka wapi kwa mtu anayeku snitch!?..
 
Sina la kukushauri labda nikupige Rungu la ugoko

20241029_165603.jpg

JobTrueTrue
 
Wewe ndio tatizo kubwa kwasababu ni MNAFIKI, rafiki gani wa karibu unayeshindwa kumwambia ukweli badala yake unakimbilia Jamii Forums!?,kama ni rafiki yako kwanini usimweleze aache hiyo tabia!?,. Hapa kuna mawili aidha wewe ni mtoto wa 2000 au huelewi maana ya mtu kuwa rafiki yako wa karibu. Urafiki wa karibu unatoka wapi kwa mtu anayeku snitch!?..
Mleta mada hajui nini maana ya rafiki,

Anachanganya Rafiki na Mtu unayejuana naye,aidha coz ulisoma nae au ni jirani yako,

Unafanyiwa yote hayo ila unaendelea tu kusema kua huyo ni rafiki yako!!
 
Wewe ndio tatizo kubwa kwasababu ni MNAFIKI, rafiki gani wa karibu unayeshindwa kumwambia ukweli badala yake unakimbilia Jamii Forums!?,kama ni rafiki yako kwanini usimweleze aache hiyo tabia!?,. Hapa kuna mawili aidha wewe ni mtoto wa 2000 au huelewi maana ya mtu kuwa rafiki yako wa karibu. Urafiki wa karibu unatoka wapi kwa mtu anayeku snitch!?..

Nikisema nimfuate direct nimwambie lazima tutakuwa maadui na mm sitaki tuwe maadui.
 
Nikisema nimfuate direct nimwambie lazima tutakuwa maadui na mm sitaki tuwe maadui.
Ndio maana nikasema wewe ndo tatizo, umewahi kujiuliza na yeye anaogopa kupoteza urafiki na wewe!?,kama anaogopa kwanini anakufanyia u snitch!?,na kama haogopi kwanini ung'ang'anie urafiki nae!?.. Kuna jamaa kadai huna akili hapo juu, yawezekana akawa sahihi.
 
Back
Top Bottom