Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025


Hao hao system unaosema wanafanya mabadiliko, ndio wafaidika kwa mfumo huu huu wenye matundu kibao. Kama hao watu wa mfumo wanapatikana kwa njia zisizo wazi bali kwa kujuana, urafiki, wizi, undugu nk, unategemea mabadiliko gani?
 
Mnyonge atoke wapi Tanzania hii wakati ndo walipa tozo? Mikono salama kwa bilioni 600+ za sensa ya mwezi mmoja tu huku bajeti za wizara fulani hazifiki hata nusu yake kwa mwaka mzima.
Sensa inafanyika kila baada ya miaka kumi hivyo bajeti take ilikuwepo, sensa Ni muhimu katika mipango kazi ya kimaendeleo, unasema sensa gharama halafu unakuta hapo hapo unataka katiba utazani yenyewe siyo gharama au utazani utafanya mwenyewe kwa hela zako
 
Kama wezi wa kodi zetu awachukuliwi hatua sababu ya udhaifu wa uongozi kwann tuhisi tunalipa Ili kunufaisha walamba asali.
 

Ingia kwenye link ya Twaweza uone kama wananchi walisema wanakubaliana na hizo tozo. Unafuata upotoshaji unaofanywa na chawa wa mama ndio unafanya ni utafiti wa Twaweza?
 
Hao hao system unaosema wanafanya mabadiliko, ndio wafaidika kwa mfumo huu huu wenye matundu kibao. Kama hao watu wa mfumo wanapatikana kwa njia zisizo wazi bali kwa kujuana, urafiki, wizi, undugu nk, unategemea mabadiliko gani?
Sawa lakini akiamua Rais litafanyika tuu,hapa Tzn Rais ndio anaweka muelekeo wa Nchi.
 

Hatuwezi kufanya mikutano maana hatuna silaha za kupambana na vyombo vya dola, lakini mikutano iko kisheria. Kama yeye ni mwanamke kweli, ajitokeze azuie hiyo mikutano bila vyombo vya dola. Akae mbele yeye na watoto wake kuzuia hiyo mikutano iliyoko kisheria
 
Sensa sio ujinga na haiwezi kuwa ujinga, jisomee faida zake ujionee

Nadhani hujamuelewa ila umeamua kujibu tu. Hajasema siyo mhimu na wala haina faida
Tangu na kabla ya uhuru tumekuwa na sensa kila baada ya miaka 10. Wote wenye umri kuanzia 30 na kuendelea wanakumbuka jinsi tulivyokuwa tunahesabiwa hata mashuleni.
Mara ya mwisho nakumbuka tulihesabiwa 2013 na kwenye nyumba tulikuwa watatu. Tuliulizwa kama kuna mtu alilala hapa kwetu kama swali lilivyokuwa linauliza nakumbuka.
Wanaobeza sensa ni watoto ambao yawezekana walikuwa na wanaishi maisha ambayo hawana makazi maalum au ni watoto ambao sensa ya mwisho walikuwa chekechea.
Tuwasamehe.
 
Kelele nyingi kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Huu ni.uongo uliopitiliza.

Mkapa, kikwete na Magufuli walisemwa sana na kutukanwa kila aina ya tusi. Mama Samia Kama kiongozi lazima pia apitie hayo ni ngumu watu wote kumsema kwa mazuri, haiwezekani.

Kikukwa aendelee na kazi na asisikie kelele.
 
Misingi ya kutegemea kudra na hisani za kiongozi ili kupata suluhu ya matatizo yetu ndo chanzo mpaka Sasa tupo hapa tulipo pasi kuzingatia sheria na kanuni zinataka nini au zina toa muongozo gani kuhusu jambo hilo.kama taifa ni muda Sasa kuunda misingi bora ya kuzingatia sheria na kanuni kwa kuweka mifumo imara yenye uwajibikaji na kila mtu anapaswa kuwajibika kulingana na sheria na kanuni.

Tabia za kuona viongozi Kama miungu watu ndo imeleta shida mbalimbali mfano leo hii shida ya kukatika kwa umeme hovyo hovyo lawama zote kwa rais ,ufisadi katika miradi mbalimbali ya umma lawama zote kwa rais wakati Kuna TAKUKURU na muda huo huo ana wasaidizi kibao chini yake hili ni zao la katiba yetu ambapo rais anapewa nguvu katika kila kitu hivyo jambo lolote ili lifanyiwe kazi lazima pawepo msukumo wa kauli ya rais.

mfumo wa check and balance haupo katika nchi yetu hivyo dhana ya uwajibikaji wa kila mihimiri ya serikali kuwa hovyo.
 
Jehanamu zimebadilika tu sura. Sa hivi ni jehamu ya kulia huko huko ulipo, mpinga tozo si katimliwa kazi kuna uhuru hapo? Ndugai si alisema ipo siku nchi itapigwa mnada yuko wapi sa hv? Muamala mmoja sa hv unaweza kukamliwa hata mara 3 kwa tozo. Yule aliwaliza wanasiasa zaidi ila huyu anawaliza wananchi kwa tozo.
 
Sawa lakini akiamua Rais litafanyika tuu,hapa Tzn Rais ndio anaweka muelekeo wa Nchi.

Hilo la rais kuweka muelekeo wa nchi ndio limetufikisha hapa. Kila rais akiingia anaongoza kwa utashi wake na genge lake. Ndio maana tunataka katiba mpya ili utashi wa rais usiwe dira ya nchi.

Leo hii inakuwa ngumu kupata uwekezaji wa maana, kwani sera za nchi ni tabia binafsi za rais. Hali hiyo haifanyi muwekezaji serious kuwekeza, maana hajui rais ajaye atakuwa na tabia zipi. Tungekuwa na marais wanaoingia madarakani kwa ridhaa ya umma wangalau wangefanya watakavyo wananchi, lakini hao wanaoingizwa madarakani na kundi dogo lijiitalo system, tutabaki hapa hapa na maendeleo ya propaganda. Unakuta maendeleo kiuhalisia ni sungura, lakini sifa zake unaweza kudhani ni tembo.
 
Ndio ilivyo kote huko hata Duniani ndio maana ya kuwa na manifesto za vyama.
 
Hukumbuki kitu. Ilikuwa 2012, na hakuna aliyeibeza sensa. Bajeti ya wizara ya mifugo na uvuvi ni chini ya bilion 500 kwa mwaka mzima lkn sensa ya watu na makazi inayochukua mwezi mmoja tu mchakato wake kukamilika ni bilion 600+
 
Mimi nakuunga mkono kwa zaidi ya 200%
Shida ya nchi hii ni chawa

Chawa wapi wengi kuliko watendajii

As well as walamba asali.

Wai ngoja nipige mapambiooo


Wee angalia hii thread ulioianzisha.
Wapo ambao kwa makusudi wanadiriki kusema serikali haikuletei chakula .

Bila kujua sera ngumu inaweza kukwamisha kupata chakula.

Leo kila kitu bei juu ,hatujakaa sawa
Tozo.

Mfano

Mshahara wa mtumishi unable kodi ngapi

Moja Paye
Pili SDL
tatu sijui chama
Nne tozo benki akati PAYE Ashakata

Mishahara yenyewe ndio kuongezeana 12,000

Double taxation
 
Sema ''wewe'' na siyo ''sisi''. Au kama wewe na familia yako mnaona hivyo basi ni ruksa
 
Ndio ilivyo kote huko hata Duniani ndio maana ya kuwa na manifesto za vyama.
Siyo kweli bongo tu. Uingereza mfumo ulitoka kumwajibisha waziri mkuu juzi tu hapa, unasemaje ndo ilivyo kote duniani? Wengine viongozi wako answerable kwenye mfuno lkn huku kwetu viongozi / mfumo uko answerable kwa rais.
 
Kipimo cha utimamu wa uongozi wako ni well-being ya watu wako. Kama watu wako 90% awamudu basic needs wewe sio kiongozi unaabisha taaluma ya uongozi
 
Mkuu mbona unazunguka sana,ushasema udhaifu wake wote alafu unasema 2025 apumzike!!!
"SAA YA KUPUMZIKA SAMIA NI SASA 2022"
 
Akifanya hivyo, atakuwa amejiwekea heshima, kuliko kuondolewa kitini kwa nguvu ya umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…