Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Hata hivyo mama atawanyoosha tuu subiria apate mrejesho wa namna ya kuboresha utendaji Kazi wa Public service na Vyombo vya dola..

Mama ameshasema atakata bil.500 zinazopotea kwa uncessary expenditure na Amesema atafuta mashirika na kuunganisha mengine..

So systems are working wewe subiria mda utapata majibu tuu..

Hao hao system unaosema wanafanya mabadiliko, ndio wafaidika kwa mfumo huu huu wenye matundu kibao. Kama hao watu wa mfumo wanapatikana kwa njia zisizo wazi bali kwa kujuana, urafiki, wizi, undugu nk, unategemea mabadiliko gani?
 
Mnyonge atoke wapi Tanzania hii wakati ndo walipa tozo? Mikono salama kwa bilioni 600+ za sensa ya mwezi mmoja tu huku bajeti za wizara fulani hazifiki hata nusu yake kwa mwaka mzima.
Sensa inafanyika kila baada ya miaka kumi hivyo bajeti take ilikuwepo, sensa Ni muhimu katika mipango kazi ya kimaendeleo, unasema sensa gharama halafu unakuta hapo hapo unataka katiba utazani yenyewe siyo gharama au utazani utafanya mwenyewe kwa hela zako
 
Watanzania Tupo Tayari kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe, Sasa wewe Kama hutaki kutoa Kodi na Tozo unataka Nani akujengee nchi yako, unataka Nani akupe ili wewe utumie huduma utakavyo wewe, unataka watoto wako wakapate wapi huduma ikiwa wewe Kama mzazi hutaki kubeba mzigo utakao leta matunda kwa wanao

Unazani hao wa ulaya waliyapokea maendeleo Kama kuangua tunda mtini, lazima tuwajibike kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe, mh Rais wetu ameongoza njia hiyo hatuna budi kumpongeza na kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa, tutakuwa tegemezi mpaka lini,tutarishwa mpaka lini, tutahudumiwa mpaka lini, chini ya mama yetu tunataka tuijenge Tanzania Yetu kwa mikono yetu wenyewe

Asali ndio hizi huduma ambazo tumesogezewa karibu yetu na mh Rais wetu mpendwa, juhudi za mh Rais wetu katika kutuinua kiuchumi Ni kubwa Sana na tunapaswa kumuunga mkono Rais wetu, hatupaswi kumkatisha tamaa Bali kumpa faraja maana amejitolea kututumikia watanzania kwa nguvu zake zote
Kama wezi wa kodi zetu awachukuliwi hatua sababu ya udhaifu wa uongozi kwann tuhisi tunalipa Ili kunufaisha walamba asali.
 
Hujasikia utafiti wa twaweza, sisi tumekubali kulipa maana tunachohitaji Ni maendeleo na katika Hilo tunampongeza Sana mh Rais wetu mpendwa maana tunayaona matunda ya tozo zetu kwa kuwa tunaona miradi mbalimbali ikijengwa kutokanaa na tozo zetu, mama tunaendelea kumuunga mkono Sana tu na bado Tunamuhitaji ili aendelee kutuongoza watanzania

Ingia kwenye link ya Twaweza uone kama wananchi walisema wanakubaliana na hizo tozo. Unafuata upotoshaji unaofanywa na chawa wa mama ndio unafanya ni utafiti wa Twaweza?
 
Hao hao system unaosema wanafanya mabadiliko, ndio wafaidika kwa mfumo huu huu wenye matundu kibao. Kama hao watu wa mfumo wanapatikana kwa njia zisizo wazi bali kwa kujuana, urafiki, wizi, undugu nk, unategemea mabadiliko gani?
Sawa lakini akiamua Rais litafanyika tuu,hapa Tzn Rais ndio anaweka muelekeo wa Nchi.
 
Hizi hadithi mlianza kuongea toka Machi mwaka 2021..

Saizi mumesogeza mbele hadi lini niweke Kumbukumbu sawa?

Kama nyie ni wanaume fanyeni mikutano ya Hadhara tuwaone..

Tumetoa mfano mdogo kwa yule aliyejifanya kupinga tozo, serikali ikitoa msimamo wiki ijayo tutaanza kunyooka na wote.

Hatuwezi kufanya mikutano maana hatuna silaha za kupambana na vyombo vya dola, lakini mikutano iko kisheria. Kama yeye ni mwanamke kweli, ajitokeze azuie hiyo mikutano bila vyombo vya dola. Akae mbele yeye na watoto wake kuzuia hiyo mikutano iliyoko kisheria
 
Sensa sio ujinga na haiwezi kuwa ujinga, jisomee faida zake ujionee

Nadhani hujamuelewa ila umeamua kujibu tu. Hajasema siyo mhimu na wala haina faida
Tangu na kabla ya uhuru tumekuwa na sensa kila baada ya miaka 10. Wote wenye umri kuanzia 30 na kuendelea wanakumbuka jinsi tulivyokuwa tunahesabiwa hata mashuleni.
Mara ya mwisho nakumbuka tulihesabiwa 2013 na kwenye nyumba tulikuwa watatu. Tuliulizwa kama kuna mtu alilala hapa kwetu kama swali lilivyokuwa linauliza nakumbuka.
Wanaobeza sensa ni watoto ambao yawezekana walikuwa na wanaishi maisha ambayo hawana makazi maalum au ni watoto ambao sensa ya mwisho walikuwa chekechea.
Tuwasamehe.
 
Kelele nyingi kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
Huu ni.uongo uliopitiliza.

Mkapa, kikwete na Magufuli walisemwa sana na kutukanwa kila aina ya tusi. Mama Samia Kama kiongozi lazima pia apitie hayo ni ngumu watu wote kumsema kwa mazuri, haiwezekani.

Kikukwa aendelee na kazi na asisikie kelele.
 
Misingi ya kutegemea kudra na hisani za kiongozi ili kupata suluhu ya matatizo yetu ndo chanzo mpaka Sasa tupo hapa tulipo pasi kuzingatia sheria na kanuni zinataka nini au zina toa muongozo gani kuhusu jambo hilo.kama taifa ni muda Sasa kuunda misingi bora ya kuzingatia sheria na kanuni kwa kuweka mifumo imara yenye uwajibikaji na kila mtu anapaswa kuwajibika kulingana na sheria na kanuni.

Tabia za kuona viongozi Kama miungu watu ndo imeleta shida mbalimbali mfano leo hii shida ya kukatika kwa umeme hovyo hovyo lawama zote kwa rais ,ufisadi katika miradi mbalimbali ya umma lawama zote kwa rais wakati Kuna TAKUKURU na muda huo huo ana wasaidizi kibao chini yake hili ni zao la katiba yetu ambapo rais anapewa nguvu katika kila kitu hivyo jambo lolote ili lifanyiwe kazi lazima pawepo msukumo wa kauli ya rais.

mfumo wa check and balance haupo katika nchi yetu hivyo dhana ya uwajibikaji wa kila mihimiri ya serikali kuwa hovyo.
 
Unataka kuturudisha jehanam! Watu tumekuwa tunasema Ee mwenyezi mwenye rehema mpe huyu dada afya nzuri ili tuwe naye kwa miaka mitano zaidi.
Wewe unayeandika haya, ungethubutu kuandika haya ungepotea kama Ben Saa nane au Azori.

Waulize watu walivyoswekwa lupango bila makosa na mtu aliyekuwa anamtumia MUNGU wetu kwa dhihaka?
Jehanamu zimebadilika tu sura. Sa hivi ni jehamu ya kulia huko huko ulipo, mpinga tozo si katimliwa kazi kuna uhuru hapo? Ndugai si alisema ipo siku nchi itapigwa mnada yuko wapi sa hv? Muamala mmoja sa hv unaweza kukamliwa hata mara 3 kwa tozo. Yule aliwaliza wanasiasa zaidi ila huyu anawaliza wananchi kwa tozo.
 
Sawa lakini akiamua Rais litafanyika tuu,hapa Tzn Rais ndio anaweka muelekeo wa Nchi.

Hilo la rais kuweka muelekeo wa nchi ndio limetufikisha hapa. Kila rais akiingia anaongoza kwa utashi wake na genge lake. Ndio maana tunataka katiba mpya ili utashi wa rais usiwe dira ya nchi.

Leo hii inakuwa ngumu kupata uwekezaji wa maana, kwani sera za nchi ni tabia binafsi za rais. Hali hiyo haifanyi muwekezaji serious kuwekeza, maana hajui rais ajaye atakuwa na tabia zipi. Tungekuwa na marais wanaoingia madarakani kwa ridhaa ya umma wangalau wangefanya watakavyo wananchi, lakini hao wanaoingizwa madarakani na kundi dogo lijiitalo system, tutabaki hapa hapa na maendeleo ya propaganda. Unakuta maendeleo kiuhalisia ni sungura, lakini sifa zake unaweza kudhani ni tembo.
 
Hilo la rais kuweka muelekeo wa nchi ndio limetufikisha hapa. Kila rais akiingia anaongoza kwa utashi wake na genge lake. Ndio maana tunataka katiba mpya ili utashi wa rais usiwe dira ya nchi.

Leo hii inakuwa ngumu kupata uwekezaji wa maana, kwani sera za nchi ni tabia binafsi za rais. Hali hiyo haifanyi muwekezaji serious kuwekeza, maana hajui rais ajaye atakuwa na tabia zipi. Tungekuwa na marais wanaoingia madarakani kwa ridhaa ya umma wangalau wangefanya watakavyo wananchi, lakini hao wanaoingizwa madarakani na kundi dogo lijiitalo system, tutabaki hapa hapa na maendeleo ya propaganda. Unakuta maendeleo kiuhalisia ni sungura, lakini sifa zake unaweza kudhani ni tembo.
Ndio ilivyo kote huko hata Duniani ndio maana ya kuwa na manifesto za vyama.
 
Tangu na kabla ya uhuru tumekuwa na sensa kila baada ya miaka 10. Wote wenye umri kuanzia 30 na kuendelea wanakumbuka jinsi tulivyokuwa tunahesabiwa hata mashuleni.
Mara ya mwisho nakumbuka tulihesabiwa 2013 na kwenye nyumba tulikuwa watatu. Tuliulizwa kama kuna mtu alilala hapa kwetu kama swali lilivyokuwa linauliza nakumbuka.
Wanaobeza sensa ni watoto ambao yawezekana walikuwa na wanaishi maisha ambayo hawana makazi maalum au ni watoto ambao sensa ya mwisho walikuwa chekechea.
Tuwasamehe.
Hukumbuki kitu. Ilikuwa 2012, na hakuna aliyeibeza sensa. Bajeti ya wizara ya mifugo na uvuvi ni chini ya bilion 500 kwa mwaka mzima lkn sensa ya watu na makazi inayochukua mwezi mmoja tu mchakato wake kukamilika ni bilion 600+
 
Kwa mtazamo wangu binafsi napendekeza Rais wetu Mama Samia apumzike mwaka 2025 kama analo wazo la kuendelea kutuongoza.

Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.

Ila shida yake ipo kwenye kuchukua hatua juu ya watu wanaomzunguka na kufanya mambo ya hovyo katika utawala wake.

Naunga mkono michakato yote ya kodi inayoanzishwa kufanyika Ila shida ipo kwenye matumizi yake ni jinsi gani tunaitumia hiyo pesa inayopatikana kwenye kodi, mfano serikali kwa ujinga imetumia bilioni 629 kwenye zoezi la sensa pekee huu ni ufisadi.

Zoezi lenyewe watu wengi bado hawajahesabiwa mpaka sasa. Leo ni siku ya 6 ndani ya zile siku saba zilizopangwa maana yake kesho ni siku ya mwisho. Zoezi limegubikwa na wizi na ufisadi wakati zoezi lingewatumia mabalozi wa nyumba kumi tu na mwenyekiti wa kijiji lingekuwa limeshakamilika kwa 100%.

wangetumia karatasi za kawaida kujaza taarifa za watu, then kwenye kata ndio wangeweka mfumo wa TEHAMA wa kuingiza zile taarifa kwa kutumia tablet tungefanikiwa kwa 100%

Kukwama kwa zoezi la katiba na tume huru ya uchaguzi kabla ya 2025, ili nalo ni donda ndugu. Watu wanakushauri kwamba utashindwa uchaguzi 2025 ukileta sasa Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Wanakudanganya ungeweka mazingira sawa ya uchaguzi na katiba lazima watu wangukupigia kura 2025 ili kulipa mema uliyowafanyia hata kama wasingekuchagua mema yako yangeandikwa duniani na mbinguni.

Swala ya mfumuko wa bei ndio bomu kuu, watu hawakatai kwamba vitu vinapanda duniani lakini watu wanachokataa ni kwanini vitu muhimu ndio vipande tu kwani vitu vingine ambavyo havipandi vitu havisafirishwi?

Mfano unakuta kiberiti kinauzwa shilingi 100 Tanzania nzima hakipandi bei zaidi ya miaka 10, wakati na chenyewe kinatumia mafuta kuzalishwa. Ila Ngano, mafuta ya kula na sembe inapanda kila muda kila mwaka.

Utasikia usafirishaji, kwanini mafuta ya alizeti yanayozalishwa Rukwa na Singida hapo hapo kiwandani ukiyafuata yana bei ile ile kama unayoinunua Dar es salaam?

Mh. Rais hapa tukubaliane kwamba umeshindwa ku control inflation kwa sasa, mwezi umepita mafuta yanashuka kila siku kwenye soko la dunia kwanini sisi mafuta yanazidi kupanda tu?

Kwanini uwashughulikii wafanyabiashara Ili waache ulafi wa kutaka faida kubwa?

Tofauti yetu na Zanzibar iko wapi, kwanini Zanzibar kila kitu kinachoingizwa kwenye visiwa hivyo bei zake zipo chini, hata bei zao za mafuta zipo chini kuliko sisi au ndio kusema Zanzibar ni taifa tofauti na sisi?

Basi Kama hivyo Rais Mwinyi ana uwezo wa kupambana na mfumuko wa bei vile, bora tumchukue aje atusaidie huku bara baada ya 2025.

Mambo ni mengi, Ila naomba nikushauri kama unahitaji heshima ya milele basi pumzika 2025 aje mtu mwingine afanye kazi ya Urais. Inawezekana watu wanakushauri vibaya kwa sababu haukuchaguliwa na wananchi ili kukuchonganisha kwa watanzania.
Mimi nakuunga mkono kwa zaidi ya 200%
Shida ya nchi hii ni chawa

Chawa wapi wengi kuliko watendajii

As well as walamba asali.

Wai ngoja nipige mapambiooo


Wee angalia hii thread ulioianzisha.
Wapo ambao kwa makusudi wanadiriki kusema serikali haikuletei chakula .

Bila kujua sera ngumu inaweza kukwamisha kupata chakula.

Leo kila kitu bei juu ,hatujakaa sawa
Tozo.

Mfano

Mshahara wa mtumishi unable kodi ngapi

Moja Paye
Pili SDL
tatu sijui chama
Nne tozo benki akati PAYE Ashakata

Mishahara yenyewe ndio kuongezeana 12,000

Double taxation
 
Sisi tunaona anafanya vizuri mh Rais wetu maana tunapata huduma bila usumbufu na tunaona namna anavyoongoza nchi kwa kufuata misingi ya kisheria na utawala Bora , Kama unamaoni yako kuhusu katiba nenda Katoe kwenye kikosi kazi huko utasikiliza,

Mama yupo kazini na tumeridhishwa na utendaji kazi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watu, mtuachie Rais wetu aendelee kututumikia sisi mamilioni ya watanzania tunaomuunga mkono
Sema ''wewe'' na siyo ''sisi''. Au kama wewe na familia yako mnaona hivyo basi ni ruksa
 
Ndio ilivyo kote huko hata Duniani ndio maana ya kuwa na manifesto za vyama.
Siyo kweli bongo tu. Uingereza mfumo ulitoka kumwajibisha waziri mkuu juzi tu hapa, unasemaje ndo ilivyo kote duniani? Wengine viongozi wako answerable kwenye mfuno lkn huku kwetu viongozi / mfumo uko answerable kwa rais.
 
Kipimo cha utimamu wa uongozi wako ni well-being ya watu wako. Kama watu wako 90% awamudu basic needs wewe sio kiongozi unaabisha taaluma ya uongozi
 
Mkuu mbona unazunguka sana,ushasema udhaifu wake wote alafu unasema 2025 apumzike!!!
"SAA YA KUPUMZIKA SAMIA NI SASA 2022"
 
Akifanya hivyo, atakuwa amejiwekea heshima, kuliko kuondolewa kitini kwa nguvu ya umma.
 
Back
Top Bottom