PostGE2025 Ushauri: Rais, ili kuepusha ‘D9’ kuwa siku ya damu na kuanguka kwa uchumi, zingatia haya manne

PostGE2025 Ushauri: Rais, ili kuepusha ‘D9’ kuwa siku ya damu na kuanguka kwa uchumi, zingatia haya manne

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wewe ni mpumbavu nini? Afanye yote hayo kama nani? Yule ni mpumbavu tu aliyejipa mamlaka kinyemela, lazima atoke apende asipende kmmk.
Sijui km ni sahihi lakini kwa mtazamo wangu hata akiondoka kama hatuna mfumo mzuri atakayekuja ni walewale....tupate katiba Bora ambayo inamlazimu kila mmoja kuifuata hata akitoka tunauwezo wa kusema hatufai na huyu pia hatufai.... Ukiisoma katiba unachoka maana hata haya maandamano hayana maana kwenye katiba kwasababu anayeitwa Rais ananguvu na Mamlaka makubwa kiasi kwamba akisema hakuna maandamano ni hayapo hata km katiba imeruhusu.
 
Kwahiyo kwa kipindi hicho chote za harakati za kuanda huo uchaguzi mpya tena huru na wa haki nchi inakuwa inaongozwa na nani wakati huo?
Inaongozwa na Spika wa Bunge aliyemaliza mda wake huyu aliyechaguliwa nae Zungu la Unga ni mbunge Batili
 
Endapo maandamano ya tarehe9/12/2025 yatashindwa kumtoa mama abduli madarakani basi waandamanaji inabidi tukanunue chuma za moto AK47 tuanze mapambano ya jino Kwa jino Hadi atoke aende kwao.
 
tafuta mda upate supu saf unawaza siasa sana, ccm utaondoka utaiacha
Baada ya tarehe 9D urudi hapa. Kama wewe mwenyewe ama bwanako anakula kwa mgongo wa ccm mwambie atafute kazi nyingine.
 
Ukikaa ukatafakari kwa kina uzao wetu Mungu alishaacha maisha yaende vile utashi wa mwanadamu inavyoendesha mambo,mambo mengi hata upige goti vipi hata jema haliwi.
 
Nchi itakuwa chini ya spika wa bunge.

Na wala usiogope kuhusu kuandaa uchaguzi mpya.

Linawezekana kabisa.

Uchaguzi wa 2015 baada ya CCM kushindwa Zanzibar Jecha akaufuta uchaguzi na wakaandaa uchaguzi mpya.

Kwahiyo kuandaa uchaguzi mpya sio jambo geni sana.
Spika Naye hakupatikana Kwa haki , hivyo Jaji Mkuu ndio atakayo endesha sirikali
 
IMG_20251124_084208_076.jpg


✊🏽🇹🇿 #D9 is the date. Peaceful protest to demand accountability, justice and #SamiaMustGo


🇹🇿 Gen-Z, tukutane December 9th. #MD9 #RudiTanganyika


#SamiaMustGo #TanzaniaMassacre #FreeTunduLissu #wakeupTanzania #FreePolepoleNow #struggle_for_africa #riseupTanzania #tanzania ⚠️🇹🇿
 

Attachments

  • IMG_20251124_084208_076.jpg
    IMG_20251124_084208_076.jpg
    78 KB · Views: 21
MKUU HAPO NAONGEZEA HILI MOJA KUBWA KULIKO YOTE:
ATOKE HADHARANI AKEMEE UTEKAJI NA APIGE MARUFUKU UTEKAJI MARA MOJA!
UTEKAJI NDIO JANGA KUBWA KULIKO YOTE KWA SASA MPAKA MUDA HUU BADO WATU WANATEKWA KIMYA KIMYA YAANI HAIPITI WEEK WATU KADHAA WANATEKWA
Unadhani ni rahisi mchungaji mzinzi kukemea uzinzi kanisani kwake?.
 
Utekaji siku hizi unatekelezwa kila siku. Huu ujinga unafaa kukomeshwa mara moja, na watekaji woote wasukumwe ndani na kufunguliwa kesi za mauaji
Utakemewaje ikiwa mkuu wa nchi kabariki hiyo Hali hivi umewahi kumuona mama akikemea utekaji?
 
Sijui km ni sahihi lakini kwa mtazamo wangu hata akiondoka kama hatuna mfumo mzuri atakayekuja ni walewale....tupate katiba Bora ambayo inamlazimu kila mmoja kuifuata hata akitoka tunauwezo wa kusema hatufai na huyu pia hatufai.... Ukiisoma katiba unachoka maana hata haya maandamano hayana maana kwenye katiba kwasababu anayeitwa Rais ananguvu na Mamlaka makubwa kiasi kwamba akisema hakuna maandamano ni hayapo hata km katiba imeruhusu.
Mama ndio chanzo ya yote kufika hapa tulipo alishataadhalishwa Kabla hata ya maandamano na watu tofauti tofauti na kina Polepole ambaye alimshauri kwa busara na hekima bila hata kutumia matusi au lugha Kali ila mama akampuuza, Gwajima pia lakini akapuuzwa.kwenye matukio ya utekaji mama kaa kimya Kama sio raisi wa nchi, issue ya udini imetokea lakini yupo kimya na bahati nzuri wananchi wenyewe kwa umoja wao wameuzima. Haya maandamano yameshatokea nikategemea atasawazisha makosa yake lakini ndio Kwanza anachochea moto hivi ndugu yangu unakuaje na raisi ambaye hajui uwajibikaji wake? Hii ndio maana watu hawamtaki
 
MKUU HAPO NAONGEZEA HILI MOJA KUBWA KULIKO YOTE:
ATOKE HADHARANI AKEMEE UTEKAJI NA APIGE MARUFUKU UTEKAJI MARA MOJA!
UTEKAJI NDIO JANGA KUBWA KULIKO YOTE KWA SASA MPAKA MUDA HUU BADO WATU WANATEKWA KIMYA KIMYA YAANI HAIPITI WEEK WATU KADHAA WANATEKWA
Hii ndo itarudisha waliotekwa mtaani?
Waliouwawa kuwa hai?
Maiti zilizopotea kupatikana?
Mungu ampe busara Rais wetu akae pembeni. Nadhani ndio tiba pekee.
Huku mitaani malalamiko ni mengi, sioni jinsi ya kurudisha imani kwa watu bila uwajibikaji wa mkuu mwenyewe kuwajibika.
 
Naona wiki iliyopita walihamisha mada kwa kumuua pilipili, wiki hii moto umerudi pale pale 😄😄😄 chura kazi anayo , itabidi waue celebrity mwingine ili walau mpk D9 kuwe kumepoa na maandamano yafie hapo,, teh teh teh
 

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu, kwa mujibu wa Katiba na sheria, tayari umeapishwa kuongoza nchi. Hata hivyo, katika sayansi ya siasa (wasomi watanirekebisha), kuna tofauti kubwa kati ya "Legality" (Uhalali wa Kisheria) na "Legitimacy" (Kukubalika na Umma).

Tanzania kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kuliko vyote tangu uhuru (Wazee watanisaidia zaidi). Matukio ya Oktoba 29 na kabla na baada ya siku hiyo (Vifo, ukatili, na kuzimwa kwa mawasiliano) yameacha kidonda kibichi. Hali ya sasa, ambapo viongozi wa dini na siasa wanahubiri chuki za wazi ("kuchinja", "ubaguzi wa kidini"), ni ishara ya "State Fragility" (Dola iliyo hatarini kuporomoka).

Mhe. Rais, Desemba 9 inakaribia. Nchi haiwezi kuhimili tena "Oktoba 29" nyingine. Uchumi wetu utaporomoka, na heshima yetu kimataifa itafutika. Kama kijana wa Kitanzania Chukua hatua hizi nne (4) za haraka ili kutuliza hasira za umma na kunusuru Taifa:

1. Kili tatizo na Uondoe Kinga kwa Waliohusika na Mauaji (Accountability)​

Hasira iliyopo mtaani siyo tu kwa sababu ya kura, bali ni kwa sababu ya DAMU. Hakuna mzazi anayeweza kusahau mtoto wake aliyeuawa au kupotea kisa uchaguzi ama serikali..
  • Ushauri: Achana na Tume za kuchunguza kwa miaka. Chukua hatua zinazoonekana sasa. Wale wote (Polisi au Usalama) waliotumia nguvu iliyopitiliza watajwe na wasimamishwe kazi hadharani.
  • Faida: Hii itapunguza kiu ya "kisasi" kwa wananchi. Itaonyesha kuwa Dola haibariki mauaji. Bila 'Accountability', wananchi watajichukulia sheria mkononi.

2. Tangaza Mchakato wa KATIBA MPYA wenye Tarehe (Time-Bound Roadmap)​

Kiapo chako kimekulinda kisheria, lakini hakijafuta hitaji la mabadiliko ya mfumo. Sababu kuu ya watu kutaka kuandamana ni hisia kwamba "Njia za kisheria zimefungwa".
  • Ushauri: Badala ya kusema "mchakato utaanza", tangaza Roadmap yenye tarehe kamili. Mfano: "Kufikia June 2026 tutakuwa na Rasimu Mpya" Na hapa tukitumia Ile ya jaji Warioba ni rahisi kuiboresha kidogo tu..
  • Faida: Hii inawapa watu "Matumaini ya Kesho" (Hope for the future). Watu wenye matumaini hawaandamani kuvunja nchi; wanasubiri mabadiliko waliyoahidiwa. Hii ndiyo "Soft Landing" pekee ya kisiasa iliyobaki.

3. Kemea Vikali "Wapambe" Wanaochochea Udini na Chuki​

Kosa kubwa linalofanyika sasa ni baadhi ya viongozi (wa dini na serikali) wanaojifanya wanakutetea kwa kutumia lugha za vitisho ("tutawachinja", "sisi wa imani hii dhidi ya wale").
  • Ushauri: Mhe. Rais, jitokeze hadharani WAKEMEE watu hawa, hata kama wako upande wako. Waambie kuwa wewe ni Rais wa Watanzania wote, si wa dini moja au chama kimoja.
  • Faida: Hii itarudisha imani kwa wale wanaohisi wametengwa. Nchi ikigawanyika kidini, hakuna jeshi litakaloweza kuituliza. Udini ni saratani itakayomaliza utawala wako haraka kuliko maandamano.

4. 'General Amnesty': Futa Kesi za Kisiasa na Uachie Wafungwa​

Kuweka watu ndani kwa makosa ya kisiasa au "kubambikiza" kesi za uhaini n.k hakuzuii maandamano, bali kunayatengeneza.
  • Ushauri: Tumia mamlaka yako kutoa msamaha kwa makosa yenye asili ya kisiasa yaliyotokana na uchaguzi huu (Kabla, wakati na Baada).
  • Faida: Hii inaitwa "De-escalation Strategy". Unapunguza joto la nchi,, Unawapa watu sababu ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo badala ya kwenda barabarani.
Nahitimisha kwa kusema...
Mheshimiwa Rais, Dunia inatuangalia, wawekezaji hawaweki fedha kwenye nchi ambayo wananchi wanapigwa risasi barabarani, Uchumi wetu utakufa, na tutageuka kuwa ombaomba.

Usisikilize wanaokuambia "Piga tu, watazoea" Historia inaonyesha nguvu ya umma ikifikia kikomo, hakuna risasi inayotosha,Tumia Busara (Wisdom) badala ya Nguvu (Force). Niliwahi kusema "siku wa kufa wakipatikana kama waliotayari kuuwa walivyosasa itakuwa ni hatari kubwa, na sasa wa kufa wapo tayari wamepatikana"

Mama Nakushauri kama mwanao anavyoweza kukushauri....

Okoa Desemba 9 yetu. Okoa Tanzania yetu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
(Mtanzania888i)
Ushauri mzuri ila kwa kibri yake unadhani atazingatia!?
 
5.Aachie madaraka kwa kujiuzulu kwani sio rais halali wa nchi yetu.

Hana ridhaa ya wananchi wengi pia uchaguzi uliomuingiza madarakani haukuwa wa haki na huru.
Atafanyaje yote hayo wakati yeye ndio aliyewatuma,na ameingia madarakani kwa UONGO?
 
Tetea upumbavu tuu, sio nchi ya Samia ile ni ya wote, future generations zita suffer kwa ajiri ya Wapuuzi kama wewe, your stupidity and ideas must be defeated
umeongea lini na hao future generation, una uhakika hawataki bia?
 
Wewe umerukwa na akili kwelikweli; bado unaiwaza CCM tena wakati huu?

CCM ipi tena, wakati Samia na Genge lake wamekwisha izika. Unadhani baada ya mauaji haya bado mtawadanganaya waTanzania mliowapora chama chao muendelee kukitumia kufanya uovu
unapoteza mda na usipoangalia unaweza kupoteza uhai pia
 
Back
Top Bottom