PostGE2025 Ushauri: Rais, ili kuepusha ‘D9’ kuwa siku ya damu na kuanguka kwa uchumi, zingatia haya manne

PostGE2025 Ushauri: Rais, ili kuepusha ‘D9’ kuwa siku ya damu na kuanguka kwa uchumi, zingatia haya manne

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kama lengo la Samia ni kupata pesa, basi naomba tumchangie kiasi chochote anachokitaka halafu atupishe. Vinginevyo tarehe 9D atafurushwa kwa aibu kubwa.

Samia hatakiwi na watanzania. Kwann anang'ang'ania?
 
Screenshot_20240723_161411_Photo Editor.jpg
 
Kama lengo la Samia ni kupata pesa, basi naomba tumchangie kiasi chochote anachokitaka halafu atupishe. Vinginevyo tarehe 9D atafurushwa kwa aibu kubwa.

Samia hatakiwi na watanzania. Kwann anang'ang'ania?
Naona umeamua tu kuanzisha mada ambayo kiuhalisia hukubaliani nayo wewe mwenyewe.

Utaanzia wapi kumchangia pesa mtu mwovu kama huyu?

Wewe unafikiri pesa aliyokwisha changiwa na mafisadi na uuzaji wa Bandari na mali nyingine za taifa hili hazimtoshi kama angependa kuondoka kwenye mateso haya aliyojitengenezea mwenyewe?

Huyu mwanamke hana hiari tena ya kufanya uamzi kama unavyosema wewe.

Kinachombakisha hapo sasa hivi siyo pesa tena.
 
Kama lengo la Samia ni kupata pesa, basi naomba tumchangie kiasi chochote anachokitaka halafu atupishe. Vinginevyo tarehe 9D atafurushwa kwa aibu kubwa.

Samia hatakiwi na watanzania. Kwann anang'ang'ania?
tafuta mda upate supu saf unawaza siasa sana, ccm utaondoka utaiacha
 
tafuta mda upate supu saf unawaza siasa sana, ccm utaondoka utaiacha
Wewe umerukwa na akili kwelikweli; bado unaiwaza CCM tena wakati huu?

CCM ipi tena, wakati Samia na Genge lake wamekwisha izika. Unadhani baada ya mauaji haya bado mtawadanganaya waTanzania mliowapora chama chao muendelee kukitumia kufanya uovu wenu kwao?
 
Ushauri mzuri sana ila Dkt Samia nadhani ana majini na hayo majini kuna mtu anayaongoza kufanya maamuzi yake yeye ila siyo yule Samia wa 2021. Tunachokiona leo siyo tu ni ujinga na upumbavu uliopotiliza bali siyo utanzania hata kodogo. Mpaka huyo jini aliyepo ndani yake atolewe labda anaweza jitambua. Hivyo ushauri wako ni HAUWEZI KUTEKELEZWA majini yake yanaamini lazima yamwage damu tena ili kumharibia zaidi
😃😃Alianza vizuri kweli kweli ndiyo waswahili walisema Ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka
 
View attachment 3506160

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu, kwa mujibu wa Katiba na sheria, tayari umeapishwa kuongoza nchi. Hata hivyo, katika sayansi ya siasa (wasomi watanirekebisha), kuna tofauti kubwa kati ya "Legality" (Uhalali wa Kisheria) na "Legitimacy" (Kukubalika na Umma).

Tanzania kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kuliko vyote tangu uhuru (Wazee watanisaidia zaidi). Matukio ya Oktoba 29 na kabla na baada ya siku hiyo (Vifo, ukatili, na kuzimwa kwa mawasiliano) yameacha kidonda kibichi. Hali ya sasa, ambapo viongozi wa dini na siasa wanahubiri chuki za wazi ("kuchinja", "ubaguzi wa kidini"), ni ishara ya "State Fragility" (Dola iliyo hatarini kuporomoka).

Mhe. Rais, Desemba 9 inakaribia. Nchi haiwezi kuhimili tena "Oktoba 29" nyingine. Uchumi wetu utaporomoka, na heshima yetu kimataifa itafutika. Kama kijana wa Kitanzania Chukua hatua hizi nne (4) za haraka ili kutuliza hasira za umma na kunusuru Taifa:

1. Kiri Tatizo na Uondoe Kinga kwa Waliohusika na Mauaji (Accountability)​

Hasira iliyopo mtaani siyo tu kwa sababu ya kura, bali ni kwa sababu ya DAMU. Hakuna mzazi anayeweza kusahau mtoto wake aliyeuawa au kupotea kisa uchaguzi ama serikali..
  • Ushauri: Achana na Tume za kuchunguza kwa miaka. Chukua hatua zinazoonekana sasa. Wale wote (Polisi au Usalama) waliotumia nguvu iliyopitiliza watajwe na wasimamishwe kazi hadharani.
  • Faida: Hii itapunguza kiu ya "kisasi" kwa wananchi. Itaonyesha kuwa Dola haibariki mauaji. Bila 'Accountability', wananchi watajichukulia sheria mkononi.

2. Tangaza Mchakato wa KATIBA MPYA wenye Tarehe (Time-Bound Roadmap)​

Kiapo chako kimekulinda kisheria, lakini hakijafuta hitaji la mabadiliko ya mfumo. Sababu kuu ya watu kutaka kuandamana ni hisia kwamba "Njia za kisheria zimefungwa".
  • Ushauri: Badala ya kusema "mchakato utaanza", tangaza Roadmap yenye tarehe kamili. Mfano: "Kufikia June 2026 tutakuwa na Rasimu Mpya" Na hapa tukitumia Ile ya jaji Warioba ni rahisi kuiboresha kidogo tu..
  • Faida: Hii inawapa watu "Matumaini ya Kesho" (Hope for the future). Watu wenye matumaini hawaandamani kuvunja nchi; wanasubiri mabadiliko waliyoahidiwa. Hii ndiyo "Soft Landing" pekee ya kisiasa iliyobaki.

3. Kemea Vikali "Wapambe" Wanaochochea Udini na Chuki​

Kosa kubwa linalofanyika sasa ni baadhi ya viongozi (wa dini na serikali) wanaojifanya wanakutetea kwa kutumia lugha za vitisho ("tutawachinja", "sisi wa imani hii dhidi ya wale").
  • Ushauri: Mhe. Rais, jitokeze hadharani WAKEMEE watu hawa, hata kama wako upande wako. Waambie kuwa wewe ni Rais wa Watanzania wote, si wa dini moja au chama kimoja.
  • Faida: Hii itarudisha imani kwa wale wanaohisi wametengwa. Nchi ikigawanyika kidini, hakuna jeshi litakaloweza kuituliza. Udini ni saratani itakayomaliza utawala wako haraka kuliko maandamano.

4. 'General Amnesty': Futa Kesi za Kisiasa na Uachie Wafungwa​

Kuweka watu ndani kwa makosa ya kisiasa au "kubambikiza" kesi za uhaini n.k hakuzuii maandamano, bali kunayatengeneza.
  • Ushauri: Tumia mamlaka yako kutoa msamaha kwa makosa yenye asili ya kisiasa yaliyotokana na uchaguzi huu (Kabla, wakati na Baada).
  • Faida: Hii inaitwa "De-escalation Strategy". Unapunguza joto la nchi,, Unawapa watu sababu ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo badala ya kwenda barabarani.
Nahitimisha kwa kusema...
Mheshimiwa Rais, Dunia inatuangalia, wawekezaji hawaweki fedha kwenye nchi ambayo wananchi wanapigwa risasi barabarani, Uchumi wetu utakufa, na tutageuka kuwa ombaomba.

Usisikilize wanaokuambia "Piga tu, watazoea" Historia inaonyesha nguvu ya umma ikifikia kikomo, hakuna risasi inayotosha,Tumia Busara (Wisdom) badala ya Nguvu (Force). Niliwahi kusema "siku wa kufa wakipatikana kama waliotayari kuuwa walivyosasa itakuwa ni hatari kubwa, na sasa wa kufa wapo tayari wamepatikana"

Mama Nakushauri kama mwanao anavyoweza kukushauri....

Okoa Desemba 9 yetu. Okoa Tanzania yetu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
(Mtanzania888i)
Wewe ni mpumbavu nini? Afanye yote hayo kama nani? Yule ni mpumbavu tu aliyejipa mamlaka kinyemela, lazima atoke apende asipende kmmk.
 
Back
Top Bottom