Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 1,018
- 2,366
Kwa kawaida chura hasikii..
Sembuse chura kiziwi?
Sembuse chura kiziwi?
Sio lazima awe tundu tu.Halafu TUNDU aje kuwa rais au wale makenge wa dodoma?
HAKUNA HATA MOJA AMBALO UMEONGEA SAMIA ANAWEZA KULIFANYA KI UKWELI ...SAMIA ANACHO JARIBU KUFANYA NI KUBUY TIME TU YA KUENDELEA KUBAKI MADARAKANIMheshimiwa Rais Samia Suluhu, kwa mujibu wa Katiba na sheria, tayari umeapishwa kuongoza nchi. Hata hivyo, katika sayansi ya siasa (wasomi watanirekebisha), kuna tofauti kubwa kati ya "Legality" (Uhalali wa Kisheria) na "Legitimacy" (Kukubalika na Umma).
Tanzania kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kuliko vyote tangu uhuru (Wazee watanisaidia zaidi). Matukio ya Oktoba 29 na kabla na baada ya siku hiyo (Vifo, ukatili, na kuzimwa kwa mawasiliano) yameacha kidonda kibichi. Hali ya sasa, ambapo viongozi wa dini na siasa wanahubiri chuki za wazi ("kuchinja", "ubaguzi wa kidini"), ni ishara ya "State Fragility" (Dola iliyo hatarini kuporomoka).
Mhe. Rais, Desemba 9 inakaribia. Nchi haiwezi kuhimili tena "Oktoba 29" nyingine. Uchumi wetu utaporomoka, na heshima yetu kimataifa itafutika. Kama kijana wa Kitanzania Chukua hatua hizi nne (4) za haraka ili kutuliza hasira za umma na kunusuru Taifa:
1. Kiri Tatizo na Uondoe Kinga kwa Waliohusika na Mauaji (Accountability)
Hasira iliyopo mtaani siyo tu kwa sababu ya kura, bali ni kwa sababu ya DAMU. Hakuna mzazi anayeweza kusahau mtoto wake aliyeuawa au kupotea kisa uchaguzi ama serikali..
- Ushauri: Achana na Tume za kuchunguza kwa miaka. Chukua hatua zinazoonekana sasa. Wale wote (Polisi au Usalama) waliotumia nguvu iliyopitiliza watajwe na wasimamishwe kazi hadharani.
- Faida: Hii itapunguza kiu ya "kisasi" kwa wananchi. Itaonyesha kuwa Dola haibariki mauaji. Bila 'Accountability', wananchi watajichukulia sheria mkononi.
2. Tangaza Mchakato wa KATIBA MPYA wenye Tarehe (Time-Bound Roadmap)
Kiapo chako kimekulinda kisheria, lakini hakijafuta hitaji la mabadiliko ya mfumo. Sababu kuu ya watu kutaka kuandamana ni hisia kwamba "Njia za kisheria zimefungwa".
- Ushauri: Badala ya kusema "mchakato utaanza", tangaza Roadmap yenye tarehe kamili. Mfano: "Kufikia June 2026 tutakuwa na Rasimu Mpya" Na hapa tukitumia Ile ya jaji Warioba ni rahisi kuiboresha kidogo tu..
- Faida: Hii inawapa watu "Matumaini ya Kesho" (Hope for the future). Watu wenye matumaini hawaandamani kuvunja nchi; wanasubiri mabadiliko waliyoahidiwa. Hii ndiyo "Soft Landing" pekee ya kisiasa iliyobaki.
3. Kemea Vikali "Wapambe" Wanaochochea Udini na Chuki
Kosa kubwa linalofanyika sasa ni baadhi ya viongozi (wa dini na serikali) wanaojifanya wanakutetea kwa kutumia lugha za vitisho ("tutawachinja", "sisi wa imani hii dhidi ya wale").
- Ushauri: Mhe. Rais, jitokeze hadharani WAKEMEE watu hawa, hata kama wako upande wako. Waambie kuwa wewe ni Rais wa Watanzania wote, si wa dini moja au chama kimoja.
- Faida: Hii itarudisha imani kwa wale wanaohisi wametengwa. Nchi ikigawanyika kidini, hakuna jeshi litakaloweza kuituliza. Udini ni saratani itakayomaliza utawala wako haraka kuliko maandamano.
4. 'General Amnesty': Futa Kesi za Kisiasa na Uachie Wafungwa
Kuweka watu ndani kwa makosa ya kisiasa au "kubambikiza" kesi za uhaini n.k hakuzuii maandamano, bali kunayatengeneza.
Nahitimisha kwa kusema...
- Ushauri: Tumia mamlaka yako kutoa msamaha kwa makosa yenye asili ya kisiasa yaliyotokana na uchaguzi huu (Kabla, wakati na Baada).
- Faida: Hii inaitwa "De-escalation Strategy". Unapunguza joto la nchi,, Unawapa watu sababu ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo badala ya kwenda barabarani.
Mheshimiwa Rais, Dunia inatuangalia, wawekezaji hawaweki fedha kwenye nchi ambayo wananchi wanapigwa risasi barabarani, Uchumi wetu utakufa, na tutageuka kuwa ombaomba.
Usisikilize wanaokuambia "Piga tu, watazoea" Historia inaonyesha nguvu ya umma ikifikia kikomo, hakuna risasi inayotosha,Tumia Busara (Wisdom) badala ya Nguvu (Force). Niliwahi kusema "siku wa kufa wakipatikana kama waliotayari kuuwa walivyosasa itakuwa ni hatari kubwa, na sasa wa kufa wapo tayari wamepatikana"
Mama Nakushauri kama mwanao anavyoweza kukushauri....
Okoa Desemba 9 yetu. Okoa Tanzania yetu.
Wako katika Ujenzi wa Taifa,
(Mtanzania888i)
Hili ndio jibu hasa linalohitajika5.Aachie madaraka kwa kujiuzulu kwani sio rais halali wa nchi yetu.
Hana ridhaa ya wananchi wengi pia uchaguzi uliomuingiza madarakani haukuwa wa haki na huru.
Hivi mnajua mchakato wa katiba kuwa si kitu cha kukalisha ati wabunge etc ni kupata watu ambao wanaweza kuwa neutral bila kuweka maslahi yao mbele. Kwa watanzania ninaowajua, tutatengenezewa kama ile ya JK. Mpaka sasa tunampongeza Warioba kusimamia hili ingawa Policy Takers waliikataa, kwa vile haikuwa inaakisi maslahi yao.Mheshimiwa Rais Samia Suluhu, kwa mujibu wa Katiba na sheria, tayari umeapishwa kuongoza nchi. Hata hivyo, katika sayansi ya siasa (wasomi watanirekebisha), kuna tofauti kubwa kati ya "Legality" (Uhalali wa Kisheria) na "Legitimacy" (Kukubalika na Umma).
Tanzania kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kuliko vyote tangu uhuru (Wazee watanisaidia zaidi). Matukio ya Oktoba 29 na kabla na baada ya siku hiyo (Vifo, ukatili, na kuzimwa kwa mawasiliano) yameacha kidonda kibichi. Hali ya sasa, ambapo viongozi wa dini na siasa wanahubiri chuki za wazi ("kuchinja", "ubaguzi wa kidini"), ni ishara ya "State Fragility" (Dola iliyo hatarini kuporomoka).
Mhe. Rais, Desemba 9 inakaribia. Nchi haiwezi kuhimili tena "Oktoba 29" nyingine. Uchumi wetu utaporomoka, na heshima yetu kimataifa itafutika. Kama kijana wa Kitanzania Chukua hatua hizi nne (4) za haraka ili kutuliza hasira za umma na kunusuru Taifa:
1. Kiri Tatizo na Uondoe Kinga kwa Waliohusika na Mauaji (Accountability)
Hasira iliyopo mtaani siyo tu kwa sababu ya kura, bali ni kwa sababu ya DAMU. Hakuna mzazi anayeweza kusahau mtoto wake aliyeuawa au kupotea kisa uchaguzi ama serikali..
- Ushauri: Achana na Tume za kuchunguza kwa miaka. Chukua hatua zinazoonekana sasa. Wale wote (Polisi au Usalama) waliotumia nguvu iliyopitiliza watajwe na wasimamishwe kazi hadharani.
- Faida: Hii itapunguza kiu ya "kisasi" kwa wananchi. Itaonyesha kuwa Dola haibariki mauaji. Bila 'Accountability', wananchi watajichukulia sheria mkononi.
2. Tangaza Mchakato wa KATIBA MPYA wenye Tarehe (Time-Bound Roadmap)
Kiapo chako kimekulinda kisheria, lakini hakijafuta hitaji la mabadiliko ya mfumo. Sababu kuu ya watu kutaka kuandamana ni hisia kwamba "Njia za kisheria zimefungwa".
- Ushauri: Badala ya kusema "mchakato utaanza", tangaza Roadmap yenye tarehe kamili. Mfano: "Kufikia June 2026 tutakuwa na Rasimu Mpya" Na hapa tukitumia Ile ya jaji Warioba ni rahisi kuiboresha kidogo tu..
- Faida: Hii inawapa watu "Matumaini ya Kesho" (Hope for the future). Watu wenye matumaini hawaandamani kuvunja nchi; wanasubiri mabadiliko waliyoahidiwa. Hii ndiyo "Soft Landing" pekee ya kisiasa iliyobaki.
3. Kemea Vikali "Wapambe" Wanaochochea Udini na Chuki
Kosa kubwa linalofanyika sasa ni baadhi ya viongozi (wa dini na serikali) wanaojifanya wanakutetea kwa kutumia lugha za vitisho ("tutawachinja", "sisi wa imani hii dhidi ya wale").
- Ushauri: Mhe. Rais, jitokeze hadharani WAKEMEE watu hawa, hata kama wako upande wako. Waambie kuwa wewe ni Rais wa Watanzania wote, si wa dini moja au chama kimoja.
- Faida: Hii itarudisha imani kwa wale wanaohisi wametengwa. Nchi ikigawanyika kidini, hakuna jeshi litakaloweza kuituliza. Udini ni saratani itakayomaliza utawala wako haraka kuliko maandamano.
4. 'General Amnesty': Futa Kesi za Kisiasa na Uachie Wafungwa
Kuweka watu ndani kwa makosa ya kisiasa au "kubambikiza" kesi za uhaini n.k hakuzuii maandamano, bali kunayatengeneza.
Nahitimisha kwa kusema...
- Ushauri: Tumia mamlaka yako kutoa msamaha kwa makosa yenye asili ya kisiasa yaliyotokana na uchaguzi huu (Kabla, wakati na Baada).
- Faida: Hii inaitwa "De-escalation Strategy". Unapunguza joto la nchi,, Unawapa watu sababu ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo badala ya kwenda barabarani.
Mheshimiwa Rais, Dunia inatuangalia, wawekezaji hawaweki fedha kwenye nchi ambayo wananchi wanapigwa risasi barabarani, Uchumi wetu utakufa, na tutageuka kuwa ombaomba.
Usisikilize wanaokuambia "Piga tu, watazoea" Historia inaonyesha nguvu ya umma ikifikia kikomo, hakuna risasi inayotosha,Tumia Busara (Wisdom) badala ya Nguvu (Force). Niliwahi kusema "siku wa kufa wakipatikana kama waliotayari kuuwa walivyosasa itakuwa ni hatari kubwa, na sasa wa kufa wapo tayari wamepatikana"
Mama Nakushauri kama mwanao anavyoweza kukushauri....
Okoa Desemba 9 yetu. Okoa Tanzania yetu.
Wako katika Ujenzi wa Taifa,
(Mtanzania888i)
Kabisa kama tukiweza kuanzia kwa Ile ya Warioba ilikuwa ni nzuri na Bado ni nzuri...maana kuuanza mchakato kutokea mwanzo ni ishu ... Watu wapo ila kupewa nafasi na kuruhusiwa Kisha watakacholeta kukubaliwa na waliopo juu ndiyo shida shida si watu maana waliotengeneza rasimu ya Warioba ni watanzania na wapo Bado watanzania Bora tuHivi mnajua mchakato wa katiba kuwa si kitu cha kukalisha ati wabunge etc ni kupata watu ambao wanaweza kuwa neutral bila kuweka maslahi yao mbele. Kwa watanzania ninaowajua, tutatengenezewa kama ile ya JK. Mpaka sasa tunampongeza Warioba kusimamia hili ingawa Policy Takers waliikataa, kwa vile haikuwa inaakisi maslahi yao.