Ushauri: Rafiki yangu ni msaliti na mnafiki nimfanyeje?

Ushauri: Rafiki yangu ni msaliti na mnafiki nimfanyeje?

Nisiwachoshe sana, tabia za huyu rafiki yangu ni hizi.

*Ananizungumzia vibaya kwa masela nikiwa mbali, inafika point anawaambia wajaribu kuanzisha ugomvi na mimi halafu yeye atawalipa pesa.

*Anamponda na kumkosoa kila mwanamke nitakae kuwa nae katika mahusiano ila nikiachana na huyo mwanamke yeye anaanzisha nae mahusiano.

*Hapendi kunitafuta, ila akisikia kuwa nimepewa mchongo wa pesa na mtu, atahakikisha anamjua huyo mtu then ataanza kunigombanisha nae kwa kumwambia maneno mabaya kuhusu mimi.

_Ni rafiki yangu sana huyu msela na hayo matimbwili yake najitahidi sana kuyakwepa ila sasa nimeshindwa, nahitaji ushauri wenu wadau.🙏🙏
Wewe kweli ni mwalimu wa Mamenkwa wote duniani, yaani pamoja na vituko vyote hivi anavyokufanyia huyu menkwa bado unamuweka kwenye kundi la rafiki?
 
Back
Top Bottom