PostGE2025 Ushauri: Rais, ili kuepusha ‘D9’ kuwa siku ya damu na kuanguka kwa uchumi, zingatia haya manne

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sina shida na picha ya mtu mwovu ambaye kajimaliza kwa kukosa akili kichwani mwake.

Huyu mwanamke ni boya kwelikweli kutumia kijinga namna hii?
wewe ambae hujakosa akili imekusaidia nn mpaka leo?
 
unapoteza mda na usipoangalia unaweza kupoteza uhai pia
Kukukumbusha hali yako duni, hilo halinipi shida.
Kuhusu uhai wangu, kama utapotea kwa ukombozi wa Tanzania,, hiyo ni kheri kubwa kwangu na jambo la kujivunia. Hata hivyo, nimekwisha kueleza mara kadhaa, watu pekee ambao uhai wao uko mashakani ni Samia Suluhu Hassan na Genge lake lote, pamoja na nguruwe wawafugao kama wewe.
 
wewe ambae hujakosa akili imekusaidia nn mpaka leo?
Ninajitambua kama mTanzania ninayejivunia hadhi hiyo; ndiyo maana nguruwe kama ulivyo wewe ni muhimu muelezwe mzijue hali zenu mbovu zilivyo.

Hamuwezi kuwaua waTanzania halafu mnakuja humu JF kuwasimanga hao hao mlio waua. Hii ni akili au tamaduni ya wapi hii?
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu, kwa mujibu wa Katiba na sheria, tayari umeapishwa kuongoza nchi. Hata hivyo, katika sayansi ya siasa (wasomi watanirekebisha), kuna tofauti kubwa kati ya "Legality" (Uhalali wa Kisheria) na "Legitimacy" (Kukubalika na Umma).

Tanzania kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kuliko vyote tangu uhuru (Wazee watanisaidia zaidi). Matukio ya Oktoba 29 na kabla na baada ya siku hiyo (Vifo, ukatili, na kuzimwa kwa mawasiliano) yameacha kidonda kibichi. Hali ya sasa, ambapo viongozi wa dini na siasa wanahubiri chuki za wazi ("kuchinja", "ubaguzi wa kidini"), ni ishara ya "State Fragility" (Dola iliyo hatarini kuporomoka).

Mhe. Rais, Desemba 9 inakaribia. Nchi haiwezi kuhimili tena "Oktoba 29" nyingine. Uchumi wetu utaporomoka, na heshima yetu kimataifa itafutika. Kama kijana wa Kitanzania Chukua hatua hizi nne (4) za haraka ili kutuliza hasira za umma na kunusuru Taifa:

1. Kili tatizo na Uondoe Kinga kwa Waliohusika na Mauaji (Accountability)​

Hasira iliyopo mtaani siyo tu kwa sababu ya kura, bali ni kwa sababu ya DAMU. Hakuna mzazi anayeweza kusahau mtoto wake aliyeuawa au kupotea kisa uchaguzi ama serikali..
  • Ushauri: Achana na Tume za kuchunguza kwa miaka. Chukua hatua zinazoonekana sasa. Wale wote (Polisi au Usalama) waliotumia nguvu iliyopitiliza watajwe na wasimamishwe kazi hadharani.
  • Faida: Hii itapunguza kiu ya "kisasi" kwa wananchi. Itaonyesha kuwa Dola haibariki mauaji. Bila 'Accountability', wananchi watajichukulia sheria mkononi.

2. Tangaza Mchakato wa KATIBA MPYA wenye Tarehe (Time-Bound Roadmap)​

Kiapo chako kimekulinda kisheria, lakini hakijafuta hitaji la mabadiliko ya mfumo. Sababu kuu ya watu kutaka kuandamana ni hisia kwamba "Njia za kisheria zimefungwa".
  • Ushauri: Badala ya kusema "mchakato utaanza", tangaza Roadmap yenye tarehe kamili. Mfano: "Kufikia June 2026 tutakuwa na Rasimu Mpya" Na hapa tukitumia Ile ya jaji Warioba ni rahisi kuiboresha kidogo tu..
  • Faida: Hii inawapa watu "Matumaini ya Kesho" (Hope for the future). Watu wenye matumaini hawaandamani kuvunja nchi; wanasubiri mabadiliko waliyoahidiwa. Hii ndiyo "Soft Landing" pekee ya kisiasa iliyobaki.

3. Kemea Vikali "Wapambe" Wanaochochea Udini na Chuki​

Kosa kubwa linalofanyika sasa ni baadhi ya viongozi (wa dini na serikali) wanaojifanya wanakutetea kwa kutumia lugha za vitisho ("tutawachinja", "sisi wa imani hii dhidi ya wale").
  • Ushauri: Mhe. Rais, jitokeze hadharani WAKEMEE watu hawa, hata kama wako upande wako. Waambie kuwa wewe ni Rais wa Watanzania wote, si wa dini moja au chama kimoja.
  • Faida: Hii itarudisha imani kwa wale wanaohisi wametengwa. Nchi ikigawanyika kidini, hakuna jeshi litakaloweza kuituliza. Udini ni saratani itakayomaliza utawala wako haraka kuliko maandamano.

4. 'General Amnesty': Futa Kesi za Kisiasa na Uachie Wafungwa​

Kuweka watu ndani kwa makosa ya kisiasa au "kubambikiza" kesi za uhaini n.k hakuzuii maandamano, bali kunayatengeneza.
  • Ushauri: Tumia mamlaka yako kutoa msamaha kwa makosa yenye asili ya kisiasa yaliyotokana na uchaguzi huu (Kabla, wakati na Baada).
  • Faida: Hii inaitwa "De-escalation Strategy". Unapunguza joto la nchi,, Unawapa watu sababu ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo badala ya kwenda barabarani.
Nahitimisha kwa kusema...
Mheshimiwa Rais, Dunia inatuangalia, wawekezaji hawaweki fedha kwenye nchi ambayo wananchi wanapigwa risasi barabarani, Uchumi wetu utakufa, na tutageuka kuwa ombaomba.

Usisikilize wanaokuambia "Piga tu, watazoea" Historia inaonyesha nguvu ya umma ikifikia kikomo, hakuna risasi inayotosha,Tumia Busara (Wisdom) badala ya Nguvu (Force). Niliwahi kusema "siku wa kufa wakipatikana kama waliotayari kuuwa walivyosasa itakuwa ni hatari kubwa, na sasa wa kufa wapo tayari wamepatikana"

Mama Nakushauri kama mwanao anavyoweza kukushauri....

Okoa Desemba 9 yetu. Okoa Tanzania yetu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
(Mtanzania888i)
Ushauri mzuri ila yule ni chura kiziwe remember?
 
Hapo yeye ajiuzulu ndio tiba ya matatizo yote. Atawafunga polisi waliopiga risasi wananchi vipi wakati amri ilitoka kwake??
Akiachia ngazi tu kelele zote hizi zinaisha. Watanzania hawamkubali kabisaaa. Na alikuwa na nafasi ya kurekebisha hili, ila akaendekeza ushosti na watu mfano Angela Kiziga. Akaendekeza ufalme, kumuachia nchi mtoto. Akaendekeza kubabaika kwa ‘matajiri’ /wahindi na waarabu na kuwaachia wafanye watakavyo. Nchi imekuwa shaghala baghala. Wananchi wanaona mwiba wa tatizo ni yeye tu.
 
Huyu maza kakosa washauri.
Mwanzo alianza vizuri na wote walioumizws na utawala wa Magu waliona kama wamepata tumaini jipya na hivi ni mwanamke kila mtu alimpenda.

Shida alipoanza kusikiliza wahuni na kuacha nchi iendeshwe kama haina kiongozi. Wananchi walivyoanza kuongea kuhusu utekaji akapuuzia akafanya mambo yote yaliyo sirini yaibuke..!!

Angesikiliza wananchi na kukemea utekaji na mauaji wala asingepata wa kumsumbua na urais wake.
Na Nchi kuigeuza ya familia na washkaji zake ndio kafanya watu tuzidi kumkataa!!
Ajiuzulu tumemkataa.
 
Ninajitambua kama mTanzania ninayejivunia hadhi hiyo; ndiyo maana nguruwe kama ulivyo wewe ni muhimu muelezwe mzijue hali zenu mbovu zilivyo.

Hamuwezi kuwaua waTanzania halafu mnakuja humu JF kuwasimanga hao hao mlio waua. Hii ni akili au tamaduni ya wapi hii?
kwahio kuna watu waliokata moto uku online? uku wote ni wajinga kazi yao kuambia watu waende mstari wa mbele wao wakiwa wanabonyeza button
 
Kukukumbusha hali yako duni, hilo halinipi shida.
Kuhusu uhai wangu, kama utapotea kwa ukombozi wa Tanzania,, hiyo ni kheri kubwa kwangu na jambo la kujivunia. Hata hivyo, nimekwisha kueleza mara kadhaa, watu pekee ambao uhai wao uko mashakani ni Samia Suluhu Hassan na Genge lake lote, pamoja na nguruwe wawafugao kama wewe.
basi sawa acha tuendelee kula mpake pale mtakapotutimua
 
Huko kula ukijuwa kuna kitanzi shingoni kinachosubiri kukazwa ni kula gani huko?
Mna wakati mgumu sana mnaopitia sasa hivi.
 
kwahio kuna watu waliokata moto uku online? uku wote ni wajinga kazi yao kuambia watu waende mstari wa mbele wao wakiwa wanabonyeza button
Akili yako imekuwa ya kitoto sana, bila shaka kutokana na madhara ya kutoa roho za watu. Kabla hujaondoka dunia hii utakuwa umeteseka sana.
 
mbona rahisi sana yaaan kwa watu wasifanye machafuko wala kuandamana ni kwa mamlaka kutambua huu wakat gani wajisalimishe kwa mamlaka kuuu kuliko zote kama kuna mtu yupo jiran tu na yeyote aliyepo jiran na Rais anitafute dm .... .....nitawapa siri hii ....
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu, kwa mujibu wa Katiba na sheria, tayari umeapishwa kuongoza nchi. Hata hivyo, katika sayansi ya siasa (wasomi watanirekebisha), kuna tofauti kubwa kati ya "Legality" (Uhalali wa Kisheria) na "Legitimacy" (Kukubalika na Umma).

Tanzania kwa sasa inapita katika kipindi kigumu kuliko vyote tangu uhuru (Wazee watanisaidia zaidi). Matukio ya Oktoba 29 na kabla na baada ya siku hiyo (Vifo, ukatili, na kuzimwa kwa mawasiliano) yameacha kidonda kibichi. Hali ya sasa, ambapo viongozi wa dini na siasa wanahubiri chuki za wazi ("kuchinja", "ubaguzi wa kidini"), ni ishara ya "State Fragility" (Dola iliyo hatarini kuporomoka).

Mhe. Rais, Desemba 9 inakaribia. Nchi haiwezi kuhimili tena "Oktoba 29" nyingine. Uchumi wetu utaporomoka, na heshima yetu kimataifa itafutika. Kama kijana wa Kitanzania Chukua hatua hizi nne (4) za haraka ili kutuliza hasira za umma na kunusuru Taifa:

1. Kili tatizo na Uondoe Kinga kwa Waliohusika na Mauaji (Accountability)​

Hasira iliyopo mtaani siyo tu kwa sababu ya kura, bali ni kwa sababu ya DAMU. Hakuna mzazi anayeweza kusahau mtoto wake aliyeuawa au kupotea kisa uchaguzi ama serikali..
  • Ushauri: Achana na Tume za kuchunguza kwa miaka. Chukua hatua zinazoonekana sasa. Wale wote (Polisi au Usalama) waliotumia nguvu iliyopitiliza watajwe na wasimamishwe kazi hadharani.
  • Faida: Hii itapunguza kiu ya "kisasi" kwa wananchi. Itaonyesha kuwa Dola haibariki mauaji. Bila 'Accountability', wananchi watajichukulia sheria mkononi.

2. Tangaza Mchakato wa KATIBA MPYA wenye Tarehe (Time-Bound Roadmap)​

Kiapo chako kimekulinda kisheria, lakini hakijafuta hitaji la mabadiliko ya mfumo. Sababu kuu ya watu kutaka kuandamana ni hisia kwamba "Njia za kisheria zimefungwa".
  • Ushauri: Badala ya kusema "mchakato utaanza", tangaza Roadmap yenye tarehe kamili. Mfano: "Kufikia June 2026 tutakuwa na Rasimu Mpya" Na hapa tukitumia Ile ya jaji Warioba ni rahisi kuiboresha kidogo tu..
  • Faida: Hii inawapa watu "Matumaini ya Kesho" (Hope for the future). Watu wenye matumaini hawaandamani kuvunja nchi; wanasubiri mabadiliko waliyoahidiwa. Hii ndiyo "Soft Landing" pekee ya kisiasa iliyobaki.

3. Kemea Vikali "Wapambe" Wanaochochea Udini na Chuki​

Kosa kubwa linalofanyika sasa ni baadhi ya viongozi (wa dini na serikali) wanaojifanya wanakutetea kwa kutumia lugha za vitisho ("tutawachinja", "sisi wa imani hii dhidi ya wale").
  • Ushauri: Mhe. Rais, jitokeze hadharani WAKEMEE watu hawa, hata kama wako upande wako. Waambie kuwa wewe ni Rais wa Watanzania wote, si wa dini moja au chama kimoja.
  • Faida: Hii itarudisha imani kwa wale wanaohisi wametengwa. Nchi ikigawanyika kidini, hakuna jeshi litakaloweza kuituliza. Udini ni saratani itakayomaliza utawala wako haraka kuliko maandamano.

4. 'General Amnesty': Futa Kesi za Kisiasa na Uachie Wafungwa​

Kuweka watu ndani kwa makosa ya kisiasa au "kubambikiza" kesi za uhaini n.k hakuzuii maandamano, bali kunayatengeneza.
  • Ushauri: Tumia mamlaka yako kutoa msamaha kwa makosa yenye asili ya kisiasa yaliyotokana na uchaguzi huu (Kabla, wakati na Baada).
  • Faida: Hii inaitwa "De-escalation Strategy". Unapunguza joto la nchi,, Unawapa watu sababu ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo badala ya kwenda barabarani.
Nahitimisha kwa kusema...
Mheshimiwa Rais, Dunia inatuangalia, wawekezaji hawaweki fedha kwenye nchi ambayo wananchi wanapigwa risasi barabarani, Uchumi wetu utakufa, na tutageuka kuwa ombaomba.

Usisikilize wanaokuambia "Piga tu, watazoea" Historia inaonyesha nguvu ya umma ikifikia kikomo, hakuna risasi inayotosha,Tumia Busara (Wisdom) badala ya Nguvu (Force). Niliwahi kusema "siku wa kufa wakipatikana kama waliotayari kuuwa walivyosasa itakuwa ni hatari kubwa, na sasa wa kufa wapo tayari wamepatikana"

Mama Nakushauri kama mwanao anavyoweza kukushauri....

Okoa Desemba 9 yetu. Okoa Tanzania yetu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
(Mtanzania888i)
Na awape watu maiti zao wakazike kwa heshima ilo nalo ni miongoni mwa sababu za D9#
 
Back
Top Bottom